Vancomycin
Senior Member
- Jan 7, 2011
- 171
- 111
Wakuu
Mbunge wa Nyamagana Ezekia Dibogo Wenje,MB(CHADEMA) leo atakuwepo katika viwanja vya sahara kuanzia muda wa saa tisa alasiri akizungumza na wananchi.Pamoja na mambo mengine atatoa taarifa ya utekelezaji wa mambo kadhaa aliyotumwa na wananchi katika mikutano iliyopita
Shamra shamra zilianza tangu jana wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji hususani eneo la Bugarika ambapo walikuwa wakiimba wenje wenje mida ya jioni gari la matangazO lilipokuwa likipita wakionyesha furaha yao kwa matengenezo ya barabara yao iliyowatesa kwa kipindi kirefu
Wote mnakaribishwa
updates;
Mheshimiwa Wenje amezungumzia yafuatayo
(a)suala la shariff limezungumzwa ambapo amesema shariff wamegeuza usafi wa jiji dili ambapo watu wanakamatwa ovyo wakati sheria ziko wazi sharif hawaruhusiwi kuingia kwenye nyumba za watu,migahawa ya mama ntilie hivyo amepiga marufuku na kusema hiyo ni kazi ya bwana afya na ni kinyume na sheria hiyo ya usafi
(b)Migogoro ya viwanja limezungumzwa ambapo amesema kama walivyomtuma na amekubaliana na waziri husika atafika kushugulikia kero hizo
(b)Machinga,amewataka waheshimu makubaliano juu ya maeneo ya kuuzia yaliyotengwa na sio kuvamia kila eneo na kukanusha habari kuwa aliwachochea katika vurugu zilizotokea hivi karibuni wakati alikuwa kwenye kamati za bunge na kusema yeye hana rimoti pia amewataka wafanyabiashara wawe na vyombo vya kutunzia uchafu
(c)Elimu,amekerwa na kitendo cha kufungwa kwa shule ya msingi pamba kwa kukosa choo kisa wazazi hawajachanga na kufafanua sheria inayotabanaisha michango ni hiari na siyo lazima kama ambavyo watu wamekuwa wakilazimishwa na kunyang'anywa makochi
-ameelezea mfuko wa elimu ambao mpaka sasa una milioni arobaini ambapo amesema watachonga madawati kama ilivyokubaliwa
-azimio limewekwa shule ifunguliwe na choo kijengwe kufikia ijumaa ijayo vinginevyo nguvu ya umma itazungumza
(d)hali ya kisiasa,katika kujenga hoja yake ametolea mfano wa meli ya titanic meli kubwa ambayo nahodha wake alikuwa akitamba haitaweza kuzama wenzie walioshtuka walienda gorofa ya juu siku ambapo iligonga mwamba wa barafu na kuwa na uelekeo wa kuzama.Alisema hii ngoma inazama ingawa wengine wanapinga kama nahodha huku akibeza rostam kashtuka
aliendelea na kueleza CCM imechoka ukiona waziri anaandamana kumpinga waziri mwingine akasisitiza hii ngoma inazama
(e)Sukari,kufuatia malalamiko ya watu juu ya sukari wananchi walimtaka wafanye maandamano lakini waliafikiana afanye press conference kuhusu suala hilo na kutoa muda kwa serikali kupunguza bei hiyo isipotekelezwa nguvu ya umma itahusika
Jamani nimetumia simu kwa uchache ni hayo tu sikuwa na kamera hivyo wadau wengine wekeni picha mkutano ulijaa watu wengi sana ambapo baada ya kuhitimisha alibebwa juu na baadaye kusindikizwa na wananchi wengi