<Sikushauri,binafsi najuta!

Sikushauri,binafsi najuta!

unajuta nini.? Hauna uwezo wa kulipia*

Siku za karibuni nimekuwa nikipewa sifa za king'amuzi kuwa kuna channels bomba. Nimeanza kushawishika kununua, swali langu ni channels gani zinapatikana humo. Nimesikia TBC, Clouds TV, KBC zimo humo.

Je , ITV EATV zipo pia? Kuna channel za mpira?Zzipo za majirani zetu kama TVM? CNN?

Natanguliza shukrani

Yaani ilinilazimu kufunga dstv maana antenna niliipandisha juu sana kupata angalau channel ishirini sasa balaa linaanza mchana upepo ukitingisha antenna ndani full scratch channel zenyewe nazoziangaikia hazina kichwa wala miguu upuuzi mtupu nimelifungua liantenna na decoer yake vyote tupia darini.
Yaani katika mambo ambayo nimeshaingia kichwakichwa ni hili suala la kununua king'amuzi cha startimes. hawa jamaa kosa lao la kwanza ni kukosa coverage ya channels zote za ndani kama it, startv nk. kwa hiyo inakubidi ukitaka kucheck startv au itv inabidi unyofoe decorder uunganishe upya...it is total embarasment!!!Kwa channel za TZ itakubidi uwe na vingamuzi viwili
Usijaribu kupoteza pesa yako ndugu utaishia kujuta,nakushauri kama vipi wacheki ting au kama mifuko imetuna kimtindo wacheki dstv inakidhi haja zote.
Hawa Star Times wamekuja kikora kwelikweli, na walitupata sana mwaka jana walipotutishia kuwa hatuwezi kuona World Cup, tukaingia mkenge kwa foleni! Sasa tunajuta kwani channels zenyewe hazina mashiko kabisa...hakuna sports channel yoyote ya humu ndani ukiacha TBC1 na 2 pamoja na Channel10. zingine zote za maana hamna na sidhani kama wana mpango wa ku-connect na wengine karibuni. Tido ameondoka basi tusahau!
Hata hivyo wewe ni mtu mzima una maamuzi ya kufanya ukitaka kuingia kwao