Sasa hivi naanza kuelewa kwanini JK anaogopa kutengua mikataba ya madini na ubinafsishaji uliotufikisha hapa tulipo. Naamini sio kwa sababu haimuumizi, isipokuwa njaa za watu wetu, uroho wa madaraka na umaskini wa akili ni silaha tosha ambayo JK anaweza kusulubiwa peke yake kwa maamuzi anayoweza kufanya kwa niaba ya taifa.
Amini nawaambia, matatizo yetu ndani ya Bongo yakiwekwa kwenye luninga za BBC na kuelezea uovu wa CCM dhidi ya wananchi maskini, bila shaka Zimbabwe bado itakuwa mbingu kama tunafananisha na mashaka ya watanzania ambayo si wengi tunayafahamu ingawa tunajiita watanzania.
Amini nawaambia, Mugabe ni sehemu ndogo sana ya tatizo la Zimbabwe, kubwa ni vikwazo vya uchumi ambavyo hata Saddam pamoja na mafuta yake hakuweza kuvihimili; na hakuna nchi ambayo hata kama wangekuwa na demokrasia kiasi gani na sera nzuri kupindukia, kwenye vikwazo uchumi, nchi hiyo itafukarishwa na njaa itakayotengezwa na vikwazo hivyo, inaweza kabisa kutengeneza wavunja sheria ambao wakiguswa na vyombo vya usalama wanageuka wapinzani.
Picha hii tunayoiona Zimbabwe ni ishara tosha ya nini kinaweza kumkumba JK pindi atachukua hatua madhubuti kuhakikisha watanzania wanapata chao cha halali. Swali je tutakubaliana kusimama naye na kumuunga mkono, au tutaitikia kibwagizo cha wenye maslahi yao kuwa JK anakiuka haki za binadamu, mpinga demokrasia na chanzo cha mateso ya watanzania, mateso ambayo hao hao watakaompinga kesho hawayaoni kwa sasa kwa sababu ya kufaidika na mikataba ya kishenzi?
Swali la kutafakari, leo hii bajeti yetu inategemea wafadhili kwa asilimia 42, hatuna vikwazo vya biashara, embu tujiangalie tulipo. Halafu jiulize, kama Tanzania ingekuwa Zimbabwe, kwa miaka hii minane hakuna vijisenti vya mfadhili vinavyodondoka kwenye bajeti huku uchumi ukichagizwa na vikwazo vya kiuchumi, je ni sera zipi za uchumi na busara gani ya kisiasa zaidi ya kuwa mtumwa zingeweza kuisadia nchi kupambana na madhara ambayo wenzetu wamekutwa nayo?
... inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.
Kama hawajui Psychology SHAURI YAO!
Njaa ni TATIZO LA KISAIKOLOJIA!
...heri wewe uliyeliona hilo!...
😀
maana hata kama 'wazungu' wamembana Mugabe asiuze mazao ulaya, basi hata soko la ndani, au southern Africa pia hakuna wa kununua?
Fundi Mchundo,Masanja,Koba,Kuhani Mkuu,Kitila Mkumbo,Mkandara,....
..naomba kuwauliza maswali yafuatayo wachangiaji wa mjadala huu.
..ni sera zipi za Mugabe ambazo zinasababisha inflation iwe kubwa kiasi kile?
..najua kwamba wana-print pesa kama wajinga, lakini why do they have to do it in the first place?
..vilevile ninavyoelewa mimi, in Mugabe's watch uchumi wa Zimbabwe ulipata kukua hata by double digits. what was he doing right? what is he doing wrong now?
..zaidi kuna yeyote anayefahamu sera za Morgan Tsivangarai ambazo zitaondoa hii inflation?
..pia Tsivangarai ana sera au mipango gani ya kupambana na njaa ya muda mrefu Zimbabwe?
..je Tsivangarai atarudisha ardhi kwa wazungu? kama atarudisha si kutakuwa na vita? na asiporudisha njaa itakwisha kweli? inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.
Mkuu hapa tuko pamoja. Ndo hapo tunapoona kwamba the current system we have is not working, lakini wale wanaojaribu kuibadilisha ndo tunawacrucify kama vibaraka.. Jamani ni nchi gani mpinzani atashindana na incumbent asionekane msaliti na kibaraka wa wazungu? Thats exactly what our leaders want us to believe. Sasa tusilaumu tuu, lets give alternative basi! Nani atatukomboa? au kila mtu mwenye mapenzi mema na Africa lazima aje kwenye platform ya ant western? ndo atakubalika?
Hapana, Nimekataa na nimechoka kudanganywa!
Joka Kuu said:..pia Tsivangarai ana sera au mipango gani ya kupambana na njaa ya muda mrefu Zimbabwe?
..je Tsivangarai atarudisha ardhi kwa wazungu? kama atarudisha si kutakuwa na vita? na asiporudisha njaa itakwisha kweli? inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.
Masanja said:Joka kuu acha siasa mufilisi kwamba Morgan atarudisha mashamba kwa wazungu... has he said so?
Masanja said:Yes, whites are equally culpable for the happenings in Zim, but Mugabe alifikiria kwamba unaweza kuplay na economics kwa kutumia siasa na ukafanikiwa, and that was damn wrong! Uchumi wa kiafrika bado ni tegemezi.
Tatizo kubwa la Uchumi Zimbabwe ni Uongozi mbaya wa Mugabe hasa baaya ya kuchukua ardhi...Mwalimu aliwahi kumkanya Mugabe asifanye hivyo hata siku moja akimkumbushia hali halisi ya Uchumi wa Tanzania ktk miaka ya mwisho ya Utawala wake.
...Mugabe hakusikia baada ya Muingereza kuvunja ahadi ya ugawanaji wa ardhi na hii ilitokana na shinikizo wa Wapigania Uhuru ambao walikuwa hawana ardhi sio tu ya kilimo bali hata ile isokuwa na mashamba
....wakidhani kwamba wanaweza kujiendesha wenyewe wakajipanga bungeni na kupitisha sheria ya ardhi..Toka hapo, uchumi wa nchi hiyo ulianza kuporomoka vibaya sana, na ukweli niu kwamba kila kitu kinachozalishwa nchi hiyo kilikuwa mali ya mzungu ambaye kanyang'anywa ardhi (makazi) na kuitwa mgeni hali ahadi ya awali ni kwamba wote ni Wazimbabwe.
...Baada ya hapo Zimbabwe wamewekewa vikwazo hasa na nchi za Marekani, Canada na UK ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa mali zao na fedha yao ktk market hakuwa na nguvu tena kwa sababu hakuna mtu anayetaka kununua kitu Zimbabwe..
...Haya ni matokeo ambayo aidha Mugabe aliya over look ama hakujiandaa nayo na ndio maana nashindwa kuelewa Mugabe ambaye alikuwa akisifiwa na wazungu miaka ya 80 na 90 leo kawa shetani kwa mzungu hali sera zake kiuchumi hazijabadilika, labda hilo la ardhi tu. Nyama zao za ng'ombe zilipigwa marufuku karibu dunia nzima, na binafsi siamini kuwa Wazimbabwe hawana ujuzi wa kilimo wakati ndio wao waliokuwa wakilima mashamba hayo miaka yote.
...na kashindwa hata kufikiria wananchi wake, miaka yote kashindwa kusoma alama akitumia ile aya ya kutogeuka jiwe.. Binafsi kama unakumbuka niliwahi kusema WHY hajaribu kufikia deal na wazungu hawezi kushindana nao.. ardhi igawanywe kati yao badala ya kuchukua yote. Kata kipande kisichotumiwa na wanzungu wape hao waswahili lakini pia ni muhimu kukumbuka kwamba mswahili kuwa jirani na mzungu ni issue nyingine!..
...Dunia hii huwezi kumtegemea mzungu kisha ukafikiria kuna siku unaweza kuwa fit kumgeuka atakumaliza kama Saadam Hussein. Na wanammaliza kweli hana choice Mugabe isipokuwa kung'atuka lakini Morgan sio solution ktk kutazama mustakabali wa nchi hiyo!
..labda Mugabe amchukue mtu mwingie nafasi yake, yet kama ardhi hairudi ina maana uchumi wa Zimbabwe utaendelea kushuka.. It's either you give in or else!...