Werema amkubali Dr. Slaa - Gharama za uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Werema amkubali Dr. Slaa - Gharama za uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kamakabuzi, Apr 20, 2010.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimemsikia jana Bungeni Jaji Werema akikubali kwa lugha ya kisiasa kuwa sheria ya gharama za uchaguzi inabidi ifanyiwe marekebisho. Na katika vifungu alivyotaja ni kifungu cha 7 ambacho Slaa alikuwa amekilalamikia. Japo ametumia usiasa zaidi, amekiri kuwa kwenye kamati alibanwa na kulazimika kuleta mabadiliko haya.

  Kwa upande wa msemaji wa kambi ya upinzani -yeye hakuuma maneno; ni kweli vifungu viliingizwa kinyemela na sasa vijadiliwe upya.

  Kwa wanaJF: Kuna mtu mmoja alituwekea hansard ya siku husika hasa mjadala wa sheria hii, lakini baadhi ya wanaJF wakaisoma kisiasa na kuona kuwa kuweka kifungu cha 7(3) ailikuwa sawa.

  Silazimishi wote tuwe na maoni yanayofanana, ila kwa jambo lililokuwa wazi (hansard) tulipaswa kuwaeleza wasomoaji wetu ukweli. JF inapaswa kuwa sehemu ya wasomaji kupata hoja za ukweli.
  Kwa jaji werema: Enzi za kuburuza bunge zilikwisha siku nyingi - kwenye bunge kuna serikali mbili - ile iliyo madarakani na ile inayosubiri kuingia madarakani.

  Usidhani wale wanaosubiri kuingia madarakani wataacha kuwa makini; lazima wachimbue sana ili waonyeshe udhaifu wa walio madarakani ili wao wachaguliwe awamu inayofuata - be careful; otherwise u-jaji wao utakuwa questionable!
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tungelikuwa na akina Dr. Slaa kama hamsini hivi Bungeni, mambo yangelikuwa mazuri sana. Lakini, kila siku ni Slaa tu ndiye anayefanya homework yake kwa utimilifu!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ukiwa na serikali ya hovyo hovyo obvipus utakuwa na watendaji wa hovyo hovyo
   
 4. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  UKIWA NA JAMII HOVYO UTAPATA SERIKALI HOVYO! Serikali inatokana na jamii na JAMII MAKINI HATAKUBALI SERIKALI HOVYO, ITAIONDOA NA KUWEKA MAKINI.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Apr 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Werema akielewa jambo huwa sio mbishi kulifanyia kazi... Alikuwa hajaelewa tu lakini jamaa he is good yuko flexible kwa kweli.
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hamsini wote wanini? >>>>>...Slaa + Zitoo + vichwa vitatu kama hivyo= Bungeni Ze patamus!....acha bwana,
   
 7. Mwathirika

  Mwathirika JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Sisi ni akina Slaa pia. Tuwasaidie kwa kila hali. Endeleza!! Yes we can!!
   
 8. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  hatuwezi kuwapata wote hao itakuwa ngumu kwani hawa jamaa waupinzani wamelenga kwenda ikulu tu.Hawataki kukimbizana na serikali ya chini kama mwenyekiti wa serikali ya mtaa na udiwani.Huko ndo wanakoanzia kupatikana kina Slaa.
  Mfano mzuri eneo la kata ya mbweni DARjimbo la Kinondoni hakukuwepo na chama kingine zaidi ya CCM katika uchaguzi. Hivyo hata kura haikupiwa maana waliendelea wale wale waliopitishwa na CCM.
  Sijui upinzani wa TZ unaanzia wapi?
   
 9. R

  Rayase Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Binafsi naishukuru serikali chini ya Mhe rais kukubali bila ubishi maoni na kuyafanyia kazi! Serikali sikivu huwa naikubali sana
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  kumbe sisi wanajamii ndio tunasababisha serikali yetu kuwa ovyo ovyo kivip Lebabu11 bado sijaipata point yako vizuri
   
 11. Bright

  Bright Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama huyo jaji Werema yuko 'flexible' hatufai kwani kwenye shaeria hakuna 'flexibility'. 'Flexibility' yake ndio imepelekea kuongeza hivyo vifungu.
   
 12. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu Dr. Slaa hamsini wote hao wa nini! Wangekuwepo angalu watano tu kama yeye, hakika tungeshuhudia mabadiliko makubwa sana.
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mkuu Boramaisha, bado siamini kwamba hawa jamaa ni mambumbumbu kiasi hicho yaani hata kushindwa kugundua vipengere vilivyo chomekewa ki fisadi ndani ya muswaada kabla ya Rais Kusaini kweli? hapana mi naona kinachofanyika ni uzembe / ufisadi wa makusudi wakijua fika kwamba wasaidizi wa Rais na Rais mwenyewe hapendi kupitia pitia vipengele katika makaratasi kabla ya kutia wino.

  Rais kama hasomi na wasaidizi wake hawasomi basi wapuuzi wengine wanachomeka mambo ya ajabu wakijua kuna udhaifu mule - yale yale ya kukabidhi magari yanajirudia tena.

  Ni kweli bila kuwa na DR. Slaa basi mambo yangekuwa zaidi ya hiyo HOVYO HOVYO tunayoisema. Cha ajabu hakuna mtu yeyote atachukuliwa hatua juu ya uhuni huu - hii nchi mimi sielewi tunakwenda wapi - na kama CCM wakiongoza nchi hii in next 20 years naapa Tanzania itakuwa jalala la takataka.

  Mimi ningekuwa Rais kwanza ningeanza na wale waliochomeka upuuzi huo - pili katibu mkuu wangu na ofisi yake wote maliganyaja - lakini aaaaa nipo YUESII sina tatizo mtu wa watu.

  Hongera sana Dr Slaa sisi watanzania wanaelewa sana mchango wako - nafikiri itafika hatua hata utafaa kuitwa baba mdogo wa taifa (2nd father of the Nation) - maana we ndiye umebakia mwenye uchungu na nchi yako wengine hawayaoni haya yote. Thanks once again - Mtetezi wa wanyonge - BIG UP.
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hivi unaaamini kwamba kuongeza hivyo vifungu baada ya muswada kuwa umpetishwa bungeni na kabla Rais hajasaini ulikuwa ni uamuzi wa Werema peke yake? Tutakuwa tunajidanganya hapa. Serikali kupitia kwa Werema waliamua kufanya hivyo na Rais alijua hilo kabla ya kusaini. Cha kushukuru ni kwamba mpiganaji Dr. Slaa aliwashtukia au labda alitonywa na mtu juu ya mchezo mchafu uliochezeka kwenye huo muswada.

  I stand to be corrected.

  Tiba
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuchomekwa kwa hivyo vifungu si kwamba rais alikuwa hafahamu lilikuwa ni deal lakini kwa vile siku zote Mkubwa huwa hakosei ikatafanywa coverup kuwa yeye hakuusoma ili kumlindia heshima yake lakini vilevile wakasahau hata kule kusaini bila kuusoma ni kashifa nyingine.
   
 16. B

  Bobby JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  GS ninahofu na huo uelewa wake au may be alikuwa mwelewa b4 kuwa mwanasiasa. Jaji Werema umetusikitisha sana sisi tuliokuwa tunakufahamu before. Ulimshambulia kabisa Dr. Slaa infact ulitoa mpaka press release kwenye magazeti kwa kutumia kodi zetu kupinga kitu kilichokuwa wazi hata kwetu sisi ambao hatukuwapo Bungeni. Sifahamu zilitumika pesa kiasi gani kutoa hizo adverts kwenye magazeti lakini ninafahamu watanzania wengi tu ambao mlo mmoja kwa siku kwao ni muujiza. Sasa ili tukusamehe kwenye hili ulilofanya nashauri pesa iliyotumika kutoa press release ukatwe toka kwenye mshahara wako kwani kuna watanzania kama wewe ambao wanakufa kwa njaa.
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  100% correct...
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Na bado
   
 19. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Sehemu kubwa ya viongozi wakuu serikalini wamekaa kiwiziwizi tu. Ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi kukubali huo uchafu wa kuongezi vifungu kinyume na utaratibu/sheria. Nafikiri alifanya hivyo baada ya kuona vina maslahi kwake (CCM). Sidhani kama angekubali kusaini kama kipengele hicho kinge wasaidia wapinzani.

  Kwa ufupi ni kwamba yeye mwenyewe ni fisadi ndo maana anashindwa kuwabana mafisadi.
   
 20. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Laiti Watanzania wangeelewa hili mbona raha Oktoba
   
Loading...