Wewe ni nani? Swali gumu sana

Wewe ni nani? Swali gumu sana

King Octavian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Posts
403
Reaction score
353
Wewe ni nani?

Ni swali ambalo ukiulizwa unaweza kuliona rahisi sana na kulijibu haraka haraka kwa kutoa jibu linalotaja jina lako. Mimi ni James, ama nimi ni Janeth. Lakini ni ukweli ulio wazi kua wewe si jina lako. Wewe ni zaidi ya jina lako.

Ama unaweza kujibu kwa kutaja kazi yako, wewe ni nani? Ukajibu, mimi ni Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, mwingine atasema mimi ni Mbunge au mimi ni Waziri, ama mimi ni Mwalimu. Lakini ukweli ni kwamba wewe si kazi yako, wewe si cheo chako. Wewe ni zaidi ya kazi yako. Na kazi yako sio wewe.

MIMI NI NANI?
Naweza kujibu hivi.
Mimi ni mimi duniani kote, nipo mimi mwenye mawazo ya aina yangu, hakuna mwingine kama mimi, Nikifa. Akizaliwa mwingine akapewa jina langu, atakua mwingine mwenye jina langu. Mimi hana mbadala ila kuna mwingine atakayefanya niliyofanya. Mimi hawezi kua ndani ya mwingine popote, kabla yangu na baada yangu.

Je! Wewe ni Nani?
 
Jamani hili swali acheni masihara humu tunapeana uzoefu pamoja na kuwa tofauti na watu ambao sio critical thinkers humu ni jf jamani
Mimi hili swali lilinipa kazi jamani wanaobeza poa
 
Im Tycoon for Life, Field Marshal Al Hadji Professor Amalinze The cat my back never touch the ground, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Tanzania in Particular"
 
Mimi ni Roho iliyoko ndani ya nyumba ambayo ni mwili wangu, Mimi sio muonekano wangu ila muonekano wangu ndio mwili wangu ulionibeba Mimi, Mimi ni roho iliyotokea mbinguni kwakusudi maalum na kazi maalum niyotumwa hapa duniani, nikamilisha kazi hiyo nitarudi mbinguni nilikotokea na mwili wangu nitauacha kapa dunini maana nimeukuta hapahapa, muonekano wangu wa mwili unaweza ukakusaidia kujua Mimi nafana aje, Mimi ni zaidi ya Maelezo yangu
 
Unaweza kuniambia roho unawezaje kuihisi..?
 
Unaweza kuniambia roho unawezaje kuihisi..?
Roho inajitambua kuliko mwili, roho inayohisia kuliko mwili, Roho Ina macho yanaona vizuri kuliko ya mwili, Ina masikio,Ina nguvu kuliko mwili,
 
Back
Top Bottom