Nokla
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 3,190
- 1,780
- Thread starter
- #21
1. kusugua sufuria kwa mchanga,
2. kutambiana kupigana kwa kuchora msitari wa kati na kutambiana wa kuuvuka,
3. kutotaka taa izimwe wakati nataka kulala kwa hofu,
4. kuchapwa bakora na walimu (ilikuwa kama kaoperation fulani) baada ya kugundulika kuwa una mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzako
5. kuibiana penseli/kalamu mashuleni kwani sikumbuki kama kuna wanafunzi walikuwa wakimaliza wino katika kalamu zao zaidi ya kupotea
6. Kuandikiana barua za kimapenzi mashuleni
7. kuwahofu form two wakati ninyi mkiwa form one
8.Mchezo wa baba na mama ingawa mimi sikuexperience huo mchezo
Hiyo namba saba tulikuwa tunaitwa NJUKA, au SALAMANDA au UNYOYA dah