Namshakende
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 860
- 2,256
Hivi nyinyi watu mnaokwenda baa halafu mnaagiza chupa moja tu ya maji na kukaa nayo zaidi ya masaa matatu, kichwani zinawatosha kweli? 😂
Wenye baa, wekeni utaratibu mpya au mpandishe bei ya maji! Mtu hawezi kukalia meza masaa matatu kwa matumizi ya shilingi elfu moja au elfu mbili huku wateja wenye hela za kutumia wakikosa nafasi.
Hawa mabingwa wa kukalia viti wanajaza baa bure!
Halafu bado utamsikia 🤥,
“Mimi huwa napenda tu kwenda baa kupumzisha akili” au “mimi ni mgonjwa, situmii pombe.”
Kupumzika gani bwana?
Hivi kweli mtu anayeumwa sehemu yake sahihi ya kwenda kupumzika ni baa kwenye kelele za spika, moshi wa sigara, na taa za disco?
Kama unaumwa au upo kwenye dozi, si ubaki nyumbani kwako kwenye utulivu mpaka upone? Umeenda kufanya baa ya watu kuwa sebule yako!
Kumbuka, wenye baa wapo kwenye biashara, sio huduma za jamii au asasi za kutoa misaada! Mwenye baa ana bili za umeme zinazotakiwa kulipwa, anapaswa kulipa mishahara ya wahudumu na walinzi, anastahili kulipia ada za taka, kodi za serikali, na uendeshaji wa eneo zima.
Unapokalia meza masaa manne na chupa yako moja ya maji ya buku, hizo bili unataka akazilipe kwa kutumia chupa yako ya plastiki?
Kama huna hela ya kutumia au afya yako haikuruhusu kuwa hapo, kaa nyumbani kwak
o!