Kuondolewa kwa Baadhi ya chaneli katika king'amuzi cha Azam, Nimkakati wa CCM ili watu watazame TBC.

Mar 6, 2017
33
135
Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu kutaka kujua nini hatima ya chaneli za ITV, Star TV, EATV, Clouds TV, Capital TV n.k kutopatikana katika king'amuzi cha Azam, nimekutana na mtonyaji toka Lumumba ambaye hapendezwi na kinachoendelea nchini kwa wakati huu na kuniambia kuwa ukimya wa serikali juu ya sakata hili ni kutaka watu watazame TBC hasa habari ambazo nyingi ni za chama dola.

Huu mpango ni kwasababu Azam inawapenzi wengi hivyo itakuwa ni fursaya pekee kwa chama na serikali kuonekana kwa watu.

Ndio maana kila mwezi kifurushi tunalipa elfu 18 lakini chaneli zaidi ya 6 za ndani ya nchi ( mfano ITV, Star TV, EATV, Clouds TV, Capital TV,Wasafi,n.k ) hazipatikani.

Mtonyaji anaongeza kuwa star times walichukuliwa hatua mara moja lakini Azam inakuwa ngumu sababu ni sehemu ya mkakati.
 
Yaan mawazo mengine bwana, dah inamaana Azam ndo alikuwa anaonesha local channels tu? Hakuna visumbuzi vingine kama Zuku na startimes?
 
Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu kutaka kujua nini hatima ya chaneli za ITV, Star TV, EATV, Clouds TV, Capital TV n.k kutopatikana katika king'amuzi cha Azam, nimekutana na mtonyaji toka Lumumba ambaye hapendezwi na kinachoendelea nchini kwa wakati huu na kuniambia kuwa ukimya wa serikali juu ya sakata hili ni kutaka watu watazame TBC hasa habari ambazo nyingi ni za chama dola. Huu mpango ni kwasababu Azam inawapenzi wengi hivyo itakuwa ni fursaya pekee kwa chama na serikali kuonekana kwa watu. Ndio maana kila mwezi kifurushi tunalipa elfu 18 lakini chaneli zaidi ya 6 za ndani ya nchi ( mfano ITV, Star TV, EATV, Clouds TV, Capital TV,Wasafi,n.k ) hazipatikani. Mtonyaji anaongeza kuwa star times walichukuliwa hatua mara moja lakini Azam inakuwa ngumu sababu ni sehemu ya mkakati.

Mbona hata dish la kawaida (analogy) ukiweka juu ya paa lako unazinasa vyema tu CAPITAL, STAR, ITV na EAT TV na channels zingine kibao kama Aljezeera, CNBC, BLOOMBERG, KBC Kenya, Mozambique TV nk nk bila shida tena bure hulipii chochote?
 
TV suku hizi imekuwa ya kuangalizia mpira na tamthilia tu. Mambo ya habari hakuna anayesikiliza. Habari tunapatia kwenye magroup ya WhatsApp na social media. Walijaribu kuingia kwenye WhatsApp wakashindwa. Huko kwenye TV watafanikiwa kuua biashara na kudidimiza uchumi tu, ila siyo kupata wasikilizaji wa habari za CCM.
 
Write your reply...Inachosha yaani nilikuwa nalipa 18000 kwa mwezi naangalia channel zote baadhi ya chaneli zimeondolewa lakini nalipa ile ile sasa hapa serikali inamsaidia mwanchi au inatukandamiza?
 
Wakitaka kufaulu waifungie mitandao nani anaangalia tbccm, Jana tu sababu ya mpira, ukiwa na mawazo ya Miaka 47 sio wote wawe na mawazo yako
 
Hbr kamili watu uzipata kwenye mitandao magazeti na hizo TV watu wanaangalia habari za michezo
 
Back
Top Bottom