What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Hapo unamaanisha ulichoandika au otherwise?
 
ushauri mzuri sana hata kama sio kweli, anatakiwa awe makini sana
 
Dr slaa aliwahi kusema majimbo yanayoongozwa na chadema yatakuwa mfano wa kuigwa sasa tujiulize hilo limefanyika?
 

Watu wanapima ufanisi ili kufikia maamuzi ya ama kupigia kura CDM 2015 au la. Kama ni kweli I have one doubt: Kama Rais mtarajiwa padri slaa ameshindwa kusimamia agizo katika jimbo moja, ataweza kusimamia utekelazaji wa maagizo yake kwa nchi nzima?
 
Acha longolongo wee sema una shingi ngapi
Tatizo la nyie mambwiga wawili akili zenu hamjazipeleka jando........linalosemwa juu ya mdee ni yawezekna kweli.....kawaida ya wabunge kusahau majimbo yao japo yeye najua yuko busy na harakati za kichama zaidi......
 

hao ndo wafuasi wa CDM, great thinkers wasiopenda kuckia hoja yoyote iliyo agaist na wanachokiamini
 
Tatizo la nyie mambwiga wawili akili zenu hamjazipeleka jando........linalosemwa juu ya mdee ni yawezekna kweli.....kawaida ya wabunge kusahau majimbo yao japo yeye najua yuko busy na harakati za kichama zaidi......
Yo Yo, sikujua kama mimi ni Mbwiga, nadhani umenifanisha. Kina Mbwiga nilikuwa nakaa nao jirani siku za nyuma.
 
Last edited by a moderator:
Tangu achaguliwe kuwa mbunge Halima Mdee amefunguliwa threads nyingi sana. Baadhi tu ya threads hizo ni hizi.

Kwako Mbunge wangu Halima Mdee.....!!!!

What has Halima Mdee done for Kawe in the Last 3 years?

Halima Mdee (Mheshimiwa sana)

Mbunge wetu Halima Mdee, njoo utuokoe Kunduchi Machimboni

Report card ya wabunge wa Dar: Halima Mdee

Mheshimiwa Halima Mdee Kulikoni???

Mheshimiwa Halima Mdee Karibu Tegeta Namanga

Kipindi kigumu jimboni Kawe

Pamoja na hii inayoendelea.

Nadhani ndiye mbunge aliyefunguliwa threads nyingi zaidi ya kuuliziwa utendaji wake, na anayefuatia kwa wingi wa threads ni John Mnyika.

Kutokana na wingi wa threads hizi kuna uwezekano wa mambo kadhaa, lakini mie nataja mawili.

Kwanza. Kwamba Halima Mdee hatimizi wajibu wake.
Hapa kwanza itabidi tuainishe wajibu wa mbunge ni upi? Katika kupitia katiba nimeona haya hapa:
Kazi kuu za Bunge
· Kutunga sheria
· Kujadili mipango ya maendeleo na kupitisha makaridirio ya fedha za matumizi ya serikali kupitia Wizara husika.
· Kudhibiti mwenendo wa serikali, wakati wabunge wanapouliza na kuhoji mambo mbalimbali ya serikali. (maswali na majibu Bungeni).

Nini kazi za Wabunge?
Kazi za Wabunge ni pamoja na:-
· Kuwakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi.
· Kuhoji utendaji wa serikali
· Kuchangia uboreshaji wa miswada kabla haijawa sheria, na kuipitisha miswada iliyoboreshwa

Kitu gani kitarajiwe kutoka kwa mbunge?
Mbunge anatarajiwa:-
· Awe muelewa wa mahitaji na matatizo ya raia wake
· Ashirikiane kwa karibu na raia wake katika kutatua matatizo yao na kuleta maendeleo kwa kusikiliza wananchi juu ya kero zao, kusimamia utendaji wa halmashauri, kwa kutetea mgao wa bajeti ya serikali (si kwa kutumia pesa zake binafsi)
· Awawakilishe kikamilifu katika Bunge.

