Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 3,267
- 17,032
Umewahi kukutana na mtu ambaye ana kinyaa kilichopitiliza? Hali yake ya maisha vipi?
Ukweli ni kuwa, sisi binadamu ni wachafu kiasili. Na hii ni kutokana na ukweli kuwa huwezi kuwa msafi kwa asilimia zote. Maisha yetu ya kila wakati yanajumuisha uchafu. Mazingira na miili yetu huzalisha taka nyingi hivyo kuufanya uchafu sehemu ya maisha yetu.
Lakini, kuna watu ambao hali ile huwasababishia usumbufu wa kuchafukwa nafsi kwa namna moja ama nyingine.
Ambacho nimekishuhudia kwa watu wengi wenye kinyaa ambao nimewahi kukutana nao ni kwamba hawasadiki usafi. Yaani ni wachafu kuliko hata wale ambao wao wanaona kawaida.
Watu wenye kinyaa ni wavivu kuushughulikia uchafu husika badala yake wanaona namna ya kuuepuka ni kuukimbia. Badala ya kuondoa huo uchafu wanaukimbia.
Mtu anachukia harufu ya uani, badala ya kuchukua hatua kufanya usafi wanabaki kuziba pua na kuondoka sehemu husika. Huku akimsakazia jirani yake akafanye usafi.
Mtu hapendi kula au kutumia sahani moja na mwenzake kwa madai kuwa ni uchafu, ila ulaji wake wake unachefua mno.
Sawa, hakuna anayependa uchafu ila mwingine ni wa kawaida wala haudhuru.
Kinyaa chako kilandane na kiwango cha usafi wako.
Ila uwe na kinyaa cha kuzama kwa mpalange na chumvini, huko sipo kabisa. Pakimbie.