Wenyeviti wa Bunge wote wako wapi?

saidi kindole

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
310
792
Sasahivi takribani wiki ya tatu sijaona mwenyekiti yoyote wa bunge akikalia kiti kuanzia asubuhi hadi jioni ni Naibu Spika tuu.

Je, wenyeviti akina Zungu, Chenge na wengine wamepigwa Ban?
 
Baada ya kuongoza karibu vikao vyote vya kujadili na kupitisha bajeti,Naibu Spika,Dr. Tulia Ackson,amechoka kimwili na kiroho. Anajipanga kuwapisha,kuongoza Bunge,wenyeviti watatu wa Bunge wakiwemo Chenge na Zungu.

Taarifa za kiintelijensia hapa Dodoma zinabainisha kuwa Dr. Tulia amewaambia watu wa karibu yake kuwa 'amesaidia vya kutosha na sasa anahitaji kupumzika'. Dr. Tulia anatajwa kama aliyetumika wakati wote wa bajeti 'kuwafukuza' Wabunge wa Upinzani kwakuwa Wabunge hao hawako tayari kuongowa nao Bungeni.

CCM na Serikali yetu tulimtumia Dr. Tulia ipasavyo katika kupunguza au kuondoa changamoto za Wabunge wa vyama vya upinzani wakati wa mjadala na kupitishwa kwa bajeti. Ni kusutwa kwa nafsi? Ni kuchoka kweli? Sasa wanarudi Chenge na Zungu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Back
Top Bottom