Wenye ndoa piteni hapa kwa ushauri

Wenye ndoa piteni hapa kwa ushauri

Mambo ya kishule shule ndo yapi na ya kiutu uzima ndo yapi..
Kishuleshule ni honey, sweet, asali wa moyo, na kama hayo. Ya kiutu uzima ni miriam, juma, asha. Ndio heshima kwake. Andika jina lake.
 
You are really an intelligent,washauri wengi wameona kosa kwenye kuseviwa madam,hayo matamshi hawakuyaona. Na kuna thread humu huyu bwana alishalalamika kuhusu ukorofi wa mkewe,hilo la 'madam' ni muendelelezo wa muvi zao.

Basi kama ni hivyo huu ni upumbavu wa watu wazima kupotezeana muda bure.
 
uelewa tu tofauti,me mke wangu nimemsave "wife" lakin yeye namba zangu zote hajasave jina lolote toka uchumba,na sijawahi jisikia vibaya...ok,mpe elimu,mpe tena elimu na mwisho mpe elimu tena na tena.
 
Aisee mambo mengine ni complications zisizo na msingi, binafsi ikitokea nikao bas mke wangu nitam save kwa jina lake tu.
 
Wewe ni mwana ndoa mwenzangu....lakini inategemea na alivyopokea japokuwa jina Madam halina uzito na jinsi alivyokwako.....amini hata wewe ungekuwa saved GUY sijui ungejisikiaje,mfano mie mke wangu awali nilimsave Mama Jaz yaaan mama wa mtoto wetu ....lakin akaja akasema hapend ni msave hivyo yeye ni mke wangu hivyo anataka nimsave WIFE...nikaona yupo sawa pia hivyo nikamsave kama alivyopenda.....mpaka Leo tunaish kwa amani na furaha
 
Habari za keekend wapendwa.

Leo Jumapili nakwenda kuimaliza vibaya. Nikiwa nitulia hapa nyumbani mke wangu ameomba simu yangu ili ampigie mtu maana simu yake ilikuwa haina credit, nikampa mi nikaingia chumbani kupumzika, amekuja chumbani amefura, akauliza namba yake nimeisevu kwa jina gani?

Mi nikamjibu kuwa nimesevu kwa jina la "Madam" Hapo ndio kivumbi kikaanza, kwanini unasevu hivo? Mbona hujasevu mrs?Akaendelea," ina maana una mtu mwingine ndio mkeo? Huyo ndie ulie msevu mrs? Akaendelea tangu leo mi sio mkeo, na ndg zako waondoke hapa kwangu...."

Mi muda huo nilikuwa nimepigwa butwaa, namsikiliza, baadae nikamwambia kusevu jina hilo ni kukupa heshima, nikamwambia ile simu nyingine nimesevu kwa jina la 'mrs' wala sina maana mbaya.

Kwa kweli baadae akasema hata simu yake haina thamani maana ni ya hela ndogo (akimaanisha simthamini maana nimemnunulia simu ya bei ndogo), na kwa maana nyingine akimaanisha yupo mwanamke ninaye mthamini na ndie huenda nimemsevu kwa jina la 'mrs' akasema mambo mengi sana, lakini mi nikiangalia sijamkosea jambo kubwa kiasi cha maneno anayoyasema. Imefikia mahali nikaivunja simu yake.

Eti wanajanvi, ni kosa mkeo kumsevu kwa jina la 'madam' Nipeni mchango wenu tafadhari, maàna bado mgogoro upo na kwa sasa ameondoka sjui amekwenda wapi. Ila katika kufoka kwake nimemsikia akisema hii kesi anaipelwka kwa mchungaji, nadhani ameenda huko kupeleka kesi.

Nipeni ushauri tu ili niona namna ya kumaliza tatizo hili.

Hahahaaaa!Bora mkeo umemsave Madam aisee kuna mtu alimsave mumewe wa ndoa 'kidondandugu':laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh::laugh:
 
Madam is too formal bhana huwezi kumwita mkeo hvy, its yeye akwite SIR(mmmhhh sounds awkward) apologize n muonyeshe kwamba hukuwa n ufaham na uzito wa hilo neo. Tttz wanaume hawajui tu jaribu kuwaweka wake zenu wajifeel proud jmn
 
hahahahaaaaa!!! imebidi nicheke... mimi ni save utakavyo madam, mama Fulani, kwa jina mradi isiwe tusi, ila mwisho wa siku mimi ni mkeo na wewe ni mume wangu. hao wengine save utakavyo darling, honey, baby, sweetheart, ila mwisho wa siku ni michepuko tu. sioni kilichomkera mkeo kwa kweli. inawezekana pia ki cheap handset ni sababu, alikua anatafuta namna ya kuanza kukueleza. mnunulie iPhone 6 umalize ugomvi:A S wink:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom