Wenje katika kashfa ya kutotimiza ahadi

Wenje katika kashfa ya kutotimiza ahadi

Nani Mwanasiasa Mkweli Tanzania.wote ni sawa sawa hawana ahadi hata moja watakayoitekeleza
 
Sina imani kabisa na Wenje toka alivyokula michango ya madawati. Mbunge makini hawezi kushindwa kulipa ada...ngoja muda wake upite wana Mwanza wachague mbunge makini.
 
Tunaomba kama mh. Wenje yupo humu azungumzie hilo, vinginevyo unaweza ukawa mwanzo mbaya!

Nani asiyejua kuwa somo la mathematics kwa watanzania ni tatizo?
Kama shule za kata wanachangia Tshs. 20,000 kwa mwaka, wanafunzi 130 kwa miaka mitatu inabidi wadaiwe Tshs. 7,800,000/=.
Mtoa mada ni kilaza mkubwa na wala hawezi kuwa Chagulani kwa kuwa Chagulani namfahamu kuwa anajua hesabu vizuri na anaendelea na kazi zake za udiwani kama kawaida.
Tusipende kupotoshana hapa! Msimsumbue mbunge wangu kujibu utumbo wa hivi!
 
Sina imani kabisa na Wenje toka alivyokula michango ya madawati. Mbunge makini hawezi kushindwa kulipa ada...ngoja muda wake upite wana Mwanza wachague mbunge makini.
Mbunge sio Mweka hazina; mbona unatuletea habari za vijiwe vya kahawa! Au uko pale kemondo kijiwe cha uongo wa kisiasa nini?
Kama unataka real data nenda ofisi ya mbunge pale Nyamagana (karibu na ofisi za mkuu wa wilaya) utapata data zote kama zilivyo kwa usahihi.
 
suala la madawati alishawahi kujibu redioni kuwa kila mara ana utaratibu wa kugawa madawati kila mwisho wa mwaka,na mwaka huu atafanya hivyo mbele ya wananchi kwa pesa zilizochangwa[/QUOTE mkuu zilipatikana 70ml + anakaa nazo mwaka mzima ndio agawe madawati au anazizungushia mahali na kula riba,pili VIC FISH waliahidi kuchonga 40% zaidi ya tulizochanga wananchi.

Acha uongo,ahadi na michango hazikufika mil 70 mimi mwenyewe nilikuwepo sahara siku hiyo
 
Mbunge sio Mweka hazina; mbona unatuletea habari za vijiwe vya kahawa! Au uko pale kemondo kijiwe cha uongo wa kisiasa nini?
Kama unataka real data nenda ofisi ya mbunge pale Nyamagana (karibu na ofisi za mkuu wa wilaya) utapata data zote kama zilivyo kwa usahihi.

Sasa hao mnaowalalamikia kwa ufisadi ni waweka hazina? Mwezi uliyopita nilikuwa Mwanza nimetembea maeneo mbalimbali Igoma, Nyakato, Mabatini, Isamilo, Mirongo, kwa kweli watu wanalalamika sana kuhusu Wenje hana msaada wowote kwa wananchi kiufupi wamemchoka.
 
unaweza kutuwekea picha mkuu?
 
Sasa hao mnaowalalamikia kwa ufisadi ni waweka hazina? Mwezi uliyopita nilikuwa Mwanza nimetembea maeneo mbalimbali Igoma, Nyakato, Mabatini, Isamilo, Mirongo, kwa kweli watu wanalalamika sana kuhusu Wenje hana msaada wowote kwa wananchi kiufupi wamemchoka.

Wanaolalamika hawajui mipaka ya kazi ya Mbunge. Ndo maana yeye kila siku analia na Mkurugenzi wa Jiji; balaza la madiwani linaweza kupitisha azimio fulani lakini Mkurugenzi kwa mamlaka aliyopewa na aliyemteua akatengua, ndo hapo Mhe. Wenje anawahamasisha wananchi waandamane kumpinga Mkurugenzi wa jiji ambaye ndo muidhinishaji wa mambo yote ya kifedha.
 
Mimi ni mzaliwa na mkazi wa mwanza naishi maeneo ya k/bwiru kwa hili Jamani muitendee haki chadema katika jiji la mwanza kwani kuna miradi mingi imetekelezwa ikiwa chini yao kuna soko kubwa la africa mashariki ujenzi unaendelea maeneo ya kirumba,barabara kiwango cha lami kutoka buzuruga,kiloleli,nyasaka,pasiansi,k/hewa hadi k/bwiru mradi unaendelea nyanza road yuko site na kesha anza kumwaga lamiKuna daraja kubwa linajengwa mabatini yaani mabatini fly over inayofanana na lile ya mazense kandarasi imekwisha tangazwa,barabara nyingi za mjini zinawekewa lami ikiwemo karuta ,libert,malaika beach kwenda airport,mkuyuni jct to butimba kiwango cha lami mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege unaendelea yote haya yanafanyika yakiwa chini ya uongozi wa chadema
 
suala la madawati alishawahi kujibu redioni kuwa kila mara ana utaratibu wa kugawa madawati kila mwisho wa mwaka,na mwaka huu atafanya hivyo mbele ya wananchi kwa pesa zilizochangwa
Kama tayari wananchi wameshachanga hela ni kwa nini ichukue mwaka mzima kuwakabidhi madawati yao. Halafu kwa nini kama ni michango ya wananchi Mbunge ndiye aamue ni lini fedha hizo zitumike?
 
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika nilizozipata kutoka kwa Mh. Wenje mwenyewe ni kwamba, ni kweli kwamba alitoa ahadi ya kusaidia kuwalipia ada watoto ambao wazazi wao walikuwa hawana uwezo kabisa kwenye shule mbali mbali katika Jiji la Mwanza, kupitia mfuko wa maendeleo wa jimbo (CDCF) ambao wajumbe wake ni diwani mmoja wa ccm(kata ya buhongwa),diwani mmoja CDM(viti maalum),watendaji wawili wa kata wanaoteuliwa na mkurugenzi wa halmashauri na katibu wa kamati hiyo ni mchumi wa jiji la Mwanza.Hizo pesa serikali inatuma moja kwa moja kwenye account za halmashauri na wala mbunge hazioni.Kamati ya CDF ambayo mbunge ndo mwenyekiti wake ilishaidhinisha malipo ya hizo pesa kwenda kwenye shule mbalimbali toka mwaka jana mwezi wa nne, halmashauri ya jiji ambayo imejaza makada wa CCM ambao wao kazi yao ni ku-sabotage wamekataa kupeleka hizo pesa kwenye shule hizo hadi leo huku wakitoa visingizio mbalimbali kila kukicha,na ndoo maana hivi karibuni alifanya mkutano wa hadhara kwenye shule ya mbugani na alieleza wananchi kwa masikitiko jinsi gani mchumi wa jiji bwana Patrick Karangwa anatumiwa kudhoofisha jitahada hizo za kusaidia watoto ambao wanatoka kwenye mazingira magumu kiuchumi. Nilipo muuliza Mh. Wenje kuhusu way forward akaniambia kikao kijacho cha CDCF ndo wajumbe wataamua hatua za kinidhamu za kuchukua dhidi ya katibu wa kamati.
 
Sasa hao mnaowalalamikia kwa ufisadi ni waweka hazina? Mwezi uliyopita nilikuwa Mwanza nimetembea maeneo mbalimbali Igoma, Nyakato, Mabatini, Isamilo, Mirongo, kwa kweli watu wanalalamika sana kuhusu Wenje hana msaada wowote kwa wananchi kiufupi wamemchoka.

Huna haja ya kutusemea wana Mwanza.labda wewe ndio umemchoka.Tunaojua kama hana msaada kwetu ni sisi wenyewe wana mwanza tutahukumu na hatutangoja Ritz atusemee.Kwa taafa ni kuwa 2015 ccm isahau kabisa nyamagana hata kama Wenje hatasimama kutetea jimbo
 
Kama tayari wananchi wameshachanga hela ni kwa nini ichukue mwaka mzima kuwakabidhi madawati yao. Halafu kwa nini kama ni michango ya wananchi Mbunge ndiye aamue ni lini fedha hizo zitumike?
watu walioahidi b ado hawajakamilisha Michango yao akiwemo mbunge wa Rorya (ccm) na wengineo.
 
Acha uongo,ahadi na michango hazikufika mil 70 mimi mwenyewe nilikuwepo sahara siku hiyo
muongo ni wewe na wenje ungetuandikia basi ahadi ilifika ngapi na cash ngapi na ni shule gani zimepata madawati mangapi,usifanye watu wooote ni wajinga.tufike mahali tuache kutetea ujinga na tusipokuwa makini Dialo anakuja kwa kasi.....
 
Source- Gazeti la Baruti??????????????????????
 
kuna dalili za uongo, yaani
watoto hawajalipiwa ada miaka miwili, nani kakwambia kuna utaratibu wa
kulimbikiza ada hata kwa nusu muhula, mtawadanganya wasiosomesha kwa
sasa. ccm inaharibu ufahamu wa watanzania.

kamanda kunawanafunzi wamemaliza senior 4 mwaka huu na wanadaiwa toka 2010:
 
Back
Top Bottom