Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,988
Hivi siku hizi umehamia madale?
Singida umehama?
Unamlaumu Halima Mdee kwani Chadema ina tinga tinga na polisi wa kusimamia bomoa bomoa, mmeiweka madarakani serikali dhaifu na hayo ndo malipo yenu............................... unamlaumu mkwezi wakati nazi imeliwa na mweziHata mimi nasikitika Halima Mdee ametuacha amekuwa kimya kama hakuna lilitoke jimboni kwake. mimi nina kiwanja nusu heka na nimejenga kanyumba kangu kadogo jamaa wamekabomoa? wanasema eti sisi ni wakimbizi wanadangany'a public sisi ni wakimbizi kutika Congo mara sijui Burundi ili public iwasupport na kuona imefanya vyema. lakini yote haya yakitokea Halima Mdee amekuwa kimya yani nikikumbuka siku ya uchaguzi mwaka juzi niliamka alfajiri kwenda kumpa Mdee kura yangu yani roho inaniuma. nashangaa kwanini hawa wabunge wanafuatilia mambo ya majimbo mengine alafu yao wanayanyamazia tu. Halima Mdee tunakuomba basi ongea hata neno tukusikia sisi tunajua wewe unaujua ukweli wote dada yetu
hebu tuongee ukweli wakuu,Mh Halima Mdee yuko wapi??naombeni jibu hapo,vilevile tunaomba record ya utendaji kazi jimboni mwake,tusiwe tunabisha kila hoja inayoletwa hapa bila kuwa na ushahidi!
Nilikuwa na imani kuwa wabunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HALIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.
wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la Kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.
Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.
My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakana na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.
source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.
Mvamizi unaomba msaada kwa mbunge. Wakati unavamia ulimshirikisha?source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.
Huyu alima Mdee amejisahau sana, Hata kuanzisha mchakato kwa wakazi wa Wazo na Madale kupata maji ameshindwa. Poleni wakazi wa jimbo la KAWE. Ilitakiwa agombee Kinondoni maana ninamuona anashinda baa za Kinondoni na wapambe wake.
Mwita! Mwita! Mwita! ukweli tutasema hata kama unaumiza. Punguza jazba.Umekosa hela ya bia wewe ndio maana unamuonea donge Mdee kwenda baa na wapambe wake. Kama vipi peleka maombi ya kuwa mpambe ili ufaidi pombe za bure.
Ingekuwa enzi zile wakati CHADEMA wanaiheshimu Jamiiforums viongozi wake wangekuwa washakuja kutolea swala hili ufafanuzi...
Kwanza it is an insult kumwita HARIMA ni HALIMA... Hii inaonyesha jinsi usivyomheshimu... Kwanini ni YEYE ANAYESHAMBULIWA Umeona
Wabunge wa TEMEKE na ILALA na KINONDONI? Hawajawahi kuulizwa CHOCHOTE HUMU ndani na wao ndio MATAJIRI WAKUU zaidi ya
HALIMA... Kafanya kazi kubwa JIMBONI zaidi ya HAO WA CCM yeye ndio wa kutishiwa na wewe?
Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.
Kama una jazba ya mambo yako ya kimaisha, haidha huna ajira, umebwaga na kicheche wako au umepatwa na jambo lolote linalofanana na hayo niliyoyaorodhesha basi usitumie uwanja huu wa great thinkes kuja kujifariji kwa kutoa mineno yako ambayo kimsingi haina mantiki katika hoja tajwa hapo juu. Sio lazima utoe maoni wala mawazo kama unajua hayajazi hata kikombe cha kahawa, ni bora ubaki nayo kichwani usubiri yapevuke ndio uyatoe maana ndio yanaweza kuleta manufaa zaidi.
Swala la mwananchi kutoa malalamiko yake kumuelekezea mbunge wake ni jambo ambalo linakubalika kabisa na hapa ndio maala sahihi kabisa kuyaleta ili kundi kubwa la watu waliolewa na mapenzi ya upinzani waamshwe kwa mifano sahihi kabisa, kwamba kuweka chama pinzani sio mwarubaini wa matatizo yanayotukabili wananchi, kama wengi wenu humu mnavyojiaminisha.
Ningependa kumaliza kwa kusema, viongozi wa chadema hawana utayali wa kuona mabadiliko kwa umma wa watanzania, bali wapo tayari kuutumia umma kwa ajili ya mabadiliko yao binafsi, kwenye hili la mabadiliko yao binafsi linajionesha waziwazi kwa kuona viongozi wa chadema wanavyoshinda na kula bata marekani mara kwa mara, wakitembelea magari ya kifahari na kupanga kwenye apartment za gharama kubwa, all in all wanawanyonya wanachama wao effectively na kuwatekenya kwa maneno matamu kama M4C na mengine mengi ya namna hiyo, wewe unaendelea kuenyeka huku wenzako wanapanda pipa tu. Badilika ubadili Taifa.
Bado hajaolewa, mchumba wake wa mwisho alikuwa Joshua Nasari sijui wamefikia wapi walitangaza hadharani kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki.
Mama Porojo, Maralia Sugu, tandale one, yaani signature nyinginyingi tu, kesho utasema unaishi tandale kwa tumbo ooh mbunge wangu Mnyika, wiki ijayo utakuja na ile ya kike uliyoweka kapicha ka kuvutia utajifanya unaishi Arumeru. In short hamtawabadili mtazamo watanzania kwa JF, face book na hii mitandao ya jamii. Mwambie nape asimamie serikali yake kutekeleza ilani yao ya 2010. Hilo ndilo jibu, kushindwa hilo ndio anguko lenyewe, kumsakama Halima Mdee haitawasaidia, wapiga kura wameelimika. M4C daima, "Changes are innevitable, if you do not change, change will change YOU". Nape anajua, Mukama anajua, ila wanawaficha tu. Ndio maana leo tuna vyama vingi, unadhani CCM ilipenda vyama vingi, ililazimishwa na wind of change. Mwambie ndugu yako Komba, kama alifikiri alikuwa anaimba tu kuburudisha hadhira, basi hiyo ndio maana yake "The wind of change is sweeping accross the african continent. In fact is in Tanzania for real.
Sidhani kama issue hapa ni kuigusa CDM. Tambua CDM haipo madarakani ila wananchi kwa mamilioni wameamua kuwaamini. 2015 utayashuhudia haya nisemayo. Mheshimiwa MDEE hahitaji porojo ili nyota ing'ae. Utendaji wake makini ndo unaowafanya wananchi wa kawe waendelee kumuamini,Najua nimewagusa chadema lakini huo ndio ukweli kama tunataka nyota ya Halima Mdee izidi kung'aa tumfikishie ujumbe huu.... haitakuwa na maana kama tutakuwa tunawalaumu wabunge wa CCM tu lakini hao mbadala tukaonekana ni kosa kuwaambia wanapojikwaa.