Huyo mzee sio mganga kwahiyo hawezi kukupa dawa, ni mfanyabiashara mwenye hardware, mashamba na mifugo. Wala sikumbuki jina lake na hanijui, na sidhani kama unaweza mpigia akakupa msaada au akakubali kuwa ana jambo hilo.Samahani mkuu,naweza kumpata huyo mzee?
Eneo la tukio kupata nyayo ni ngumu kwakuwa nimefika na kukuta wamevunja mlango na eneo lina nyasi fupi fupi.Nitafute pm,nitakupa dawa ambayo mtu akiiba si ataacha nyayo? Unaifunika kisha nakuja mimi naitengenezea dawa,huyo mwizi eidha atawehuka,kama sio kufa kabisa
Sawa mkuu..shukrani kwa wazo lako pia.Huyo mzee sio mganga kwahiyo hawezi kukupa dawa, ni mfanyabiashara mwenye hardware, mashamba na mifugo. Wala sikumbuki jina lake na hanijui, na sidhani kama unaweza mpigia akakupa msaada au akakubali kuwa ana jambo hilo.
Mimi nimetoa observation tu, mbinu kama hiyo utapata wapi hilo ni nje ya uwezo wangu.
Huwa siandiki kutafuta kiki mkuu. Nchi kubwa hii ina mambo ya kushangaza.Sasa ulikuwepo?
Simple tu mbona.
Tafuta kijana ambae hajulikani maeneo hayo, panga nae dili kwa makubaliano maalumu.
Kesho yake saa kumi na moja alfajiri, mnafika, anakaa hapo Garden peke yake mpaka mida kama ya saa 12:30 asubuhi.
Ikifika mida ile watu wanaanza kupita kwenda makazini, anajifanya kama hayuko sawa, anazunguka zunguka tu hapo bustanini, kama kuna ufagio anachukua anaanza kufagia fagia.
Watu wakianza kumtilia maanani na kuanza kuongezeka kuona kulikoni, yeye ndio kwaanza azidi kuongeza mbwembwe, ikibidi hata anaanza kuvua nguo.
Watu wakishajaa na kuwa wengi(hii ni kawaida ya mswahili na kumpiga hawawezi) unajitokeza pale mwenye mali, unamuangalia huyo mwizi wako halafu unapiga simu kwa mganga wako(jamaa mwingine uliempanga na wala hayupo mbali)
Ukishapiga simu unaweka loudspeaker, unamwambia mganga tayari mtu kanasa huku.
Basi chap mganga anakuja hata kwa bajaj na vitambaa vyake vyekundu na vyeusi, anafanya fanya dawa pale mpka mwizi wa mchongo anarudiwa na fahamu mnampakia kwenye bajaj haooooo unaenda kuwalipa hela yao mbele kwa mbele.
Tazama hii video mtangazaji wa itv alivyotuletea tangazo la dawa ya kukamata wezi.
View: https://youtu.be/m1fhoU_pbTg?si=Pc5BywrRA2-d1fFz
Matokeo ni guaranteed.😁😁shukrani,nitajaribu kufanya hili nalo nione matokeo yake
Hahaha..ningepata mtu kazi mwenye dawa hiyo ingekuwa vyema sanaKUNA WAHUNI PALE MWANZA MIAKA HIYO ILEMELA, KUNA MUUZA MKAA ALIIBIWA SIMU NI MUHA AKATANGAZA JAMANI ALIENIIBIA SIMU YANGU ARUDISHE MATEJA WAKACHUNA, ALASEMA HAYA WAKUU, AISEEE ILE SIMU ILIANZA KUITA TUMBONI KWA MDAU MMOJA TEJA, AKACHUKUA KISU ILI ATOBOE TUMBO AITOE, PARAPANDA ITALIA PARAPANDA TUMLAKI BWANA YESU MAWINGUNI,,, KWISHAAAA
Mkuu wapo SHIDA kuwapata, MANA WATU KAZI huwa SI waongeaji kabisa WAO huwa ni KIMYA MPAKA usontewe na wadauHahaha..ningepata mtu kazi mwenye dawa hiyo ingekuwa vyema sana
Tafadhali naomba unijulishe wapi- huko dar -nitapata ving'ora vya solar.Kwanza achana kabisa na kitu kinaitwa waganga.. Maana hao watakufilisi na hata kukugombanisha na watu
Watakuwekea masharti magumu ili wajivue lawama madawa yao feki yakibuma.. Siku hizi uganga umekuwa ni utapeli
Nashauri
1. Funga ving'ora vile vya solar wakisogea tu vinapiga kelele
2. Tega mitego ya kamba na ya mashimo
3. Tega upupu
4. Nk
Ajiri Wamaasai wawili hao hawana bei ,ukiandaa bajeti ya "Shuka 10 za kimaasai" aka KIlo moja aka Jiwe aka Box kwa mwezi kila mmoja anachukua.Habari wanajamvi...
Kwamuda wa mwaka na miezi kadhaa,nimekuwa nasumbuliwa na wezi kuiba kwenye sehemu ninapofanyia shughuli zangu za uzalishaji wa kipato cha kila leo.
Ninafanya shuguhuli za bustani ya mazao ya kilimo haswa michikichi na miti(matunda) na ya kawaida..Wezi wamekuwa wakiniibia mbegu kila wanavyojisikia kufanya hivo na nimejitahidi kufanya mbinu kadhaa ikiwemo kuripoti polisi bila mafanikio,kuweka waganga kadhaa napo sijafanikiwa maana dawa zao hazijafanya kazi,kuweka walinzi wa kampuni na wamasai napo hakujaleta mafanikio yoyote.
Tafadhali,kwa yoyote anayeweza kunisaidia mbinu mbadala nitashukuru sana. Imefikia hatua nashindwa kuendeleza shughuli hii kwani kila ninapopata mbegu hizo,wezi wanaziiba wanavyojiskia.
Natanguliza shukrani.
Sure mkuu Kuna wataalam wanatengeneza mpaka nyoka anakuwa mlinzi wa eneo Hilo akiingia mhalifu anaee! Ila sasa kuwapata wataalam wa namna hiyo ni mbinde kwa sasa wamejaa matapeli mpaka ufanikishe unaweza jikuta umeliwa pesa nyingi sanaShida yenu mnajifungia hapo Kinondoni mkijua mambo ya mjini tu, hii nchi kubwa.
Kuna mzee ana shamba lake jamaa alimuibia ndizi alivyokata mkungu asubuhi ile akaupeleka nyumbani kwake. Kufika kule akatua chini mkungu ukatoa sauti na kumuuliza mbona umepitiliza kwetu. Yule bwana ikabidi aubebe ampelekee mwenyewe na alipofika akujieleza sana alidai alikuta mkungu umeanguka amewasaidia kuwaletea na mmiliki halali akatoa shukrani. Bila drama, bila kuumizana wala kuleta taharuki.
Ukienda mikoani ukazunguka vijijini utajionea mwenyewe, upande wa kulia shamba moja mahindi yameibiwa shambani, upande wa kushoto hata lililoanguka kwa upepo halijajibiwa linaliwa na ndege. Kasoro tu wanafunzi wa shule ndio wagumu kudhibitiwa.
😂😂😂😂😂😂😂Hakuna mganga nchi hii wala dunia hii akusaidie wakati yeye menyewe hawezi kujisaidia ana maisha magumu mpaka kwenye meno
Hahaha ndio waganga hao tunaotaka kuwakimbilia watusaidie😂😂😂😂😂😂😂