Je Halima Mdee anatekeleza haya? Kila mmoja anaweza fanya tathmini yake. Lakini mimi binafsi naona anatoa mchango mkubwa sana katika majukumu haya ya kibunge.
· Anachangia sana miswada mbalimbali ya kutunga sheria mpaka Mwanasheria mkuu na Mh. Lukuvi wanamwona kama anawasumbua.
· Anawatetea sana wananchi kwa maswali anayouliza bungeni, pamoja na michango anayotoa katika kuchangia mijadala ya bajeti. Hii hapa ni baadhi ya michango na maswali yake.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518750.html?highlight=#post4518750
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518392.html?highlight=#post4518392
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518191.html?highlight=#post4518191
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518111.html?highlight=#post4518111
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...years-post4518061.html?highlight=#post4518061
· Hata hivi sasa ametayarisha hoja binafsi itakayotetea wananchi wa Kawe na Watanzania kwa ujumla juu ya masuala ya ardhi.
· Anafanya pia vikao na wananchi wake. Hapa ni mfano mmojawapo.

Lakini tukirudi jimboni Kawe kuna mambo yanayoonekana ambayo yameshafanyika kwa juhudi zake:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.

2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.

3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.

4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.

5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.

6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.
7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.
8. Ameshiriki unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.
9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.

10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.

11. Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.

12. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.

Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.

Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri inayoongozwa na CCM (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha. Masuala ya ardhi ni mfano wa kukwamishwa na madiwani wake.

Pili, kwamba, huyu mtu anaikera system. Inawezekana anaikera system kwa michango yake bungeni ambayo huhoji ubadhirifu, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi wakubwa wa serikali. Kumbuka hata uvunjaji wa baraza la mawaziri wa mara ya mwisho, ulichochewa katika hatua za mwanzo na Halima Mdee. System ina namna yake ya kunyamazisha wenye kelele. Mifano ipo mingi tu Tanzania sihitaji kutaja. Inawezekana kuna watu hutumika humu na system kwa ajili ya kutekeleza hilo. Mfano: threads nyingi hapo juu zimeanzishwa na MAFILILI.

Kama hili ndilo, sisi wananchi wa kawaida tuwe makini kuangalia na kutokurupuka kumshambulia bila kutafakari vizuri. Nasema hivi kwa kuwa mtu anayeikera system kwa kutetea masuala yenye maslahi kwako mtu wa kawaida, huyu hayuko kinyume chako.

Mwisho najiuliza swali: hivi sisi watanzania tunatamani bunge letu liweje?
· Bunge lililojaa wabunge wa chama kimoja ambao wameapa kulinda maslahi ya Chama chao hata kama inabidi mwananchi wa kawaida apigwe teke?
· Bunge ambalo kazi yake ni kupigia makofi mawaziri, au bunge linalowawajibisha mawaziri?
· Bunge lililojaa wabunge matajiri ambao wana uwezo wa kuwahonga fedha zao binafsi, au wabunge wenye uchungu na wananchi na japo hawana uwezo wa kutumia fedha zao binafsi, lakini wanaibana serikali kuhakikisha kodi yako wewe mwananchi inakufanyia kazi wewe mwananchi?

Ndio maana wanasema akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Mie ni mchanga sana hapa jamvini lakini huu ndio mchango wangu katika maswala ya demokrasia ya vyama vingi.
 
Last edited by a moderator:
Naomba tulinganishe na utendaji wa wabunge wa Ilala, Segerea, Ukonga, Kinondoni , Temeke, Kigamboni na Ubungo.

Nani zaidi katika hawa? Na kwa lipi. Hapa tayari points za Mdee zimetajwa. Karibuni wadau.
 
Nimekusoma jfmwaipopo. kama kweli yuko hv nami nikiwa mwanachama mtiifu wa CDM nashauri abadirike mapema. Hawa magamba wanalitamani sana hili jimbo na tukifanya mzaha tumekwisha.Kamanda Mdee kama umenipata plz we dont want to lose you in 2015 wake up. Tembelea kata zote fungua mashina na matawi usitutie aibu.But BIG UP in Parliament.
 
sijaona la msingi hapa,acha wivu wa kike
 
Naomba tulinganishe na utendaji wa wabunge wa Ilala, Segerea, Ukonga, Kinondoni , Temeke, Kigamboni na Ubungo.

Nani zaidi katika hawa? Na kwa lipi. Hapa tayari points za Mdee zimetajwa. Karibuni wadau.

