Elections 2010 Wenje achangiwa samani za Ofisi....Zitto apuuza mpasuko.....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Gazeti la Majira la leo linatuhabarisha ya kuwa Mbunge wa Nyamagana Mheshimiwa Wenje amechangiwa samani za ofisi ambazo mbunge wa zamani Masha aliziondoa...........

Na wakati huohuo Zitto amekanusha madai ya kuwepo kwa mpasuko ndani ya Chadema..........

Wakati huohuo gazeti la Uhuru limeendelea na kampeni yake ya kuichafua chadema kama ilivyokuwa ikifanya wakati wa zile enzi za NCCR-MAGEUZI pale walipodai ya kuwa ........Mbunge wa Chadema Mheshimiwa Wenje ahamasisha vurugu na ya kuwa ataka machinga waharibu mali za jiji......................kisa ni kama Chadema haitanyakuwa nafasi ya umeya wa jiji hilo..................

Mbunge ahamasisha machinga kuchoma mali za halmashauri

Wednesday, 08 December 2010 07:55 newsroom




* Pia, ataka viwanda, hoteli za wana-CCM zichomwe
* Ni iwapo CHADEMA itashindwa kiti cha umeya wa Jiji
NA PETER KATULANDA, MWANZA
MBUNGE wa Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekia Wenje, anadaiwa kuanza siasa chafu kwa kuhamasisha wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wachome mali za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kama chama hicho hakitatwaa kiti cha umeya. Wenje pia anadaiwa kuwahamasisha wafuasi wa CHADEMA kuchoma viwanda na hoteli za baadhi ya matajiri ambao ni wanachama wa CCM kama watakikosa kiti hicho. Alitoa maelekezo hayo juzi saa 11.00 jioni, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sahara kata ya Pamba, wilayani Nyamagana. Akizungumza kwenye umati uliojitokeza kumsikiliza, alisema wananchi wasikubali maeneo yao yapimwe na maofisa ardhi wa jiji watakaokwenda kupima kwa lengo la kuwalipa fidia ili wauze viwanja hivyo, wachome moto magari yao .
ìTunasikia maofisa wa Jiji wanataka kuja kupima viwanja katika baadhi ya maeneo kwa lengo la kuwaondoa na kuwauzia matajiri, msikubaliane nao na waambieni waondoke, wakiwabishia basi mchome magari yao kuonyesha kuwa hamkubaliani nao kupora ardhi yenu,î alisema. Alidai kwamba baadhi ya wana-CCM wanawashawishi madiwani wa CHADEMA wamchague Meya wa Jiji kutoka CCM, hivyo wananchi wasikubaliane na matokeo yatakayotangazwa Desemba 17, mwaka huu, iwapo Meya hatatoka CHADEMA. ìTumewaeleza madiwani wetu kuwa siku hiyo tutapiga kura za wazi kumchagua Meya wa Jiji la Mwanza, atakayetusaliti tunaanza naye kisha tunawafuata matajiri wa CCM na kutatahakikisha mali zao tunaziharibu au kuzichoma ili wajue hatuko tayari kuibiwa,î alisisitiza Wenje.
Aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo waendelee kufanya biashara zao popote bila kubugudhiwa na mgambo wa jiji. Wenje pia alikaririwa akiwaonya walimu wa sekondari na shule za msingi kutowatoza wanafunzi michango yoyote, huku akisema anamshukuru mfanyabiashara mmoja mzalendo kutoka Dar es Salaam kwa alichodai kumsaidia kuwa mbunge. Kutokana na kauli hizo, baadhi ya wananchi akiwemo Jumanne Magembe na wengine ambao hawakutaka kutajwa majina yao waliponda kauli za Mbunge huyo na kudai kwamba ni uchochezi wa kisiasa ambao utasababisha uvunjifu wa amani hapa. ìHuu ni uchochezi na siasa chafu, Wenje amezungumza maneno ya uchochezi anapaswa kukemewa na mamlaka husika kabla mambo hayajawa kama Kenya na kusababisha machafuko kwa manufaa ya wanasiasa wasiokuwa na uchungu na damu ya Watanzania,î alisema Magembe. ìNyie waandishi, hayo ndiyo maneno ya kuja kuwaeleza wananchi kama si kuleta uchochezi?" alihoji mkazi mwingine na kuongeza: "Hii ni hatari kwa wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa, jiji lina sheria zake na pia kila jambo lina utaratibu wake wa kisheria."



Zitto: Sihami, sifukuzwi Chadema Tuesday, 07 December 2010 20:49 0diggsdigg

kabwe%20zitto.jpg
Joyce Mmasi
"SIWEZI kuhama Chadema na siwezi kufukuzwa kwa kuwa hakuna kosa lolote la ajabu ambalo nimelifanya na ambalo adhabu yake ni kufukuzwa katika chama. Lakini pia siwezi kuhama kwa kuwa hiki ndicho chama pekee ninachoamini kuwa kitawavusha Watanzania na kuwaletea mabadiliko na maendeleo wanayoyataka," hiyo ni kauli ya Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mwanasiasa huyo kijana alisema hayo nilipomwuliza kama anakusudia kukihama chama hicho endapo tuhuma zinazomkabili za kukiuka maamuzi ya uongozi zitamgharimu kufukuzwa au mwenyewe kulazimika kujiondoa.

Anasisitiza kuwa Chadema ndicho chama pekee anachokusudia kukitetea na kukilinda na hata mipango yake ya kugombea urais ataitekeleza akiwa ndani ya chama hicho kikubwa cha upinzani na si katika chama kingine chochote cha siasa.

