Wenje katika kashfa ya kutotimiza ahadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenje katika kashfa ya kutotimiza ahadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Oct 24, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje ametuhumiwa kushindwa kutimiza ahadi ya kulipia wanafunzi 130 wa sekondari ada.

  Wakitoa malalamiko yao wakuu wa shule walisema Mh Wenje aliahidi kusomesha wanafunzi hao lakini toka Januari mwaka jana hajalipa ada kwa wanafunzi hao. Ada hiyo imefikia Tsh mil 18.

  Source: Gazeti la Baruti.

  Maoni yangu.
  Mheshimiwa Wenje hizi zinaweza kuwa propaganda za kukuchafua, lakini kama ni kweli, hii itakuwa draw-back kubwa kwa chama makini kama chadema.

  Nilitegemea Muwe wa kwanza kutimiza ahadi tena bila kuhimizwa, lakini kama na nyinyi mnashindwa kutimiza ahadi mlizozitoa bila wenyewe basi hatuna pa kukimbilia. Tutamwamini nani, hata vyama vya upinzani vinatugeukia.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  kuna dalili za uongo, yaani watoto hawajalipiwa ada miaka miwili, nani kakwambia kuna utaratibu wa kulimbikiza ada hata kwa nusu muhula, mtawadanganya wasiosomesha kwa sasa. ccm inaharibu ufahamu wa watanzania.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Inawezekana mkuu, ndio maana nikasema inaweza ikawa habari ya kumchafua
   
 4. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nafikiri ili kuingia form one au kuanza mwaka mpya LAZIMA uwe umelipa kiasi fulani cha ada.Sasa hao walimu au mwalim mkuu alikuwa wapi.Sidhani
   
 5. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tusubiri taarifa Kamili,Wenye akanushe au athibitishe uwepo wa deni hilo!
   
 6. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280

  Source: Gazeti la Baruti.

  hapo ndo napata wasiwasi, Mbunge wangu hayupo hivyo.
   
 7. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...dah!...Chagulan umerudi tena?...
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mtoa mada fafanua ada ya shule ambazo aliahidi kuwasomesha ni shilingi ngapi???? Watoto 130 miaka miwili ada 18ml!!!!
   
 9. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaomba kama mh. Wenje yupo humu azungumzie hilo, vinginevyo unaweza ukawa mwanzo mbaya!
   
 10. Super H

  Super H JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 1,004
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii hujuma inafanywa na mkurugenzi wa jiji la mwanza kuna habari nilishasikia Wenje akimlalamikia kuwa amekataa kuidhinisha check ya nmb ya hizo ada.tusubirie majibu ya wenje ukweli utajulikana.
  Mimi lawama zangu kwa Wenje tulichanga pesa pale viwanja vya sahara kwa ajili ya madawati na sijawahi sikia pesa zilipoenda
   
 11. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red,

  Kimahesabu ya haraka-haraka mambo yako hivi:-
  Tzs. 18,000,000 / wanafunzi 130 / miaka miwili = Ada ya mwanafunzi mmoja (kwa wastani) ni Tzs. 69,230.77 kwa mwaka !!
  Hapo sidhani kama ni ada za shule za sekondari.
   
 12. r

  raymg JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jk katimiza ahadi gani?....
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Jambo limezua jambo!
   
 14. n

  nyangasese Senior Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili gazeti lina takriban mwezi mmoja na nusu tangu lianzishwe.Ukifuatilia matoleo yake ya kwanza utaona kuwa mengi yanazungumzia habari za kumchafua wenje.kila mara linapotoka linakuwa na habari za wenje.Anayejiita mmiliki wa gazeti hili ni mfanyakazi ktk kampuni ya Diallo.Huenda huu ni mkakati wa 2015 kulirudisha jimbo ccm maana bosi wake sasa ndio mwenyekiti wa ccm mkoa Mwanza
   
 15. n

  nyangasese Senior Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  suala la madawati alishawahi kujibu redioni kuwa kila mara ana utaratibu wa kugawa madawati kila mwisho wa mwaka,na mwaka huu atafanya hivyo mbele ya wananchi kwa pesa zilizochangwa
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Ni utoto kuto jua maana ya kashfa!

  Hichi nacho nimoja ya kiwanda alicho sema jk
   
 17. n

  nyangasese Senior Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi lawama zangu kwa Wenje tulichanga pesa pale viwanja vya sahara kwa ajili ya madawati na sijawahi sikia pesa zilipoenda[/QUOTE]
  Acheni uzushi mh mbunge alishatoa ufafanuzi kuwa wengi wa waliotoa ahadi hawajatimiza ahadi zao.Tungoje huo mwisho wa mwaka ambao ni utaratibu wake wa kugawa madawati mara kwa mara kama akishindwa ndio tumhukumu
   
 18. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ikiwa ni Kashfa basi rais JK anaongoza.
   
 19. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutasikia mengi lakini ukweli utajulikana tu!
   
 20. Super H

  Super H JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 1,004
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
   
Loading...