Baada ya kuongoza karibu vikao vyote vya kujadili na kupitisha bajeti,Naibu Spika,Dr. Tulia Ackson,amechoka kimwili na kiroho. Anajipanga kuwapisha,kuongoza Bunge,wenyeviti watatu wa Bunge wakiwemo Chenge na Zungu.
Taarifa za kiintelijensia hapa Dodoma zinabainisha kuwa Dr. Tulia amewaambia watu wa karibu yake kuwa 'amesaidia vya kutosha na sasa anahitaji kupumzika'. Dr. Tulia anatajwa kama aliyetumika wakati wote wa bajeti 'kuwafukuza' Wabunge wa Upinzani kwakuwa Wabunge hao hawako tayari kuongowa nao Bungeni.
CCM na Serikali yetu tulimtumia Dr. Tulia ipasavyo katika kupunguza au kuondoa changamoto za Wabunge wa vyama vya upinzani wakati wa mjadala na kupitishwa kwa bajeti. Ni kusutwa kwa nafsi? Ni kuchoka kweli? Sasa wanarudi Chenge na Zungu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)