Wenzetu wanaenda mbele, sisi tunarudi nyuma

Wananchi wako buzzy kupinga ushoga na usagaji, hebu usiwasumbue plz.
 
Kuna karne itafika kwa wajinga kuwa viongozi na werevu kuwa wafuasi nadhani Karne yenyewe ndo hii "Shaaban Robert

"Tumeruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa" mchungaji Peter Ms

"Shida kubwa ya viongozi wa Afrika ni kuwaza chaguzi kuliko kutatua matatizo ya wananchi" Tony

Namna utakavyo panda ndivyo utakavyo vuna Watanzania Sasa tuna vuna tulicho panda hakuna wa kumpa lawama zaidi yetu sisi wenyewe na hato tokea mtu kutusaidia kututoa hapa tulipo zaidi yetu sisi wenyewe "tujisahihishe"

Tulikuwa na viwanda vingi Sana ndani ya nchi hii niliwahi pita kiwanda cha urafiki nilibaki kutikisa kichwa tu

Leo hii sehemu ya kiwanda ni kanisa la mtu
alafu vijana waume kwa wake wanajikusanya kuombewa kupata ajira uku ndo tuliko fikia

Mpaka Sasa huwa sijapata majibu ni viongozi gani walihujumu ranch za taifa za mifugo ?

"CCM Kuna mafisi"JK
 
Nimekuwa nikikwepa kwa maksudi kabisa kusoma yaliyoandikwa chini ya kichwa cha mada hii toka niione imebandikwa hapa, lakini uvumilivu umeniishia, imenilazimu tu niangalie kilichoandikwa humu.

Na kama ilivyo kawaida ya kumbi hizi za JF, mada nzito nzito kama hizi huoni uchangiaji unaoendana na uzito wa mada yenyewe.
Toka asubuhi hadi wakati huu, ni kurasa 2 tu, za mada ya namna hii!

Ingekuwa ni kutunukiwa PhD kwa wagawa asali, bila shaka tungekuwa mbali sana na hii mada.
Sasa kama hiki si kielelezo cha waTanzania wa leo sijui tukiite kitu gani

WaTanzania tunapoteza umakini wetu, na yote hii inatokana na uongozi unaotuongoza, huu ndio uamini wangu.

Itahitaji kupata viongozi ambao wanaamini katika uwezo wa waTanzania kufanya mambo muhimu, mazito, na kusimamia juhudi hizo kikamilifu kulibadilisha taifa hili kutoka kwenye hali hii ya aibu inayotukabili sasa hivi.
 
Hata upinzani tulikuwa na akina Christopher Kasanga Tumbo aliyeambiwa na Nyerere " niko tayari kukuteua kwa Cheo chochote sema unapenda kuwa nani" Kasanga Tumbo akamjibu " Nataka hicho Cheo chako cha Rais wa JMT"

Lakini Wapinzani wa Leo ndio hao akina Mbowe,, Zitto, Dr Slaa na Halima Mdee na wenzake wanaorambishwa asali Bila aibu!
Acha kupotosha kama huijui historia, maneno hayo haya kutamkwa na marehemu Christopher Kasanga Tumbo bali mtu mwingine.
Kajifunze upya au acha kudandia

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Wakati ule nauli ilikuwa sh 5, yaani sawa na dola 1. Kwa hiyo nauli ya mabasi ya mzunguko mjini ilikuwa dola moja. Neno hilo dola ndiyo lilizaa jina daladala wakimaanisha kila unakoenda unalipa dola moja. Watu walikuwa wakilipa na kuona ni hela ya kawaida. Leo waambie abiria kuwa nauli ya daladala ni sh 2,350; watatweza kutoa, au itakuwa ni malalamiko kila mahali?
Hela yetu ilikuwa na heshima na thamani bro sio leo
Yote haya ni wizi tu halafu anakuja mjinga anasema wakoloni waesababisha umasikini wetu

Wengine wanasema vita ya Amin
Ila hawaoni wanavyoiba utafikiri punda anapoona majani maana anakula mpaka mizizi, tofauti na mbuzi anaeacha na ya kesho
 
Mtu mnafiki, mwongo, na ambaye hana uhuru wa mawazo huwa hagundui kitu chochote, akijitahidi ataishia kuiga na kukariri.

