Wewe Kada Mwandamizi wa hapo CCM Ofisi Ndogo Lumumba uliyehoji kwanini simkubali Hussein Mwinyi haya ni Majibu yangu Kwako

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
Kwanza nimefurahi kujua kumbe nawe ni mwana JamiiForums Mwandamizi na mkubwa kabisa lakini pia kumbe ni Mtu ambaye unapenda sana Kufuatilia Mada (Threads) zangu hapa hasa za Kisiasa. Sitaki Kukutaja Jina ila nashukuru tu ya kwamba Mtu ambaye umemuuliza Asubuhi ya Leo kwamba kwani Mzukulu hakubali Dkt. Hussein Mwinyi awe Rais Zanzibar amenifikishia Salamu zako.

Haya sasa kwa Faida yako, wana CCM hapo Lumumba na kule Zanzibar hadi wale waliopo hapa JamiiForums hizi ndizo Sababu zangu kwanini simkubali ambazo naomba ziheshimiwe kwani ni zangu binafsi kutokana na ninavyomfahamu lakini pia kupitia kwa Vyanzo vyangu Muhimu na vya karibu nae ambao wanamjua na wamefanya nae Kazi.

1. Ni Mnafiki sana.
2. Ana Upole usio na tija Kiutendaji
3. Ni Muongo kitu ambacho ni Hatari kwa Ustawi wa Nchini (Kisiwa )
4. Mbinafsi kuliko Maelezo
5. Mdini mno na wala hajifichi
6. Si mtoa Ushirikiano mzuri katika mambo ya Kimsingi
7. Ni mtengeneza Makundi kila mahala ambapo huwa anakuwepo Kiutendaji

Mzukulu naendelea Kusisitiza CCM mkimpitisha Dkt. Hussein Mwinyi Jumapili huko Kikaoni Dodoma mtakuwa mmefanya Kosa Kubwa na mtakuja kunikumbuka na kuukumbuka huu Uzi wangu. Mkimpitisha Profesa Makame Mbarawa Mnyaa au Shamsi Vuai Nahodha mtakuwa mmefanya Maamuzi sahihi. Na atakayeshinda kati ya hawa Wawili basi Mmoja wao awe ndiyo Makamu wa Pili wa Rais huko Kisiwani Zanzibar.

Sina Chuki naye ila kwa upande wa Urais Dkt. Hussein Mwinyi hafai kabisa.
 
Mzukulu,

Umesaha kwamba ana dharau na hatengamani na watu. Kwa uongo ni kweli kwa sababu hta Cv aliyo weka haiko sawa. Kwa mfano anasema kazaliwa Tanzania, hataji wapi haswa, katiba ya Zanzibar, ina mtaka mtu anae omba nafasi ya urais. Zanzibar lazima uwe umezaliwa Zanzibar, yeye kazaliwa Tanzania. Twende na Mbarawa na Khamis Mussa.
 
Umesaha kwamba ana dharau na hatengamani na watu. Kwa uongo ni kweli kwa sababu hta Cv aliyo weka haiko sawa. Kwa mfano anasema kazaliwa Tanzania, hataji wapi haswa, katiba ya Zanzibar, ina mtaka mtu anae omba nafasi ya urais. Zanzibar lazima uwe umezaliwa Zanzibar, yeye kazaliwa Tanzania. Twende na Mbarawa na Khamis Mussa

Nashukuru Ndugu kwa Kuendelea nawe Kuonyesha Madhaifu (Mapungufu) yake na nazidi Kusisitiza na Kuwaonya CCM katika Kikao chao cha Uteuzi huko Mkoani (Mji Mkuu) Dodoma kuwa wakimpitisha tu Dkt. Hussein Mwinyi watakuja Kujuta na nina uhakika kuna Siku watakuja hapa hapa JamiiForums na Kuzisoma upya hizi Mada zangu Kumhusu Yeye na Kukataa asiteuliwe kuwa Isles next President.

Ni ama wampe Mbarawa au Nahodha na Mmoja wao hawa akiapishwa tu basi haraka sana amteue Mwenzake kuwa Makamu wa Pili wa Rais huko.
 
u. Mkimpitisha Profesa Makame Mbarawa Mnyaa au Shamsi Vuai Nahodha mtakuwa mmefanya Maamuzi sahihi.
Huyo Shamsi Vuai Nahodha unayempigia debe hayumo kwenye majina yaliyopendekezwa unapoteza nguvu bure kwa kitu hewa unajifanya mjuaji wakati hata list ya majina kichwani huna
Una ujuaji hewa

Tano bora waliopita mchujo wa Uchaguzi wa U Rais CCM Zanzibar ni kama ifuatavyo,
1. Dr. Hussein Mwinyi
2. Perera Silima
3. Prof Makame Mbarawa
4. Dr khalid
5. Khamis Mussa
 
CCM Makao Makuu na hata Mhusika Mkuu wa Mkutano wa CCM uliopitisha Majina hadi leo hii amesema kuwa hawezi kuyatoa hayo Majina hadharani kwani ni Siri na kwamba yatakwenda Kujulikana hiyo Siku ya Jumamosi na Jumapili huko Kikaoni Dodoma. Wewe Mwenzetu haya Majina umeyatoa wapi na kwa uhalali upi? Hopeless!
 
Huna hoja na hujui chochote kuhusu Mwinyi . Yaani unajisemea tu ni mnafiki ni mdini bila kueleza alifanya lipi lililokuaminisha kuwa ni mnafik au mdini? Hivi yupo Mtanzania au Muafrika ambaye sio mnafiki?
 
