Wenyeviti wa Bunge wote wako wapi?

Wenyeviti wa Bunge wote wako wapi?

Katika hili nawaonea huruma wana UKAWA,,,

Siamin kama kweli vichwa vyoote vile vya upinzani vimemshindwa huyu dada....
Labda wewe ulitaka wamfanyaje?? Kumbuka hata wakati wa mama anna makinda haya yalikuwepo lakini alikuwa mwepesi sana kuhitaji maridhiano yule mama pamoja na mapungufu yake mengine lakin haikuwah kutokea kama ilivyinsasa

Sasa wewe unapo sema wamemshindwa ulitaka wamfanye wamvizie wampige? Au wamwagie tindikali? nini wakati huo kumbuka bunge sio ulingo wa ngumi au mieleka kwamba kutakuwa na ushind wa K,O huo ni utaratibu na ndio maana walikuwa wanatafuta mbinu mbalimbali za kueleza hisia zao maana bungen huwezi kumkwida mtu kabali maana kuna vyombo vya ulinzi utatolewa tu. Ref; mbunge wa mbeya( sugu) kwa hivyo ni swala la busara tu ikiwepo kutakuwa hakuna kutunishiana misuli.
 
Dada kichwa kweli. Kapata First Class ya Sheria Mlimani. Utalinganisha na kichwa kipi pale UKAWA?
Hiyo first class yake ya sheria imesaidia nini kwenye jamii ya watz? Au inakusaidia wewe na wenzio wenye mawazo sawa na mwenye first class ya sheria? Umuhimu wa elimu bora ni kutatua matatizo/changamoto zinazokabili jamii,sasa yeye angeanza kutatua changamoto za kutokuelewana na wabunge wa ukawa,hapo hiyo first class yake ingekuwa na value mbele ya watz wengi wanaojielewa!!
Lakini pole sana ndio maisha yalivyo kwa sasa,bila kujipendekeza maisha hayaendi!
Keep it up!!
 
Baada ya kuongoza karibu vikao vyote vya kujadili na kupitisha bajeti,Naibu Spika,Dr. Tulia Ackson,amechoka kimwili na kiroho. Anajipanga kuwapisha,kuongoza Bunge,wenyeviti watatu wa Bunge wakiwemo Chenge na Zungu.

Taarifa za kiintelijensia hapa Dodoma zinabainisha kuwa Dr. Tulia amewaambia watu wa karibu yake kuwa 'amesaidia vya kutosha na sasa anahitaji kupumzika'. Dr. Tulia anatajwa kama aliyetumika wakati wote wa bajeti 'kuwafukuza' Wabunge wa Upinzani kwakuwa Wabunge hao hawako tayari kuongowa nao Bungeni.

CCM na Serikali yetu tulimtumia Dr. Tulia ipasavyo katika kupunguza au kuondoa changamoto za Wabunge wa vyama vya upinzani wakati wa mjadala na kupitishwa kwa bajeti. Ni kusutwa kwa nafsi? Ni kuchoka kweli? Sasa wanarudi Chenge na Zungu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Katika kumtumia kwenu Tulia kama ulivyokiri hapo juu,je KUMTUMIA huko kuna faida gani za moja kwa moja kwa Taifa?

Maana kwa namna ulivyotiririka ni kama unafurahia hako ka mchezo.
 
Katika hili nawaonea huruma wana UKAWA,,,

Siamin kama kweli vichwa vyoote vile vya upinzani vimemshindwa huyu dada....
Ukiongeza elimu utajua kuwa hajashinda kwa kuwa na akili bali kwa kuwa yuko upande wa dola
 
Tumeleta ingizo jipya. Si sawa na UKAWA mnaookoteza wazee waliojichokea kama Lowasa, Kingunge, Sumaye, Mgana Msindai, Hamisi Mgeja nk
Uzuri wake ni kwamba ingizo hilo jipya linaiunguza nchi na cheche za moto wake zitakugusa wewe na ndugu zako!
 
Dada kichwa kweli. Kapata First Class ya Sheria Mlimani. Utalinganisha na kichwa kipi pale UKAWA?
Kuna DC Fulani aliingia kwenye mgogolo na kisha kupumzishwa kutoka wilaya fulani ya kasakazini mashariki baada ya kusema mwanasheria wake sijui ana degree ya nini vile nimesahau
 
Back
Top Bottom