Moja ya sababu, wanasaikolojia wanasema kwa nchi ya China kutokufanya ugunduzi, na kuwa nchi ya copy and paste, ni wananchi wake kuelelewa katika mazingira yasiyoheshimu uhuru wa mtu.

Tanzania kuna wakati ilikuwa inaunganisha malori aina ya Scania, sasa hivi tumeishia kuunganisha pikipiki za China.

Kuna wakati tulikuwa tunaunganisha matrekta bora kabisa ya valmet, sahizi hatuunganishi hata power tiller.

Tulikuwa tunatengeneza baiskeli aina ya swala, baiskeli nzuri kabisa,sahizi hatutengenezi hata sindano ya cherehani.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza matairi bora kabisa yakijulikana General Tyre, sahizi tumebakia kuwa watumiaji wa matairi ya hovyo kabisa kwa ubora kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza mashuka bora kabisa toka kiwanda cha Mutex, siku hizi tumebakia kuwa watumiaji wa mashuka ya hovyo kabisa, yapo kama vikaratasi, kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza viatu bora vya ngozi toka kiwanda cha Moro Shoes, siku hizi tumebakia kuwa wanunuzi wa viatu duni kabisa toka China, ukijikwaa tu kimechanika au kuraruka.

Tulikuwa tunatengeneza ndoo za ubora wa hali ya juu, Amboni Plastics, siku hizi tumebakia na ndoo takataka ukibebea tu maji, mshikio unachomoka au ndoo yenyewe kupasuka.

Wakati ule ilikuwa kipimo cha umaskini kwa mama ni kuvaa kanga iliyotengenezwa China au India, huku mwenye uwezo akivaa kanga ya Urafiki, leo hata ukiwa na hela, kanga nzuri huipati popote, kila mahali ni takataka za kutoka China.

Zamani, katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi angalao ilikuwa inaonekana kuwa na demokrasia, leo ndiyo nchi ya mfano kwa utawala usiozingatia sheria, usioheshimu mgawanyo wa mihimili. Tena imekuwa ni nchi ya kidikteta ambayo hata kura ya mwananchi haina maana yoyote katika kuwapata viongozi.

Kenya tuliokuwa tunawaona hawajastaarabika kwa kuendekeza siasa za ukabila, sasa ni nchi ya mfano Afrika Mashariki kwa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia, haki za watu, uhuru wa maoni, na katika kuheshimu mfumo wa siasa za vyama vingi.

Wakati wenzetu, kuendelea inamaanisha kuboresha, sisi kuendelea inamaanisha kuendeleza uharibifu. Tumekuwa Taifa bandia, taifa linaloongozwa kwa hadaa na ulaghai. Majukwaani wanatamka vingine, matendo yanakuwa kinyume. Wateule wamebakia kuumsifia anayewateua kwa unafiki. Kila mahali watasimama na kumsifia aliyewateua ili awaone na kuwasikia, wakiachia mic, wanamsema vibaya. Unafiki mtupu.

Watawala, hata pale ambapo mambo yanaenda vibaya, watakuambia kuwa sasa ndiyo tunapaa, wakati hata vyandarua vya mbu tunapewa msaada. Zamani, Serikali ilikuwa na watu wanapita mitaani kufanya fumigation kuua mbu na mende, leo tunashindwa hata kununua chanjo kwaajili ya watoto wetu wanaozaliwa.

Ni nani atalirudisha Taifa kutoka kwenye unafiki kulipeleka katika uhalisia? Nani ataweza kusimama na kusema kuwa Taifa letu ni duni katika nyanja nyingi, tusimame, turudi na kuanza upya?

Siku zote hatua ya kwanza kuleta mabadiliko chanya ni kuutambua na kuukubali udhaifu wako.
Unapoandika kwamba "....Zamani, katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi angalao ilikuwa inaonekana kuwa na demokrasia..." wengi wanaamini demokrasia imeanza mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye siasa za ushindani (wa kwenye makaratasi). So usipoelezea zaidi tutashindwa kuoanisha ujumbe wako mkuu wa namna nchi ilivyorudi nyuma sana kiuwezo wake wa kujitegemea na jinsi ambavyo kurudi huko nyuma kunatokana na kuzorota kwa demokrasia na haki za binadamu. Nifahamuvyo mimi uwezo wetu wa kujitegemea ulianza kurudi nyuma mara tu baada ya kutii masharti ya SAPs ya kibeberu. Wale IMF na World Bank waliotulazimisha tuingie kwenye mfumo wa kibeberu wa free market ndio walioua kila kahatua tulikoanza kukapiga kuelekea nchi huru. Magufuli ndiye alietaka turudi kuwa nchi huru lakini napo wamemmaliza.
 
Kuutambua na kuukubali udhaifu kwanza kutanguliwe na kuifuta mentality ya kuwaona wapinzani ni maadui, halafu hiyo mentality ikishafutwa, ndipo patakuwa na mazingira ya kuaminiana kati ya pande mbili, ambayo yataleta umoja na kusikilizana.

Huu ujuaji unaoendelea sasa hivi kwa watawala, wasiotaka kuwapa nafasi wapinzani ya kusema, kwa namna moja au nyingine unachangia kuidumaza nchi yetu kimaendeleo.

Kwasababu majukwaa ya kusemea wanayonyimwa wapinzani, yangetumika kuleta fikra mpya za kuinasua nchi yetu toka hapa tulipo, lakini bahati mbaya, watawala wetu wao wanawaza siasa tu muda wote.

Ajabu wanakwambia baada ya uchaguzi tuache siasa tufanye kazi, kazi zenyewe wanataka kuzifanya wao tu bila kuruhusu mawazo ya wengine, wao ambao wameshathibitisha kwa vitendo wameshindwa kuwaondoa wale maadui watatu tangu tupate uhuru mwaka 1961, miaka zaidi ya 60 mpaka sasa!.
 
Mkuu yote hayo uliyoyaandika ni kweli na humu tumo tulioshuhudia neema hizo wakati huo
Miaka hiyo kulikuwa na meter za maji kila nyumba yenye uwezo wa kulipia maji, tulikuwa na landlines manyumbani na unaongea na operator anakuunganisha au unasikia mlio unapokea unaambiwa ni simu ya fulani

Maisha yote hayo na makampuni yote kulikuwa na kitu kimoja in common
Kulikuwa wizi hakuna kama wa leo

Na rushwa ilikuwa sio kubwa sana au hakuna kabisa sehemu nyingi

Nakumbuka wazee walikuwa wanajua haki zao kuliko vijana wa leo ambao neno lao ni moja tu kuiba sana na kuomba rushwa

Viongozi wa juu wakiwa waadilifu naapa hata wa chini watanyooka

Ila tatizo viongozi wengi ni waizi na wanahalalisha wizi kwa kuwahamisha toka sehemu moja kwenda nyingine kufukia mashimo

Hatutafika popote kama juu kumeoza
Dah!..nyie wakongwe mliishi vizuri mno.
 
Mtu mnafiki, mwongo, na ambaye hana uhuru wa mawazo huwa hagundui kitu chochote, akijitahidi ataishia kuiga na kukariri.

Moja ya sababu, wanasaikolojia wanasema kwa nchi ya China kutokufanya ugunduzi, na kuwa nchi ya copy and paste, ni wananchi wake kuelelewa katika mazingira yasiyoheshimu uhuru wa mtu.

Tanzania kuna wakati ilikuwa inaunganisha malori aina ya Scania, sasa hivi tumeishia kuunganisha pikipiki za China.

Kuna wakati tulikuwa tunaunganisha matrekta bora kabisa ya valmet, sahizi hatuunganishi hata power tiller.

Tulikuwa tunatengeneza baiskeli aina ya swala, baiskeli nzuri kabisa,sahizi hatutengenezi hata sindano ya cherehani.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza matairi bora kabisa yakijulikana General Tyre, sahizi tumebakia kuwa watumiaji wa matairi ya hovyo kabisa kwa ubora kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza mashuka bora kabisa toka kiwanda cha Mutex, siku hizi tumebakia kuwa watumiaji wa mashuka ya hovyo kabisa, yapo kama vikaratasi, kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza viatu bora vya ngozi toka kiwanda cha Moro Shoes, siku hizi tumebakia kuwa wanunuzi wa viatu duni kabisa toka China, ukijikwaa tu kimechanika au kuraruka.

Tulikuwa tunatengeneza ndoo za ubora wa hali ya juu, Amboni Plastics, siku hizi tumebakia na ndoo takataka ukibebea tu maji, mshikio unachomoka au ndoo yenyewe kupasuka.

