Duh!! Mimi gf wangu alipekua simu yangu akakuta nimeandika jina lake na eneo analoishi, yaani kwa mfano Evelyn Salt kamanga ferry". Huo ugomvi wake balaa
Duuh hii mpyaa aisee seriously?? Poleepole yake ila msevu hata mama flani mm hata cjaseviwa namba tu imekaririwa kichwan
Ngekua ndo mie namind kimoyomoyo afu nawe nakusave "panya road"
Women! Women! Women!
Mentor bado nipo nipo kwanza....sipendi ugomvi..sipendi kupeana presha!!!
Japo jina lina ukakasi kidogo, lakini sioni ni kwa vipi imeweza kumpandisha hasira hadi kufikia ugomvi wa kiwango hicho. Ninachokiona ana mashaka na mienendo yako tangu mda mrefu na hii ni sababu tu ya kutoa kile kilichoujaza moyo wake. Kaa chini tafakari safari ya maisha yenu. Ugomvi mkubwa mpaka wa kupelekana kwa mchungaji hauwezi kuletwa na jina "Madam". Kuna sababu iliyobackground. Ichunguze
Wala hujakosea mkubwa. Kiusalama sio vizuri kumsevu mkeo wife, honey, mrs. Hizi simu za mkononi zina mengi, inaweza kupotea ikawa balaa. Kusevu baba, mama, haishauriwi. Mweleweshe tu, unaweza poteza simu ikaokotwa na wakora wakaona mrs wakamwita sehemu kitakachotokea huko utajuta kusevu mrs. Nina mifano hai mkuu
Umemdekeza sana. Hajachezea kichapo tu?
Kosa ni kuvunja ile simu yake. Je, yeye amekuandika vipi kwenye simu yake? (lakini ndio umeshaivunja hivyo!). Sasa huko kwa mchungaji usiku huu, na wachungaji wenyewe wa siku hizi. Kwani hamna waliowasimamia ndoa yenu, au ndio wale mnaowachagua kisa mkewe anaendana na umbo la bi harusi!!
Sio kila mtu anatoa presha bana. Kuna watu tunatoa raha mfano wake hakuna :mmph::wink1:
..am kaming ur way!!!!
Tatizo la teknolojia katika Afrika. Kwa wenzetu kila teknolojia ina utamaduni wake. Sasa kwetu ni shida kwani teknolojia imekuja bila utamaduni wake. Huyo mkeo anatatizo lingine sio simu. Anatafuta nafasi ya kulisema. Hujakosea hata chembe mkuu.
Naachaje kukupokea kwa mfano?!
Kabla ya kwenda mbali ningependa kukuuliza maswali 2. Kwa nini uvunje simu yake? Kwa nini umsev madam?. Majibu utakayopata ni sehemu kubwa ya tatizo katika ndoa yenu. Tukiachana na hayo niseme kitu kimoja, kitu kinachoonekana kidogo maisha ya kila siku basi katika mapenzi huonekana kikubwa. Leo ukimpigia sim rafiki yako asipopokea haitakuuma sana. Lakini asipopokea mpenzi wako unaweza usilale kwa mawazo. Kwa hiyo hivyo vitu unavyoviona vya kawaida vina impact kubwa sana. Leo kumsev mpenzi wako madam unaona kawaida lakin hujui jinsi gani imemuuma.kutomnunulia mpenzi wako simu wakati anajua uwezo huo unao, lazima itamuuma. Atahisi humpendi. Tujitahidi kutengeneza kumbukumbu nzuri kwa wapenzi wetu.