Kwanza nimefurahi kujua kumbe nawe ni mwana JamiiForums Mwandamizi na mkubwa kabisa lakini pia kumbe ni Mtu ambaye unapenda sana Kufuatilia Mada (Threads) zangu hapa hasa za Kisiasa. Sitaki Kukutaja Jina ila nashukuru tu ya kwamba Mtu ambaye umemuuliza Asubuhi ya Leo kwamba kwani Mzukulu hakubali Dkt. Hussein Mwinyi awe Rais Zanzibar amenifikishia Salamu zako.

Haya sasa kwa Faida yako, wana CCM hapo Lumumba na kule Zanzibar hadi wale waliopo hapa JamiiForums hizi ndizo Sababu zangu kwanini simkubali ambazo naomba ziheshimiwe kwani ni zangu binafsi kutokana na ninavyomfahamu lakini pia kupitia kwa Vyanzo vyangu Muhimu na vya karibu nae ambao wanamjua na wamefanya nae Kazi.

1. Ni Mnafiki sana.
2. Ana Upole usio na tija Kiutendaji
3. Ni Muongo kitu ambacho ni Hatari kwa Ustawi wa Nchini (Kisiwa )
4. Mbinafsi kuliko Maelezo
5. Mdini mno na wala hajifichi
6. Si mtoa Ushirikiano mzuri katika mambo ya Kimsingi
7. Ni mtengeneza Makundi kila mahala ambapo huwa anakuwepo Kiutendaji

Mzukulu naendelea Kusisitiza CCM mkimpitisha Dkt. Hussein Mwinyi Jumapili huko Kikaoni Dodoma mtakuwa mmefanya Kosa Kubwa na mtakuja kunikumbuka na kuukumbuka huu Uzi wangu. Mkimpitisha Profesa Makame Mbarawa Mnyaa au Shamsi Vuai Nahodha mtakuwa mmefanya Maamuzi sahihi. Na atakayeshinda kati ya hawa Wawili basi Mmoja wao awe ndiyo Makamu wa Pili wa Rais huko Kisiwani Zanzibar.

Sina Chuki naye ila kwa upande wa Urais Dkt. Hussein Mwinyi hafai kabisa.
Uaneni tu

Who cares!
 
Mzukulu,

Umesaha kwamba ana dharau na hatengamani na watu. Kwa uongo ni kweli kwa sababu hta Cv aliyo weka haiko sawa. Kwa mfano anasema kazaliwa Tanzania, hataji wapi haswa, katiba ya Zanzibar, ina mtaka mtu anae omba nafasi ya urais. Zanzibar lazima uwe umezaliwa Zanzibar, yeye kazaliwa Tanzania. Twende na Mbarawa na Khamis Mussa.
Hivi mbona niko peke yangu humu JF ninaeona Jecha the Great ndie anafaa urais sababu ni jeshi la mtu mmoja ni jasiri ana uthubutu, ni mzaliwa na mkaazi wa Zenjibari , mzee huyu ana hekima na busara ana umri mzuri kwa urais na ili kuikalia vizuri Zenji tunahitaji mzalendo wa kweli alieupigania muungano kwa vitendo na si mwingine ni Jecha aliejificha uvunguni na kumtangaza Shein rais kwanini tumtupe?

Jecha ni fundi wa fitna figisu na rafu kwenye siasa, mzee huyu bara tunammudu, mzee anajua wazenji wote ni maadui zake wamekataa kumdhamini huyu pekee afaa sana urais ili baadae wazenji wakiandamana kupinga chochote cha muungano Jecha hatosita kuagiza FFU wafanye kazi yao mara moja kupitia mabuti virungu na maji ya washawasha!! mimi nina uhakika 200% mtu pekee atauenzi muungano ni Jecha hawa wengine ni ndumilakuwili wote!! ukitaka kumjua mtu rangi yake halisi mpe cheo na pesa!! nani alijua rangi halisi ya sasa ya Magu akiwa waziri?
 
CCM wakimpitisha Hussein Mwinyi ACT watapita bila ya kupingwa. Kwa sababu hajazaliwa Zanzibar! Najuwa kuhalalisha uzaliwa wake ni rahisi kwa chama kilichopo madarakani, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli!
 
Huyo Shamsi Vuai Nahodha unayempigia debe hayumo kwenye majina yaliyopendekezwa unapoteza nguvu bure kwa kitu hewa unajifanya mjuaji wakati hata list ya majina kichwani huna
Una ujuaji hewa

Tano bora waliopita mchujo wa Uchaguzi wa U Rais CCM Zanzibar ni kama ifuatavyo,
1. Dr. Hussein Mwinyi
2. Perera Silima
3. Prof Makame Mbarawa
4. Dr khalid
5. Khamis Mussa

Haya majina hayajawekwa rasmi wewe umeyatoa wapi
 
hadharani kwani ni Siri na kwamba yatakwenda Kujulikana hiyo Siku ya Jumamosi na Jumapili huko Kikaoni Dodoma. Wewe Mwenzetu haya Majina umeyatoa wapi na kwa uhalali upi? Hopeless!
Mkuu unaijua Siri? Siri inakuwa ni ya Mtu binafsi na Moyo wake; Kukiwa na kamati fulani haiwezekani kuwa siri mzee.
 
Mzukulu bwana, ujuaji mwiiingi kumbe CHUKI na KIJICHO PEMBE ndio kinachokuongoza ktk mjadala wa kumponda Mh Mwinyi
 
Back
Top Bottom