Wenye ndoa piteni hapa kwa ushauri

Wenye ndoa piteni hapa kwa ushauri

Kosa ni kuvunja ile simu yake. Je, yeye amekuandika vipi kwenye simu yake? (lakini ndio umeshaivunja hivyo!). Sasa huko kwa mchungaji usiku huu, na wachungaji wenyewe wa siku hizi. Kwani hamna waliowasimamia ndoa yenu, au ndio wale mnaowachagua kisa mkewe anaendana na umbo la bi harusi!!
 
mh watu tunatofautiana kuseviwa maadam timbwil namna hyo ningeeleza mi nayokutana nayo kweny ndoa ingekua ni yeye nahc ashafungasha cku nying
 
pole yake ila msevu hata mama flani mm hata cjaseviwa namba tu imekaririwa kichwan
 
Women! Women! Women!
Mentor bado nipo nipo kwanza....sipendi ugomvi..sipendi kupeana presha!!!

Presha he ndio mnazitaka
Yaani amsave mwenzie kwa jina la madam then madam amkenulie meno tuuuuu.
 
Last edited by a moderator:
Lakina mkuu kwanini haujampa heshima yake kama Mke hili neno madam haujalitumia mahali sahihi
 
hivi TCU hawajatoa majibu hawa watoto waende shule vioja vimezidi humu
 
Japo jina lina ukakasi kidogo, lakini sioni ni kwa vipi imeweza kumpandisha hasira hadi kufikia ugomvi wa kiwango hicho. Ninachokiona ana mashaka na mienendo yako tangu mda mrefu na hii ni sababu tu ya kutoa kile kilichoujaza moyo wake. Kaa chini tafakari safari ya maisha yenu. Ugomvi mkubwa mpaka wa kupelekana kwa mchungaji hauwezi kuletwa na jina "Madam". Kuna sababu iliyobackground. Ichunguze

Ameshasema mkewe anapenda kukumbushia mambo ya nyuma/zamani kwahiyo atakuwa ameongezea hapo kwenye issue ya jina.
 
Wala hujakosea mkubwa. Kiusalama sio vizuri kumsevu mkeo wife, honey, mrs. Hizi simu za mkononi zina mengi, inaweza kupotea ikawa balaa. Kusevu baba, mama, haishauriwi. Mweleweshe tu, unaweza poteza simu ikaokotwa na wakora wakaona mrs wakamwita sehemu kitakachotokea huko utajuta kusevu mrs. Nina mifano hai mkuu

Tusaidie mkuu,unashauri amsevuje?
 
Kosa ni kuvunja ile simu yake. Je, yeye amekuandika vipi kwenye simu yake? (lakini ndio umeshaivunja hivyo!). Sasa huko kwa mchungaji usiku huu, na wachungaji wenyewe wa siku hizi. Kwani hamna waliowasimamia ndoa yenu, au ndio wale mnaowachagua kisa mkewe anaendana na umbo la bi harusi!!

Matatizo ya ndoa huwa yanatatuliwa na mchungaji pamoja na mama mchungaji wakiwa pamoja...Btw sio wachungaji wote ni wahuni.
 
Tatizo la teknolojia katika Afrika. Kwa wenzetu kila teknolojia ina utamaduni wake. Sasa kwetu ni shida kwani teknolojia imekuja bila utamaduni wake. Huyo mkeo anatatizo lingine sio simu. Anatafuta nafasi ya kulisema. Hujakosea hata chembe mkuu.
 
Nakubaliana na wewe, naona dalili hizo, ila nimetulia, sjamuuliza tena tangu alivorudi wala hajaniliza kitu..still we not in good terms

Tatizo la teknolojia katika Afrika. Kwa wenzetu kila teknolojia ina utamaduni wake. Sasa kwetu ni shida kwani teknolojia imekuja bila utamaduni wake. Huyo mkeo anatatizo lingine sio simu. Anatafuta nafasi ya kulisema. Hujakosea hata chembe mkuu.
 
Sante kwa maswali yako mazuri.


Nimemsave madam sio kwa dhana mbaya, just imagine..ni sababu gani mkeo au mmeo akuite baba/mama, this means ni heshima tu lakini sio kwamba amekuzaa!..wala skuchukua muda kifikiri namna gani ya kusave jina lake.


Nilivunja hiyo simu maana alionyesha dharau. Imagine tuna watoto 3, wako boarding over 5 millions nalipa, bado ananiambia hahitaji hata kasimu kangu(ile yake niliivunja), nikaona huyu anataka kunigeuza mi hawala! Mbona nimeishi naye huu mwaka wa 17? Hata hivo nilivunja mpaka nikamwona ameanza kuteyemeka...kuna kitu amejifunza kwa uropokaji wake

Kabla ya kwenda mbali ningependa kukuuliza maswali 2. Kwa nini uvunje simu yake? Kwa nini umsev madam?. Majibu utakayopata ni sehemu kubwa ya tatizo katika ndoa yenu. Tukiachana na hayo niseme kitu kimoja, kitu kinachoonekana kidogo maisha ya kila siku basi katika mapenzi huonekana kikubwa. Leo ukimpigia sim rafiki yako asipopokea haitakuuma sana. Lakini asipopokea mpenzi wako unaweza usilale kwa mawazo. Kwa hiyo hivyo vitu unavyoviona vya kawaida vina impact kubwa sana. Leo kumsev mpenzi wako madam unaona kawaida lakin hujui jinsi gani imemuuma.kutomnunulia mpenzi wako simu wakati anajua uwezo huo unao, lazima itamuuma. Atahisi humpendi. Tujitahidi kutengeneza kumbukumbu nzuri kwa wapenzi wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom