Wenzangu mnaishije na jirani anayefungulia sabufa hadi mwisho

Wenzangu mnaishije na jirani anayefungulia sabufa hadi mwisho

Hapa nilipo tupo wapangaji nane sasa kama tukisema wote tushindane kwa kufungulia sauti hadi mwisho wote si tutaonekana vichaa
Hapakufai hapo. Kodi ikiisha hama, hela yako isikutese. Mkataba niliowapa wapangaji wangu ni marufuku kuwa kero kwa wapangaji wengine au majirani. Nikiletewa taarifa ya mpangaji wa aina hio mkataba wake ukiisha naachana nae.
 
Nilichogundua wengi wa watu design hiyo wana stress na maisha magumu sana so huwa wanapambana kuitafuta furaha kilazima kupitia mziki wa sauti kubwa....chunguza hii utagundua
Cha pili mtoa mada epuka sana kuishi nyumba za bei rahisi,nyumba nyingi za kupanga za bei chee huwa zinakusanya watu wenye maisha magumu na misongo na access nyepesi ya furaha kwao kuipata ni muziki wa fujo.
 
Huwa tunamuambia punguza sauti, akikaidi tunatoa onyo kali. Hata tv huwa tunawaambia waweke sauti isiyotoka nje ya vyumba vyao. Sie wenyewe tuna sabufa ila tunafungulia sauti ya chini ili tusiwe kero kwa wenzetu
 
Hakuna haja ya kugawana majengo
Fanya hivi
Kanunue pilipili ya unga nusu kilo na mkaa wa buku mbili

Mwache apige mziki wake mpaka achoke.. Akimaliza na kujiandaa kulala wewe washa mkaa uiikolea mwaga pilipili funga chumba chako toka nje
Mpaka hapo watakua wamegawana majengo, mmoja kwa mwenye nyumba mwingine kwa jirani. Na uwe na Roho kwelikweli
 
kuna dogo alikuwa anahiyo tabia anafungulia bufa keleletu, nikaongea nae akawa anaendelea tu na makelele yake, basi hakujua mimi nina sony home theater namcheki tu anavyoleta dharau.

kuna siku akafungulia na mimi nikamuwashia ebanaee mziki wake ukamezwa ukawa hausikiki nikaona amezima bila hata ya kumwambia tena, na toka siku hiyo hakuwahi kupiga muziki sauti ya juu
Nilikua napata shida kujua BUFA ni kitu gani, comment yako imenifungua .
 
Toa taarifa kwa mwenye nyumba...

Na eleza msimamo wako kwake kwamba kama asiporekebishika basi utaachia nyumba...

Washawishi na wapangajo wengine watoe malalamiko kama ya kwako na maamuzi kama ya kwako...

Naamini mwenye nyumba ataona badala ya kupoteza watu 5, ni heri apoteze mmoja mkorofi...
 
Kodi nguo za kianajeshi alafu mgongee mlango kwa nguvu sana kama unataka kuvunja kisha ongea lugha ya kimamlaka "dogo next time ukirudia tutaenda wote kikosini" Hatothubutu

Ila fatilia kazi yake kwanza akiwa na yeye mjeda umeyakanyaga.
 
Nawe larecord ile nyimbo mama Amina k......mako unafungulia hadi mwisho alafu unaenda Mikadi Beach kule mpk jioni unaurudi hoi.

Kila mtu ukirudi atakutazama jicho la kwanini lkn wewe jamani

Weee teeena bize na pensi yako unaosha sufuria ya ugali ya jana ili ubandike nyingine na paja la kwa joti chips.

Na vitoto vyao vyooote watavilaza mapema maana kutwa wataimba huo mwimbo.

Ushenzi ushenzi tuuu uswahilini ubabe tuuuu
 
Kitambo kidogo rafiki zangu fulani walinipa story kwamba katika hali hiyo baada ya majadiliano kuto fua dafu, wafunga spika kubwa sana na kufungulia taarifa ya habari
 
Back
Top Bottom