Wenzangu mnawezaje kuacha?

Wenzangu mnawezaje kuacha?

Gwele

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2016
Posts
2,761
Reaction score
3,510
Kipindi cha miaka miwili nyuma nilipata demu kwa jina Emmy huyu dada sikumpenda ila nilimtongoza kwakua nilikuwa na uhitaji wa huduma mara kwa mara kabla sijampata mpenzi wa maisha

Emmy alinizoea sana na ndani ya miaka miwili upendo wake kwangu ulikuwa juu sana kuliko awali na akaanza kuzungumzia plan za baadaye na mimi kitu ambacho kilianza kuniwazisha kwan sikuwa na mipango hiyo.

Sasa juzi hapa niliamua kumwandikia message kumwambia mm nategemea kuoa mwakani nimeshapata mtu mwengne aisee huyu dada alilia sana na kutoa lawama mpaka nikajihisi mimi ni shetani yaani kila ninavyojitahidi kumbenbeleza maneno anayoniambia ni yananichina maana alipiga, simu akiwa anaongea analia et "muda wote ulikuwa unanichezea gwele kumbe huna malengo na mimi" yaani najikuta namuonea huruma maana hajanikosea ila simpend tu tayari nina mke wangu mtarajiwa na nampenda sana. Hebu naomba msaada wa kuachana na Emmy na kuziepuka hizi laana nitumie mbinu gani wajameni
 
Kimsingi umeamua kuumiza moyo wa mtu kwa makusudi

Nawish binadamu tuwe tunapendana milele,yaani mfano nikianzisha mahusiano na mtu basi ndio awe huyo huyo hadi mpaka kifo

Asa wewe umemkoleza dada wa watu kakupenda kweli halafu unataka kumuacha tena....sio vizuri
 
Kimsingi umeamua kuumiza moyo wa mtu kwa makusudi

Nawish binadamu tuwe tunapendana milele,yaani mfano nikianzisha mahusiano na mtu basi ndio awe huyo huyo hadi mpaka kifo

Asa wewe umemkoleza dada wa watu kakupenda kweli halafu unataka kumuacha tena....sio vizuri
Joanah ni bora unisaidie maneno yako na wewe yanazidi kuniumiza na kujiona mkosaji ukweli ni kwamba huyu dada sikuwa na mipango ya kumuoa toka tunaanza mahusiano ila huwezi mueleza mtu jambo kama hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom