Hivi ni mimi tu au Tanzania watu wengi wanaona kumuuliza mtu “unaitwa nani?” siku ya kwanza ni kama umemtongoza?

Hivi ni mimi tu au Tanzania watu wengi wanaona kumuuliza mtu “unaitwa nani?” siku ya kwanza ni kama umemtongoza?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,595
Reaction score
59,929
Unaweza kukutana na mtu mkasalimiana, mkapiga story dakika 20, mkacheka kabisa… lakini hakuna anayesema jina lake. Mpaka mnaombana namba ndipo mchezo unaanza:
“Ni-save nani?”

Kuna ile culture ya kuzunguka sana kabla ya kuingia kwenye personal details. Watu wanaogopa kuonekana too direct au wanahisi kuuliza jina mapema ni kama unamvamia mtu. Ndiyo maana wengine hutumia tricks kama:
“Nikupigie missed call?”
“Una Instagram?”
“Ni-saveje?”
wakati swali la msingi lilipaswa kuwa rahisi tu:
“Mimi khaleed btw, wewe nani?”
Cha kushangaza ukienda baadhi ya nchi nyingine, mtu anakwambia jina lake ndani ya sekunde 5 tu:
“Hi, I’m Kevin.”Lakini huku unaweza kukutana na mtu mara tatu ndipo ujue kumbe anaitwa Kelvin ,,hio kutoambina majina ina faida gani?
 
Tanzania kwa 85-90% watu wake ni uncivilized hawajaendelea.

Ni kutokana na umasikini, unaopelekea kupata Elimu duni au hafifu, kukosa exposure n.k

Ila kwa jamii za western Jina ni kitu muhimu sana kumuuliza MTU , n.k

Ila hapa Tanzania ukimuuliza MTU unaitwa nani anahisi unaenda kumroga n.k watu wapo scared na Wana hofu isiyokuepo.
 
Mfano , nikikutana na wewe hata kama hatufahamiani

Ila nikakuambia John , tayari nakuwa nishatengeneza mazingira ya kusikilizwa.

Ila utamaduni wa Tanzania ni utamaduni wa kiswahili sana.

Kiasi cha MTU kutojua Name =Currency

Unakuta MTU anabadilisha namba Kila siku .

Kila mkoa anaoenda anabadilisha jina

Ukimpigia simu hapokei ,

Hataki kujulikana anaficha uhusika wake bila sababu za msingi.
 
Kusema ukweli kama vijana mmefikia hapo, ni halali wanawake walalamike. Ukutane na mtu 3× bila kumjua jina? Mimi kama mimi n salam after hapo nauliza jina na mengne yanafata sasa hata ya kuombana namba. Kuwa sharp ufanye jambo on time kuliko ati mambo, poa, unaenda wapi nikusindikize. Kwan nan kakwambia anaitaji bodyguard. Salimia mtu uliza yeye nikuite nani akianza na vijimambo vya jina langu unapeleka wapi achana na yeye huyo n mtoto ingia sehem nunua vocha mpgie yule halima umtoe out ya kushjukiza siku hiyo akileta visababu kuwa hana mda mzur achana nae hapo huna demu endelea na safar yako na kama huyo dem bado anageuka kukuangalia mfanyie ishara asimame muulize tena kwa mara ya pili jina hapo atakupa bila shombo mwambie kuwa akuachie namba utamtafuta cku nyngne coz kwa leo umekwazika nenda ukifka home futa hiyo namba na uache umalaya.
 
Hii ya kusimamishwa barabarani na kuuliza maswali kwangu mi sisimami wala siku jibu na uzee huu.

Miaka mingi iliyopita Arusha.

Hapo nilikuwa natoka triple three nakumbuka kulikuwa na saloni hapo..,.
Kipindi hicho nilitokea mpanda mining huko kwa usafiri wa kuunga unga mpaka Arusha na nilifika usiku......... Nokia jeneza ilizima njiani lakini destination ilikuwa triple three nikutane na muhusika na kipindi hicho kazi yangu kuu ilikuwa kusafirisha dhahabu

Basi nilikaa mule na jamaa kajifanya kunielewa,, nilikuwa nakunywa reds yangu kimachale sana. Saa kumi zile saloni kwa kipindi kile zilikuwa zinafunguliwa basi nilioga na kutengeza nywele pale, nikachukua nguo mpya. Maana sikuwa na ngua zaidi ya dhahabu iliyofungwa na box na kuchanganywa na vingine isiwe rahisi kwa wanaoijua dhahabu kujua hilo maana kwa wazoefu wanakwambia Ina harafu.
Sasa bwana eee.ile natoka hivi pale natembea zangu kuelekea uelekeo nilioelekezwa na boss wangu baada ya kumpata. Akatokea kaka mmoja hivi nikahisi ni mtu wa boss japo hakunipa signal yoyote!!!! Tukatembea kwa kuongozana kama dakika tatu tu........
Nilipewaa bonge la mtama na kuzimia pale pale... Kilichonisadia tu back up ya boss ilikuwa nyuma yangu kilichoendelea sikujua zaid li ya kusimuliwa na Kuona kwenye gazeti.

Baada ya hilo tukio Mimi kama sikujui na sikuwa na mpango wa kuonana na wewe sisimami njiani na siongei hovyo.
 
Kila jamii hua zina taratibu zake na mazoea yake,
Na kila jamii hudhamini taratibu au tamaduni zao,

Ukisema westeners wako civilized kisa wanaulizana majina,
Na sisi tutawashangaa,jinsi Mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake,ila wao huona ni jambo la kawaida tu,au mwanamke kuolewa na mwanamke mwenzake!

Kuulizana majina inategemea mmekutana wapi na kwa malengo yapi,
Dunia ya sasa hivi usalama umekua mdogo sana,kila mtu anajilinda kwa kadiri awezavyo.
 
Hii ya kusimamishwa barabarani na kuuliza maswali kwangu mi sisimami wala siku jibu na uzee huu.

Miaka mingi iliyopita Arusha.

Hapo nilikuwa natoka triple three nakumbuka kulikuwa na saloni hapo..,.
Kipindi hicho nilitokea mpanda mining huko kwa usafiri wa kuunga unga mpaka Arusha na nilifika usiku......... Nokia jeneza ilizima njiani lakini destination ilikuwa triple three nikutane na muhusika na kipindi hicho kazi yangu kuu ilikuwa kusafirisha dhahabu

Basi nilikaa mule na jamaa kajifanya kunielewa,, nilikuwa nakunywa reds yangu kimachale sana. Saa kumi zile saloni kwa kipindi kile zilikuwa zinafunguliwa basi nilioga na kutengeza nywele pale, nikachukua nguo mpya. Maana sikuwa na ngua zaidi ya dhahabu iliyofungwa na box na kuchanganywa na vingine isiwe rahisi kwa wanaoijua dhahabu kujua hilo maana kwa wazoefu wanakwambia Ina harafu.
Sasa bwana eee.ile natoka hivi pale natembea zangu kuelekea uelekeo nilioelekezwa na boss wangu baada ya kumpata. Akatokea kaka mmoja hivi nikahisi ni mtu wa boss japo hakunipa signal yoyote!!!! Tukatembea kwa kuongozana kama dakika tatu tu........
Nilipewaa bonge la mtama na kuzimia pale pale... Kilichonisadia tu back up ya boss ilikuwa nyuma yangu kilichoendelea sikujua zaid li ya kusimuliwa na Kuona kwenye gazeti.

Baada ya hilo tukio Mimi kama sikujui na sikuwa na mpango wa kuonana na wewe sisimami njiani na siongei hovyo.
Ulikuwa unasafirisha dhahabu za magendo au ambazo hazijalipiwa kodi?
Halafu huu mchongo itakuwa ulianzia ofisini kwenu ulipotoka au kwa uliyekuwa unampelekea.
 
Ulikuwa unasafirisha dhahabu za magendo au ambazo hazijalipiwa kodi?
Halafu huu mchongo itakuwa ukianzia ofisini kwenu ulipotoka au kwa uliyekuwa unampelekea.
Hakuna magendo yoyote dogo hapo,, labda uelewwa wako na Tanzania hii ni mdogo sana.
Kabla ya ujio wa mabenki kila Kona Tanzania hii,, m-pesa na masoko ya dhahabu unajua hali ilivyokuwa.
Unajua kwa baadhi ya sehemu mpka Hela zilikuwa zinasafirishwa na ilikuwa ni kazi kama kazi za ajira portal.
Hiyo ilikuwa kama njia mojawapo ya kukwepa majambazi....... Na kama unavyojua ukiomba escort ya police na tofali lako la dhahabu unajua kabisa ambacho kitakupata katikati ya safari yako
 
Back
Top Bottom