Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
WANACHAMA WA MWANZO WA TANU WALITOKA RUFIJI
Shughuli ya usajili wa TANU ilifanywa na watu watatu wenye kadi zinazoongozana: Julius Nyerere kadi no. 1, Ally Sykes kadi no. 2 na Abdul Sykes kadi no. 3.
Walikubaliana Nyerere akasajili chama kwa msajili kisha wote watatu wakutane nyumbani kwa Ally Sykes Kipata Street.
Taarifa alizokujanazo Nyerere ni kuwa msajili amekataa kuisajili TANU na sababu Nyerere alishindwa kuonyesha orodha ya wanachama.
Abdul akasema atafutwe Said Chamwenyewe.
Said Chamwenyewe alipofika kwa Abdul Sykes akapewa rejesta buku na kadi za TANU aende Rufiji akaandikishe wanachama.
Said Chamwenyewe alikwenda Rufiji anaendesha baiskeli akarudi na rejesta buku ina orodha ndefu ya wanachama wapya wa TANU na fedha za manunuzi ya kadi.
Rejesta buku akamkabidhi Abdul Sykes na fedha za kadi akamkabidhi Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa TANU.
Nyerere aliwasilisha orodha ya wanachama kwa msajili na TANU ikasajiliwa.
TANU ilipata usajili mwezi November 1954. Kwa nini ilikuwa kazi rahisi kupata wanachama wa TANU Rufiji?
Rufiji takriban wenyeji wake wote ni Waislam na wafuasi wa Tariqa Qadiriyya. Khalifa wa Qadiriyya, yaani Kiongozi Mkuu alikuwa Sheikh Hassan bin Ameir.
Hawa wafuasi wanafahamika kwa jina la "Murid," na sifa yao kubwa ni utii kwa kiongozi wao.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee toka 1950 na mwanachama wa TANU mstari wa mbele 1954.
Said Chamwenyewe alikuwa mwenyeji wa Rufiji na Qadiriyya kama walivyokuwa Warufiji wengi. Hii ilifanya kazi yake ya kueneza TANU Rufiji kuwa nyepesi sana.
Picha ya kwanza kushoto ni Said Chamwenyewe na picha ya pili angalia mshale. Picha ya tatu Said Chamwenyewe wa mwisho kulia waliokaa.