Huyu wa Kigamboni anajitahidi kuwa karibu na watu. Ana website yake Faustine's Baraza ambamo anapost mambo yote anayofanya.

John Mnyika pia anafanya hivyo pia kwenye website yake JOHN MNYIKA.

Halima Mdee ndio kama kwenye mchango wangu hapo juu.

Wengine kwa kweli sijaona sana wanachofanya, na kwa kuwa ni wa chama tawala, naona watu hawahangaiki kuhoji.

Ningeshauri watu mlio karibu na wabunge muwashauri wafungue website zao au blogs kwa ajili ya kujulisha watu mambo yanavyoenda.
 
Pamoja na yote uloandika nia yako huenda ni nzuri lakini namna ya uwasilishaji na mahala pa kuiwasilisha nadhani hapa kuna mshikeli kidogo,Pili ni kwamba huenda wewe unaelalamika hujui wajibu wako pia na napata tabu na mashaka tele huenda wewe nia Gamba au la kuna hali ya kutoelewana wewe binafsi na kamanda Mdee.

M
aana ukizungumzia kujenga chama mbunge ni sehemu tu ya wajenzi wa chama na yuko chini ya uongozi wa chama jimbo la Kawe na viongozi wa Kawe kama utaniambia wanamkumbatia hujui kuwa hao viongozi wa jimbo wamechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu?

Kama hawatendi kazi yao ipasavyo mna haki ya kufuata utaratibu unaokubalika na mkawaondoa halafu kisha mtaona anaegemea wapi huyo Mbunge-kamanda Mdee.Kingine hamjui ya kwamba wabunge wote wa Chadema wako chini ya viongozi wa Jimbo,hata kwenye vikao vya kamati tendaji yeye ni mjumbe meza kuu itabaki vile vile.

M
adiwani wote wako chini ya uongozi wa kata wa chama na wote wanawajibika ku-submit report zao za utekelezaji wa kazi kwenye ofisi za jimbo -wabunge na ofisi za kata -madiwani,kama wewe nimwanachama wa CDM kasome katiba-Soma kanuni za kusimamia shughuli,mwenendo na maadili ya Wabunge wa Chadema ukurasa wa 94 ibara ya 2 (f) na maeneo mengine,lakini pi yeye ni sehemu tu ya ujenzi wa chama je uongozi ukoje huko jimboni.

Cha msingi usilalamike tu na kulaumu endelea kutafuta namna bora ya ku-rescue jimbo kama hali iko hivyo
 
nafuuuu ya kawe kuna majimbo mengine huwezi amini kama ni tz hii mfano jimbo la maige....fanya utafiti hakuna umeme bara bara wala maji hospital mpaka waende kahama mjini au mgodini kahama mining
 

Yaani cdm siku hizi imekuwa km ndo chama tawala kwa jinsi kinavyoandamwa pamoja na wabunge wake
 
Yupo katesh huko anahangaika wakati jimboni mwake hali mbaya.Akiwa mjini yeye ni kushinda saluni
hakuna nchi iliyofanikiwa kwa majungu kwa hiyo mnataka awe mchafu hebu changia maada kaka acha vijembe sisi tunajua mbunge hawezi kuwa supervisor wa chama chama wilaya kikatiba ndio kinampa mbunge dira nini afanye na wapi aende tuoneshe ni mara ngapi halima anapewa ratiba anapuuzia ama anadharau ndio mseme anaua chama msilete mambo labda ya kudai mitaji kwa mbunge kama hakuna mnajipanga kuchafua
 
Hivi wewe unajuwa kuwa mdee ndiye aliye litafuta hilo jimbo kwani chadema wali kuwa na wagombea wengi hawakuwa na uwezo wa kuishinda ccm mdee ameweza.
 



Utoto nao unachangia,yaani ushabiki fulani ule wa kiSecondary School hawajui Halima alichaguliwa na watu wengi pia wa CCM kwa ajili ya mgombea aliyesimamishwa,wanadhani 2015 watarudia tena makosa!... wanadhani kupenda chama ni kutetea tu kama unavyotetea imani yako, watakuja kuliona hili baada ya 2015 tuombe tu uhai.
 

Lazima kutambua CDM ni wanadamu sio Malaika ni lazima kukosolewa kuondoa CCM sio kazi ya kupakana Mafuta kwa Mgongo wa Chupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…