Wenye nyumba kuweni waelewa

Kuna watu hawajui kudai yaani acha tu.. unaweza kuwa na ww unamiliki nyumba nzuri na nyingi au kubwa kuliko uliyopanga na unawapangaji vile vile..

Ila huko ulipopanga ww unaendeshwa na Mwenye nyumba.. 😅 mara nyingi wengi hawajui kudai hapo ndio nakosana nao sana.. na mtu unakuwa na jeuri maana na ww una yako kali kuliko hicho kibanda anachokunanga nacho.
 
Kuna muda wapangaji wenyewe wanazingua,nimempangisha dogo mmoja na mkewe wanajitafuta kimaisha.Maana hata sielewi wanachofanya,hajalipa Kodi yangu zaidi ya miezi minne sasa juzi naliuliza hela yangu vipi January hii lilivyokosa akili linanipandishia eti kuna wapangishaji wengine wanakaa hata miezi sita bila kusumbua nimeliambia ikifika tarehe 31 nisimuone.Hakuna asiyeelewa hali ya maisha ilivyo lakini ukishindwa kutimiza wajibu wako uwe hata na busara.
 
Wapangaji wengine wasumbufu.

Mfano, kodi inaisha tarehe 30, tareh 1 inabidi unilipe, inafika tareh 1 kimya, 2,kimya, 3,4,5 mpaka nakucheki mzee vipi kimya ndio anakwambia ooh, ana changamoto kidogo alikuwa anataka kukutafuta akueleze umvumilie, huyo utamuelewa kweli, kama umekwama we nipange mapemaa, tena ikiwezekana hata kabla ya tareh 30, kwenye 20+ huko niambie tu huelewi elewi, mie nakuwa najua kabisa kipi kinajiri. Sio ukae kimya tarehe 1 inafika na tena inavuka mpaka mie nikucheki.
 
Kujenga rahisi kumbe
Mbona kuna watu kibao wana nyumba za kupangisha na nyumba zao mbali. Hata mimi siwezi kuishi na wapangaji.
And mind you, nimesema pia ni bora ukapanga nyumba ambayo mwenye nyumba hategemei kodi ya nyumba kuendesha maisha yake.
Mtu kama huyo utakuta ana nyumba nyingi na haishi na wapangaji. Nazungumza kwa uzoefu wangu wa miaka niliyopanga.
 
Nakuombea siku na wewe uwe mwenye nyumba ili ujue wanayopitia


Real estate business in Tanzania ni pasua kichwa just imagine mtu akienda dukani analipa Cash na hata akikopa analipa ila akidaiwa na mwenye nyumba anaona anasumbuliwa

kuliko kujenga nyumba ya kupangisha zingatia location tu utoe lodge au fremu tu za biashara
 
Nakuombea siku na wewe uwe mwenye nyumba ili ujue wanayopitia


Real estate business in Tanzania ni pasua kichwa just imagine mtu akienda dukani analipa Cash na hata akikopa analipa ila akidaiwa na mwenye nyumba anaona anasumbuliwa

kuliko kujenga nyumba ya kupangisha zingatia location tu utoe lodge au fremu tu za biashara
wenye nyumba hawataki kutukopesha mbona tunawalipa 6 months mapema au hata mwaka hatulalamiki kuombwa kuvumilia mwezi tu anaona namuonea ah
 
Back
Top Bottom