Wezi wa simu TAZARA

Kuna siku usiku pale mataa ya kwenda Keko,Mbele kuna taxi ina abiria ndani,Harafu kuna jamaa yupo kando ya barabara kama anataka kuvuka hivi..aisee gafra akampora yule abiria ndani ya taxi na kuvuka mfeleji mbio na kupanda bodaboda iliyokuwa kando..nilisikitika sana..
 
kuna mmoja pale ubungo nilimtiwsha ndoo za maana hadi nikaonda nundu kichwani
 
Mimi nlifanya kama hayo ya mtego baada ya kuibiwa handbag ya sista,nkipotoka kumpokea airport.
Lkn mtego wangu ulikua mkali.
Ilikua MIDA ya SAA 4 usiku nkapita pale taratiiibu ka gari inataka kuzima.
Kwa mbali namwona kibaka anakuja na ameshika kitu kama panga.
Sikufanya makosa nkatoa ka mguu ka kuku.nkavunja kwanza magoti yake.kutahamaki naona wenzie wanakimbia kwa pembeni huko huko nkawatumia ASA sijui ka walifika Salama.
Yule alitapatapa pale barabarani nkawasha gari yangu na kutimua
 
Hongera mkuu tumeshajua unamiliki gari na pia unamiliki chamoto na chabaridi lengo lako limetimia mpaka akina miss chaga wanakusifia sasa ivi utawang'oa ngoja nami nikaandae kathread kangu huenda nikang'oa pia
Hii huwa ni dalili kubwa ya umaskini mkuu.
 
aisee kumuibia raia kipindi cha magu yataka moyo...maana hadi mia unayoipata waitumia kwa step
 

UNA ROHO NGUMU NDUGU, MI SIWEZI.
 
UNA ROHO NGUMU NDUGU, MI SIWEZI.
Bado hujaibiwa wewe,yani ilikua kila nikipita pale kwenye mataa roho ilikua inaniuma sana nikikumbuka simu yangu...nikajisemea lazima nifanye kitu...nnampango wa kufanya tena nikifikisha wezi watano ndo ntaacha,afu wezi mwenyewe hata nguvu hawana basi tu,cha muhimu ni kuwa makini wanakuwaga na viwembe,bisi bisi na sindano wanatumiaga kujidungia madawa!
 
Sasa ngoja niwape stori nlikotoa ujasiri huu ya hawa wajinga!!
Zamani kidogo nilikua nimepanda daladala,nataka home,Tabata naenda temeke,ilijua jpili,sasa tulivyofika pale Buguruni chama,konda akasimama akusanye kidogo abiria,tulikua wachache kwenye gar,mateja wakawa wanamsaidia kuita,mda wa kuondoka,konda hakuwapa wale mateja miambili yao,konda akamwambia aondoe gari,wake mateja bwana wakaenda nyuma ya daladala kwenye kioo cha nyuma wakamwaga kioo chote cha nyuma,wakatokomea kwa chini Kule nyuma wanakouza mbao,konda na hela alizokusanya akawaungia,basi pale watu wakawa wanaogopa kama kawaida wanaume wa dar,wakawa wanamuonea huruma konda kwamba hatarudi Salama na hela zote watamnyanganya,
Baada ya kama dk 7 hivi jamaa akaibuka nao wote wawili,wameshaloa makofi ya kutosha..
Kumbe yule konda ndo alikua kwenye gari afu ni msoja wa Rugalo,akawapandisha kwenye gari wale mateja akawakalisha kwenye seat ya karib na mlangoni akaanza kukusanya hela nyuma uko,akawapiga biti aliwaambia so mnajua nilipo watoa,ole wenu mkimbie,yani mpka tunafika tandika wale mateja walikua wanalia tu,kweli jamaa alirudi bila abiria kutoka tandika,Sikujua kilichoendelea Uko..
 
Sasa hiyo laki tatu utapewa wewe mkuu au maana umefanikisha zoezi kwa %9.9
 
Siku hizi wezi makini hawaibi simu hasa smartphone, wanaogopa kuwa tracked na hatimaye kukamatwa kama kuku.
 
Hongera kwa kucheza kama starring mkuu
ila panya wangeula mtego nadhani jumapili na wewe ungeenda kulia kanisani kama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…