Wenyeviti wa vijiji Ngorongoro wasema hawajakubaliana kuondoka, Hawakusikilizwa na Waziri Mkuu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,830
21,460
Wasikilize…

Wenyeviti wa Vijiji huko Ngorongoro wamesema walipewa muda mdogo kusikilizwa na waziri Mkuu katika Mkutano. Na wamesema hawajakubaliana kuondoka eneo hilo kama ilivyoonekana kwa baadhi ya watu ambao walionesha kuwa tayari kuondoka katika hifadhi hiyo.



===================
NGORONGORO: WAKAZI WAOMBA KUKAA MEZANI NA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHWA

Wakati zoezi la kuwahamisha kwa hiyari baadhi ya Wananchi kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera Mkoani Tanga ikianza leo Juni 15, 2022, upande wa pili baadhi ya Wakazi wa eneo hilo wameomba kukutana na Serikali.

Wenyeviti wa Vijiji wa Ngorongoro wametoa tamko la kuomba kukaa meza moja na Serikali ili kutatua changamoto zinazokabili hifadhi hiyo kwa lengo la kuboresha mpango wa matumizi ya hifadhi hiyo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema Kaya 296 zimejiandikisha ili kuondoka katika eneo hilo. “Awamu ya kwanza itahusisha mifugo, mali na wao wakazi husika, Kuhusu makazi yao ya Ngorongoro hatutayagusa, watabomoa wao wenyewe kwa hiyari yao,” – Mongella
 
Ardhi tukufu za asili za wakristo zinaibiwa kupokonywa na kupewa waarabu. Wakristo ni wakati wa kumpigania Yesu sasa hivi. Hatutaki najis kwenye ardhi zetu.

We will fight for what is rightfully ours.

Jesus Forever!

adriz
Hao wamasai huko sio wakristu.
Kwa hiyo nakushuri wewe utangulie huko kuupigania huo ukristu wako badala ya kuupigania kwenye Smartphone
 
Hao wamasai huko sio wakristu.
Kwa hiyo nakushuri wewe utangulie huko kuupigania huo ukristu wako badala ya kuupigania kwenye Smartphone
Umemchek huyo 'die hard' Christian kwenye video kitu rosary kinaning'inia shingoni?
 
Hao wamasai huko sio wakristu.
Kwa hiyo nakushuri wewe utangulie huko kuupigania huo ukristu wako badala ya kuupigania kwenye Smartphone
Mkuu usinichukulie poa kabisa. Cheki mida ya jioni navyoitendea haki black belt yangu.
Screenshot_20220610-093602_Chrome.jpg

ngenya Kashaulo
 
Hili ni balaa kubwa sana,ni wakati muafaka Serekali ikalitafakari kwa umakini mkubwa.Ziara ya Mama huko Omani pamoja na masuala mengine mikataba ya madini,Utalii na Kilimo ilitiwa saini.

Kipengele cha UTALII ndio kimenitisha sana,isijekuwa Wamaasai wanaondolewa halafu Mwarabu anapewa ardhi yetu kwa kisingizio cha uhifadhi.
 
Hao wenyeviti wasome kwa makini katiba katika kipengele cha ardhi. Serikali imeamua kutumia ardhi yake, mwananchi ni mpangaji tu. Leta katiba mpya ili ikupe haki.
Hiki kipengele kinatumiwa kinyonyaji ili kuwafaidisha wajomba arabuni na kuwaumiza wenyeji wa maeneo hayo.

Sio fair.
 
Serikali ichambue masai wote wa Tanzania wapelekwe handeni ili kuondoa wakenya wanaosumbua huko.........yaani kunya land wame complicate swala zima na NGO zao uchwara na serikali isiwalegezee hawa manyang'au kutaka kutuzoea.
 
Hii komenti imeondolewa...
👇🏾

Maghayo said:
Ardhi tukufu za asili za wakristo zinaibiwa kupokonywa na kupewa waarabu. Wakristo ni wakati wa kumpigania Yesu sasa hivi. Hatutaki najis kwenye ardhi zetu.

We will fight for what is rightfully ours.
 
Kivipi, kwa hiyo unafurahia wakenya kuendelea kujinafasi huko ngorongoro na makundi yao ya ng'ombe kwa lengo la kudumaza utalii wa Tanzania, unazo akili kweli wewe au ni mamluki.....
I better be mamluki kuliko huu upupu unaongea....
 
Habari za uzushi hizi kutoka ngorongoro waziri mkuu amesema mbona kupo shwari tuu
 
Back
Top Bottom