Wakati ule ilikuwa kipimo cha umaskini kwa mama ni kuvaa kanga iliyotengenezwa China au India, huku mwenye uwezo akivaa kanga ya Urafiki, leo hata ukiwa na hela, kanga nzuri huipati popote, kila mahali ni takataka za kutoka China.

Zamani, katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi angalao ilikuwa inaonekana kuwa na demokrasia, leo ndiyo nchi ya mfano kwa utawala usiozingatia sheria, usioheshimu mgawanyo wa mihimili. Tena imekuwa ni nchi ya kidikteta ambayo hata kura ya mwananchi haina maana yoyote katika kuwapata viongozi.

Kenya tuliokuwa tunawaona hawajastaarabika kwa kuendekeza siasa za ukabila, sasa ni nchi ya mfano Afrika Mashariki kwa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia, haki za watu, uhuru wa maoni, na katika kuheshimu mfumo wa siasa za vyama vingi.

Wakati wenzetu, kuendelea inamaanisha kuboresha, sisi kuendelea inamaanisha kuendeleza uharibifu. Tumekuwa Taifa bandia, taifa linaloongozwa kwa hadaa na ulaghai. Majukwaani wanatamka vingine, matendo yanakuwa kinyume. Wateule wamebakia kuumsifia anayewateua kwa unafiki. Kila mahali watasimama na kumsifia aliyewateua ili awaone na kuwasikia, wakiachia mic, wanamsema vibaya. Unafiki mtupu.

Watawala, hata pale ambapo mambo yanaenda vibaya, watakuambia kuwa sasa ndiyo tunapaa, wakati hata vyandarua vya mbu tunapewa msaada. Zamani, Serikali ilikuwa na watu wanapita mitaani kufanya fumigation kuua mbu na mende, leo tunashindwa hata kununua chanjo kwaajili ya watoto wetu wanaozaliwa.

Ni nani atalirudisha Taifa kutoka kwenye unafiki kulipeleka katika uhalisia? Nani ataweza kusimama na kusema kuwa Taifa letu ni duni katika nyanja nyingi, tusimame, turudi na kuanza upya?

Siku zote hatua ya kwanza kuleta mabadiliko chanya ni kuutambua na kuukubali udhaifu wako.
Bams: umeandika kitu sana mkuu.
Tuongezee na haya, kulikuwa na kuwanda cha Viberiti kilikoenda wanajua, pale Moshi kulikuwa na Tanangozi. Pia kuwanda cha kahawa coffee curing, yamebakia majengo tu tena chakavu mbaya na sijui kama Kuna uongozi pale je wanalipwa mshahara Toka wapi wakati kahawa zimeteyuka Kwa Kasi.! Iko siku Yale majengo yatauzwa Kwa mwekezaji au mtajiri awekeze Hoteli pale kama ilivyokuwa Moshi Hoteli.
Nchi hii ni ya ajabu sana isitoshe wanapeana madaraka ni mchwa hatari!!
 
Acha kupotosha kama huijui historia, maneno hayo haya kutamkwa na marehemu Christopher Kasanga Tumbo bali mtu mwingine.
Kajifunze upya au acha kudandia

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Amejichanganya bila shaka! Maana anayehusishwa na hayo matamshi ni mwana ccm mwenzao Tuntemeke Sanga, aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Makete kwa miaka mingi! Na wala siyo huyo Christopher Kasanga tumbo.
 
Mtu mnafiki, mwongo, na ambaye hana uhuru wa mawazo huwa hagundui kitu chochote, akijitahidi ataishia kuiga na kukariri.

Moja ya sababu, wanasaikolojia wanasema kwa nchi ya China kutokufanya ugunduzi, na kuwa nchi ya copy and paste, ni wananchi wake kuelelewa katika mazingira yasiyoheshimu uhuru wa mtu.

Tanzania kuna wakati ilikuwa inaunganisha malori aina ya Scania, sasa hivi tumeishia kuunganisha pikipiki za China.

Kuna wakati tulikuwa tunaunganisha matrekta bora kabisa ya valmet, sahizi hatuunganishi hata power tiller.

