peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 13,007
- 21,725
Wasikilize…
Wenyeviti wa Vijiji huko Ngorongoro wamesema walipewa muda mdogo kusikilizwa na waziri Mkuu katika Mkutano. Na wamesema hawajakubaliana kuondoka eneo hilo kama ilivyoonekana kwa baadhi ya watu ambao walionesha kuwa tayari kuondoka katika hifadhi hiyo.
===================
NGORONGORO: WAKAZI WAOMBA KUKAA MEZANI NA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHWA
Wakati zoezi la kuwahamisha kwa hiyari baadhi ya Wananchi kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera Mkoani Tanga ikianza leo Juni 15, 2022, upande wa pili baadhi ya Wakazi wa eneo hilo wameomba kukutana na Serikali.
Wenyeviti wa Vijiji wa Ngorongoro wametoa tamko la kuomba kukaa meza moja na Serikali ili kutatua changamoto zinazokabili hifadhi hiyo kwa lengo la kuboresha mpango wa matumizi ya hifadhi hiyo.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema Kaya 296 zimejiandikisha ili kuondoka katika eneo hilo. “Awamu ya kwanza itahusisha mifugo, mali na wao wakazi husika, Kuhusu makazi yao ya Ngorongoro hatutayagusa, watabomoa wao wenyewe kwa hiyari yao,” – Mongella