Wenza wa watumishi wa Serikali nao walipwe Mafao

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
628
1,644
Kama mwenza wa Rais anapata kiinua mgongo hata watumishi wengine wana haki kwa sababu mwenza wa Rais sio mtumishi wa serikali iweje apewe malipo na serikali? Kama hoja ni kumtuliza Rais hata engineer anatulizwa na mkewe au mumewe arudipo nyumbani.
 
Nakazia
 
Tungekuwa na mahakama hili wala lisingesumbua vichwa vyetu.
 
Cha MSINGI kuwe na ndoa halali.hili lazima liingie Bunge la bajeti lijalo.shauli yenu wazee wa KATAA NDOA.watu wanaenda kulamba shavu.wananchi wanasikilizwa sana SASA HV na Keri zinatatuliwa.
 
Kama mwenza wa Rais anapata kiinua mgongo hata watumishi wengine wana haki kwa sababu mwenza wa Rais sio mtumishi wa serikali iweje apewe malipo na serikali? Kama hoja ni kumtuliza Rais hata engineer anatulizwa na mkewe au mumewe arudipo nyumbani.
Kama ni kutumikia Nchi sote tunaitumikia.

Na wake wa Wakulima pia walipwe mafao.
 
Kama mwenza wa Rais anapata kiinua mgongo hata watumishi wengine wana haki kwa sababu mwenza wa Rais sio mtumishi wa serikali iweje apewe malipo na serikali? Kama hoja ni kumtuliza Rais hata engineer anatulizwa na mkewe au mumewe arudipo nyumbani.
Kwanza nianze kwa Kumshukuru Mh Rais Samia!
Pili naunga mkono hoja hata wake wa watunza bustani za ikulu walipwe mafao!
 
Kama mwenza wa Rais anapata kiinua mgongo hata watumishi wengine wana haki kwa sababu mwenza wa Rais sio mtumishi wa serikali iweje apewe malipo na serikali? Kama hoja ni kumtuliza Rais hata engineer anatulizwa na mkewe au mumewe arudipo nyumbani.

Hii isichukuliwe kama mzaha. Wananchi walitakiwa kuishikilia hoja hii kwa nguvu zote, na ikibidi hata kuandamana bila kikomo mpaka ama Serikali ikubali au la ule upuuzi wa mafao ya wake wa Marais ufutwe, kwa maana Rais pamoja na mke wake ni binadamu na ni raia wa Tanzania kama walivyo Watanzania wengine.

CHADEMA, maandamano awamu ya pili yawe ya kupinga ubaguzi na upendeleo unaofanywa na watawala na kuungwa mkono na baadhi ya majangili ya CCM. Ni wakati wa wanaCCM wanaoipenda nchi yao kujitenga na watawala wanyonya damu na jasho la Watanzania.
 
Binafsi sisemi wasipewe lakini naiangalia tu hii Dunia yetu najiuliza mambo mengi sana. MAMBO MAKUBWA YENYE KUSHANGAZA NA KUSTAAJABISHA.

Ila ninawaza ni kwanini mke wa DAKTARI asilipwe mafao kutokana na ugumu wa kazi ya mume wake. Mwanamke wa DAKTARI ana kazi kubwa sana ya kumuhudumia mwenza wake kimwili na kisaikolojia maana mtu anarudi nyumbani hana mood kabisa kutokana na kumuhudumia mgonjwa mwenye changamoto za ajabu

MAMBO YANAYOENDELEA KWA BAADHI YA NCHI HAPA DUNIANI HUWA NAWAZA NA KUTAMANI NI HERI MWENYEZI MUNGU AIFANYIE MAREKEBISHO HII DUNIA ILI DUNIA IPATE WATU WATAKAOGUSWA NA MAISHA YA WENZAO NA SIO WAO TU. ALETE WATAWALA WA AINA YA NYERERE AMBAO HAWATAJIANGALIA WAO BALI WATAKAOWAANGALIA WANANCHI WAO.

NI KWELI Mwananchi wa kawaida au mtumishi huwezi kuwa na privilege sawa na Rais, Waziri, Mbunge nk, lakini huwa nikiangalia maslahi ya viongozi wetu halafu bado familia inapigania nayo ilipwe daaah!!!!! Nikiangalia mafao ya wabunge wetu baada ya miaka mitano nikilinganisha na wanachokifanya bungeni daaah!!!! Kwanza sijawahi kuona wabunge wakisimama kwa nguvu moja kuwatetea watumishi wa uma kuboreshewa maslahi.

MUNGU WA MBINGUNI IANGALIE NCHI YAKO YA TANZANIA . IPATIE VIONGOZI WAKILA NYAMA BASI NAO WATATAMANI WANANCHI WA NAO WALE NYAMA
 
Back
Top Bottom