Tulikuwa tunatengeneza baiskeli aina ya swala, baiskeli nzuri kabisa,sahizi hatutengenezi hata sindano ya cherehani.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza matairi bora kabisa yakijulikana General Tyre, sahizi tumebakia kuwa watumiaji wa matairi ya hovyo kabisa kwa ubora kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza mashuka bora kabisa toka kiwanda cha Mutex, siku hizi tumebakia kuwa watumiaji wa mashuka ya hovyo kabisa, yapo kama vikaratasi, kutoka China.

Kuna wakati tulikuwa tunatengeneza viatu bora vya ngozi toka kiwanda cha Moro Shoes, siku hizi tumebakia kuwa wanunuzi wa viatu duni kabisa toka China, ukijikwaa tu kimechanika au kuraruka.

Tulikuwa tunatengeneza ndoo za ubora wa hali ya juu, Amboni Plastics, siku hizi tumebakia na ndoo takataka ukibebea tu maji, mshikio unachomoka au ndoo yenyewe kupasuka.

Wakati ule ilikuwa kipimo cha umaskini kwa mama ni kuvaa kanga iliyotengenezwa China au India, huku mwenye uwezo akivaa kanga ya Urafiki, leo hata ukiwa na hela, kanga nzuri huipati popote, kila mahali ni takataka za kutoka China.

Zamani, katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi angalao ilikuwa inaonekana kuwa na demokrasia, leo ndiyo nchi ya mfano kwa utawala usiozingatia sheria, usioheshimu mgawanyo wa mihimili. Tena imekuwa ni nchi ya kidikteta ambayo hata kura ya mwananchi haina maana yoyote katika kuwapata viongozi.

Kenya tuliokuwa tunawaona hawajastaarabika kwa kuendekeza siasa za ukabila, sasa ni nchi ya mfano Afrika Mashariki kwa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia, haki za watu, uhuru wa maoni, na katika kuheshimu mfumo wa siasa za vyama vingi.

Wakati wenzetu, kuendelea inamaanisha kuboresha, sisi kuendelea inamaanisha kuendeleza uharibifu. Tumekuwa Taifa bandia, taifa linaloongozwa kwa hadaa na ulaghai. Majukwaani wanatamka vingine, matendo yanakuwa kinyume. Wateule wamebakia kuumsifia anayewateua kwa unafiki. Kila mahali watasimama na kumsifia aliyewateua ili awaone na kuwasikia, wakiachia mic, wanamsema vibaya. Unafiki mtupu.

Watawala, hata pale ambapo mambo yanaenda vibaya, watakuambia kuwa sasa ndiyo tunapaa, wakati hata vyandarua vya mbu tunapewa msaada. Zamani, Serikali ilikuwa na watu wanapita mitaani kufanya fumigation kuua mbu na mende, leo tunashindwa hata kununua chanjo kwaajili ya watoto wetu wanaozaliwa.

Ni nani atalirudisha Taifa kutoka kwenye unafiki kulipeleka katika uhalisia? Nani ataweza kusimama na kusema kuwa Taifa letu ni duni katika nyanja nyingi, tusimame, turudi na kuanza upya?

Siku zote hatua ya kwanza kuleta mabadiliko chanya ni kuutambua na kuukubali udhaifu wako.
Hapo kwa china kukopi na kupeste umeingia cha kike hauawezi kulinganisha China na mambo ya jijinga hiyo ndo democrasia yao waliyojiamulia sio lazima wawaige wamagharibi
 
Kipindi hicho tulikuwa na Rais kiongozi sahivi tuna Rais mtawala
 
Kwa sasa hivi hatutapiga hatua hata moja tena kwa jinsi watu walivyo waroho

Unakuta kila mmoja anataka kazi ili aibe
Sasa riziki unayopewa halafu unaomba rushwa halafu hela unalisha familia kwa hela za dhulma unategemea nini

Hizi hela zina laana na wanaokula ni mlolongo wa laana tu kwani ni nuksi
Cha ajabu kutwa PM anaita waandishi wa Habari na kuwakosoa wabadhirifu ila mwisho wa siku huoni la maana analofanya

Watu hawafungwi kwa sababu wote ni waizi
Mwizi hamfungi mwizi
Utamfungaje mtu ambaye alikusaidia kuingia madarakani kwa rushwa
 
Kwa sasa nchi haina kiongozi anayeweza kujipiga kifua kuwa anaongoza vita dhidi ya rushwa na ufisadi kama alivyofanya Sokoine
 
Back
Top Bottom