Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,800
- 6,294
Wakuu nimetumiwa pesa toka Europe, natumia majina 3, nimeenda Bank ya Posta wananambia Jina langu linasomeka tofauti kwenye System Yao, tofauti Na kwenye kitambulisho, kwamba jina la mwisho ambalo Ni la ukoo lipo Kati, Na la Kati lipo mwisho, Cha ajabu Sender alinitumia form yake, inasoma majina yangu sawa Na kitambulisho changu, sasa najiuliza tatizo liko wapi? Last time nilitumiwa pesa nyingine Na the same Client, nlianzia Bank hiyo hiyo ya Posta, wakakataa kunipa pesa, nikaenda Azania Bank wakanipa pesa, ila Teller akanambia next time mwambie Sender aandike majina yako Kama yalivyo, Leo nimeenda Azania wanasema Ni wiki sasa Network iko down, Posta Bank ndo hawataki hata kunisikiliza, Nimecheki Na Sender akawasiliana Na Western Union huko kwao wanasema Majina yangu yapo sawa Kama Yanavyoonekana kwenye form walionitumia, (Wanasema tatizo litakua Tanzania), System za wabongo zinasema majina yangu yamechanganywa, la Kati liko mwisho Na mwisho Kati, tatizo liko wapi? Kuna yoyote mwenye uzoefu Na kilichonikuta?
NB:Nasikitika Sana kwa kukosekana huduma ya PayPal hapa, Mimi nauza kazi zangu ulaya, sometimes client hawapendi kutumia njia ya Bank, wanataka PayPal, nawaambia nchi hairuhusu PayPal, nawaomba watume pesa kwa Western Union, Na kwenyewe Inakua usumbufu, tena nianze kumwambia Client aende kwenye office alotuma pesa kuhakiki, wenzetu hawapendi usumbufu, next time hawezi kufanya biashara Na Mimi tena!.....