WENJE MB(CHADEMA) kunguruma LEO MWANZA

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
0
Wakuu

Mbunge wa Nyamagana Ezekia Dibogo Wenje,MB(CHADEMA) leo atakuwepo katika viwanja vya sahara kuanzia muda wa saa tisa alasiri akizungumza na wananchi.Pamoja na mambo mengine atatoa taarifa ya utekelezaji wa mambo kadhaa aliyotumwa na wananchi katika mikutano iliyopita

Shamra shamra zilianza tangu jana wananchi katika maeneo mbalimbali ya jiji hususani eneo la Bugarika ambapo walikuwa wakiimba wenje wenje mida ya jioni gari la matangazO lilipokuwa likipita wakionyesha furaha yao kwa matengenezo ya barabara yao iliyowatesa kwa kipindi kirefu

Wote mnakaribishwa

updates;

Mheshimiwa Wenje amezungumzia yafuatayo

(a)suala la shariff limezungumzwa ambapo amesema shariff wamegeuza usafi wa jiji dili ambapo watu wanakamatwa ovyo wakati sheria ziko wazi sharif hawaruhusiwi kuingia kwenye nyumba za watu,migahawa ya mama ntilie hivyo amepiga marufuku na kusema hiyo ni kazi ya bwana afya na ni kinyume na sheria hiyo ya usafi

(b)Migogoro ya viwanja limezungumzwa ambapo amesema kama walivyomtuma na amekubaliana na waziri husika atafika kushugulikia kero hizo

(b)Machinga,amewataka waheshimu makubaliano juu ya maeneo ya kuuzia yaliyotengwa na sio kuvamia kila eneo na kukanusha habari kuwa aliwachochea katika vurugu zilizotokea hivi karibuni wakati alikuwa kwenye kamati za bunge na kusema yeye hana rimoti pia amewataka wafanyabiashara wawe na vyombo vya kutunzia uchafu

(c)Elimu,amekerwa na kitendo cha kufungwa kwa shule ya msingi pamba kwa kukosa choo kisa wazazi hawajachanga na kufafanua sheria inayotabanaisha michango ni hiari na siyo lazima kama ambavyo watu wamekuwa wakilazimishwa na kunyang'anywa makochi
-ameelezea mfuko wa elimu ambao mpaka sasa una milioni arobaini ambapo amesema watachonga madawati kama ilivyokubaliwa
-azimio limewekwa shule ifunguliwe na choo kijengwe kufikia ijumaa ijayo vinginevyo nguvu ya umma itazungumza

(d)hali ya kisiasa,katika kujenga hoja yake ametolea mfano wa meli ya titanic meli kubwa ambayo nahodha wake alikuwa akitamba haitaweza kuzama wenzie walioshtuka walienda gorofa ya juu siku ambapo iligonga mwamba wa barafu na kuwa na uelekeo wa kuzama.Alisema hii ngoma inazama ingawa wengine wanapinga kama nahodha huku akibeza rostam kashtuka
aliendelea na kueleza CCM imechoka ukiona waziri anaandamana kumpinga waziri mwingine akasisitiza hii ngoma inazama

(e)Sukari,kufuatia malalamiko ya watu juu ya sukari wananchi walimtaka wafanye maandamano lakini waliafikiana afanye press conference kuhusu suala hilo na kutoa muda kwa serikali kupunguza bei hiyo isipotekelezwa nguvu ya umma itahusika

Jamani nimetumia simu kwa uchache ni hayo tu sikuwa na kamera hivyo wadau wengine wekeni picha mkutano ulijaa watu wengi sana ambapo baada ya kuhitimisha alibebwa juu na baadaye kusindikizwa na wananchi wengi

IMG00009-20110909-1822[1].jpg IMG00004-20110909-1821[1].jpg IMG00005-20110909-1822[1].jpg IMG00007-20110909-1822[1].jpg IMG00007-20110909-1822[1].jpg IMG00008-20110909-1822[1].jpg IMG00009-20110909-1822[1].jpg IMG00009-20110909-1822[1].jpg IMG00012-20110909-1823[1].jpg IMG00011-20110909-1823[1].jpg IMG00010-20110909-1822[1].jpg IMG00009-20110909-1822[1].jpg IMG00008-20110909-1822[1].jpg

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,142
2,000
Safi sana kamanda Wenje hiyo ndiyo maana ya mwakilishi wa wananchi lazima uwafahamishe namna ulivyowawakilisha ili nao wakwambie ufanye nini zaidi.

Honger HUU NI MWANZO MZURI TU.

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
0
Japokuwa hukuileta sawasawa hii habari lakini tunaomba uendelee kutujuza ili sisi tulioko Igunga tujue kinachoendelea huko kwenye Jiji la CHADEMA. Pamoja na masuala mengineyo usisahau kumkumbusha Mheshimiwa WENJE kufika huku Igunga amwage salamu kutoka kwa Makamanda wa Jiji la CHADEMA.

Jatelo

Member
May 17, 2011
42
0
nimekusoma mkubwa, i will b there, Mwanza ndo home kwao chadema tulishasahau ata kama kuna chama cha magamba.

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
2,000
Nzuri hiyo,,kuwa na utaratibu wa kuwapa mrejesho waliokuchagua juu ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali na pengine kuwapa way forward inafaa sana!

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
2,000
hii ndivyo inatakiwa kuwa karibu na wananchi kuwajuza na kuwaeleza yanayojili au yaliyotokea au nini kinatakiwa

oldonyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
549
225
Mwanza tulikosa wawakilishi takribani miaka 50 ya uhuru ila mungu katushushia mzazi jembe wenje.ngoja nikaoge nikamsikilize mwakilishi wa ukweli atakayekuwa tayali jama tutafutane katika viwanja.peoplezzzz.........

Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
1,225
Usisahau kutupa dondoo mkuu baadae yatakayosemwa na kamanda Wenje hapo bdae

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,411
2,000
Hongera sana kwa kitendo hicho kutoa feed back na kuwaeleza yaliyoazimiwa ya kitaifa na yatakayohusu jimbo lako na wana Mwanza kwa ujumla,Nakuomba usisahau kuwaelezea wingi wa ndio za wenzetu wa chama chetu chenye wenyewe juu ya mambo yasiyo na mashiko kwa taifa.kumbuka pia kuwafahamisha juu ya usingizi mtamu wa mawazili unaoitwa kutafakari

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
0
Mimi ni mdau mkubwa sana wa Jiji la Mwanza, naomba utuwekee hapa agreed action points ya vikao/mikutano
iliyopita na sisi tuchangie

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,708
2,000
Huyu Mkenya ana jipya watu wameishamchoka na porojo zake. Tena Machinga na kina Mama lishe hawataki hata kumuona.
Ndio maana huo mkutano unafanyika Bugarika, kwa wale ambao hawaijui Mwanza eneo la Bugarika wanakaa wageni kutoka Kenya, Mara, Tarime, Sirali, Nyamongo, huo ndio ukweli kwa mfano Dar es Salaam kila sehemu na watu wake, maeneo ya Kisutu mpaka Posta wakaa Wahindi, Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Wanakaa Wachagga

Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
7,310

acha uongo...

Mr.Professional

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,583
1,195
Huyu Mkenya ana jipya watu wameishamchoka na porojo zake. Tena Machinga na kina Mama lishe hawataki hata kumuona.
Ndio maana huo mkutano unafanyika Bugarika, kwa wale ambao hawaijui Mwanza eneo la Bugarika wanakaa wageni kutoka Kenya, Mara, Tarime, Sirali, Nyamongo, huo ndio ukweli kwa mfano Dar es Salaam kila sehemu na watu wake, maeneo ya Kisutu mpaka Posta wakaa Wahindi, Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Wanakaa WachaggaSio lazima kujua kila kitu na kukanusha hata yasiyotakiwa nani anataka kusikia jina la ccm mza? Ni ukweli usiopingika kuwa hata wale wachache waliokuwa na imani na ccm wamekimbia mza ya sasa ni kambi rasmi ya kuchukulia uongozi wa nchi kwa chadema japo sitashangaa kusikia kuwa chadema kimekuwa chama cha wasukuma au wakurya muda sio mrefu ila napo tutashinda.

Jemedari Wenje tafadhari endelea kudhihirisha kwa vitendo kuwa chadema ndio chama mbadala wa ccm. Jamani dondoo na picha ni muhimu kwa walioko mza kwa siku hii

mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,193
2,000
Wenje hana nyumba dar? Mbona wabunge wa magamba baada ya bunge wanatimkia dar?

Halfcaste

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
972
225
Huyu Mkenya ana jipya watu wameishamchoka na porojo zake. Tena Machinga na kina Mama lishe hawataki hata kumuona.
Ndio maana huo mkutano unafanyika Bugarika, kwa wale ambao hawaijui Mwanza eneo la Bugarika wanakaa wageni kutoka Kenya, Mara, Tarime, Sirali, Nyamongo, huo ndio ukweli kwa mfano Dar es Salaam kila sehemu na watu wake, maeneo ya Kisutu mpaka Posta wakaa Wahindi, Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Wanakaa Wachagga
Bwa!bwa!bwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
OH is Wenje a Kenyan??luv Kenyans,luv Wenje?We all Africans lets unite!!Mwanza pamoja,kama vp ntakuepo hapo Sahara

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
1,500
Wabunge kwao ni jimboni na si Bongo....Big up mheshimiwa..bungeni na mimi nitakuja najipanga...

oldonyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
549
225
Huyu Mkenya ana jipya watu wameishamchoka na porojo zake. Tena Machinga na kina Mama lishe hawataki hata kumuona.

Ndio maana huo mkutano unafanyika Bugarika, kwa wale ambao hawaijui Mwanza eneo la Bugarika wanakaa wageni kutoka Kenya, Mara, Tarime, Sirali, Nyamongo, huo ndio ukweli kwa mfano Dar es Salaam kila sehemu na watu wake, maeneo ya Kisutu mpaka Posta wakaa Wahindi, Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Wanakaa Wachagga

we bwawa wa magamba nae si lazima kila kitu uchangie ata ukipinga wenje anapendeka mwanza huo ndo ukweli.tuache na mwanza yetu,tuache na wenje wetu.

Kifimbocheza

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
494
225
Wenje Kakanue Mkuuu.

Washukuru wapiga Kura wako na endelea kutoa UOZO wa chama cha Magamba.

Toa sera Nzuri za Chadema

Pamojaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,525
2,000
Huyu Mkenya ana jipya watu wameishamchoka na porojo zake. Tena Machinga na kina Mama lishe hawataki hata kumuona.

Ndio maana huo mkutano unafanyika Bugarika, kwa wale ambao hawaijui Mwanza eneo la Bugarika wanakaa wageni kutoka Kenya, Mara, Tarime, Sirali, Nyamongo, huo ndio ukweli kwa mfano Dar es Salaam kila sehemu na watu wake, maeneo ya Kisutu mpaka Posta wakaa Wahindi, Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Wanakaa Wachagga

Hata mimi naona hana jipya,mwenye jipya ni yule anaepelekwa na waarabu kununuliwa suti na boksa,au we unaonaje yakhe?

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom