Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,060
- Thread starter
- #61
Nazikumbuka siku zile. Nilikuwa shule ya msingi. Daftari limeisha u aenda nalo, store keeper anatoboa kwa kutumia punching machine, unapewa daftari jipya, kalamu unapewa, kitabu unapewa.Never mkuu
Labda tuache ushirikina na wizi
Waliokuwa sekondari, wanakwenda na kurudi makwao kwa gharama ya Serikali.
Nimefika Sekondari, utaratibu ni ule ule, unapewa daftari, tena kubwa zaidi na zuri zaidi kuliko yale ya shule za msingi. Asubuhi chai kwa viazi mviringo, saa 4 asubuhi wakati wa break, mnapata maziwa. Wakati wa likuzo unapewa cash money kwenda na kurudi.
Kufika chuo kikuu unakuwa tajiri mdogo, nauli unapewa ya daraja la pili (zaidi ya nauli ya basi kwa sababu basi ni daraja la 3), mwisho wa mwezi una high learning allowance, una faculty requirements allowance, una book allowance, na una meal allowance. Wakati mwingine unaambiwa kuwa kuna arrears, eti wakati unalipwa travel allowance, nauli ziilikuja kupanda baadaye, wewe mwebyewe mhusika huna hata habaru. Sisi wengine, allowance za UDSM mpaka tuliwasomeshea wadogo zetu private secondary schools.