"Nasema kwa dhati kabisa sitarajii kuhama Chadema, nihamie chama gani… siwezi, hata urais Mungu akipenda nitagombea nikiwa ndani ya chama hiki," anasema Zitto kwa huku akionyesha kuamini kile anachokisema.

Miezi miwili iliyopita, Zitto alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa anatarajia kugombea urais ifikapo mwaka 2015. Aliwaambia wafuasi wa chama hicho kuwa mwaka huo ukifika atarudi mkoani Kigoma akiwa mgombea urais na akaomba wananchi waliohudhuria mkutano huo kumuunga mkono.

Hata hivyo, Zitto anasema hasumbuliwi na kauli za baadhi ya watu anaowaita wasiokitakia mema chama hicho ambao wamekuwa wakimpachika majina lukuki kama vile pandikizi, kigeugeu na mengineyo na badala yake anasema mikakati yake ya sasa ni kuwatumikia wananchi wa jimbo lake waliompa heshima na kumrudisha bungeni kwa ushindi wa kishindo.

"Watu wa Kigoma kwa sasa wanataka kusikia nina mikakati gani kutekeleza ahadi zote nilizowaahidi, hawapendi kusikia Zitto akilumbana na watu, ndiyo maana unaona sasa nipo kimya nikijiandaa kuanza kutekeleza ahadi zangu zote nilizoahidi wakati wa kampeni," anasema.

Je, ni mikakati gani aliyoipanga katika kipindi cha miaka mitano ijayo katika kutumikia wakati wa jimbo lake? Zitto anasema:"Kikubwa nitakachoanza nacho ni kuhakikisha vijiji vyote 32 vya jimbo langu vinapata umeme, tayari tumeanza katika vijiji vitatu, vya Mwandiga, Msimba na Mahembe. Lengo langu ni kufikisha umeme vijijini 20 ifikapo mwaka 2015, umeme vijijini ni agenda namba moja kwangu."

Anasema kitu kingine anachokusudia kufanya katika kipindi cha miaka mitano ni kuboresha kilimo cha michikichi ili kuongeza uzalishaji wa zao la mawese.

"Watu wa Kigoma Kaskazini tunataka kuonyesha namna gani fikra, muono na mikakati mbadala inavyoweza kuondoa umasikini wa wananchi. Kama Malaysia wameweza kuondoa umaskini kutoka asilimia 55 mwaka 1970 mpaka asilimia tatu mwaka 1990, ni dhahiri Tanzania inaweza na Kigoma inaweza zaidi" anasema.

"Ili kumkomboa mkulima wa mawese, nakusudia kuanzisha viwanda vidodo vidogo vya kusindika. Tunataka kufanya Kijiji cha Mahembe kuwa ni eneo la viwanda vidogovidogo vya kusindika mawese na mazao ya maweze, ndiyo maana tumeanza kupeleka umeme eneo lile kwanza. Nia ni mafuta ya mawese yazalishwe kwa ubora na kuweza kupata soko la uhakika la bidhaa hiyo."

Anasema tayari amefanya mazungumzo na wawekezaji nchini Malaysia ambao watawekeza katika viwanda vya kuzalisha zao hilo mkoani huko.

Mbali ya mawese, Zitto anasema Mkoa wa Kigoma pia unazalisha kahawa zao ambalo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita aliwezesha wakulima wake kupata soko la uhakika katika makampuni ya watu wa Marekani ambako wanauza kwa bei nzuri tofauti na ilivyokuwa awali.

Anakusudia pia kuitumia Hifadhi ya Gombe ili wakazi wa jimbo lake waweze kunufaika na hifadhi hiyo pekee iliyopo jimboni mwake.

Je, wakazi wa eneo hilo watanufaikaje na Hifadhi hiyo ya Taifa ya Gombe, Zitto anasema: "Tunataka watalii wanaokuja Gombe, wasiende kulala mbugani. Tunataka walale katika Vijiji vya Gombe na Mwamgongo vinavyozunguka mbuga hiyo. Tunachokusudia kufanya ni kuhamasisha wananchi wajenge hoteli zenye usalama, safi na za gharama nafuu vijijini ili watalii wakae na wanavijiji, watumie pesa zao kijijini na vijana wa maeneo yale wapate ajira ya kuwaingiza hifadhini. Hii itaongeza ajira na kusaidia kupunguza umaskini na wakati huohuo, wananchi wa maeneo hayo watafaidika."

Kwa upande wa elimu anasema baada ya kufanikiwa katika ujenzi wa shule za sekondari katika kila kata, sasa anakabiliwa na changamoto ya kupeleka walimu. Anaamini baada ya kufanikiwa katika ujenzi wa miundombinu jimboni idadi ya walimu katika shule hizo itaongezeka.

"Awali walimu walikwepa kwenda kufundisha katika shule za jimboni kutokana na ubovu wa barabara na maeneo mengine kukosa umeme, sasa hivi barabara zote zimejengwa nyingine kwa kiwango cha lami, zote zinapitika wakati wote hivyo naamini tatizo la walimu litapungua au kumalizika kabisa," anasema.

Akizungumzia suala la afya, Zitto anasema, mpango wa serikali ni ujenzi wa zahanati katika kila kijiji na ujenzi wa kituo cha afya kwa kila kata. "Kwa sasa tumejenga vituo vya afya katika kata tatu, mkakati ni kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya kwa kata zilizosalia" anasema.


Mgogoro Chadema: Lissu, Zitto lugha moja
Tuesday, 07 December 2010 20:41 0diggsdigg

Joyce Mmasi

BAADA ya ushindi wa kihistoria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, furaha nderemo, vifijo na mikakati zaidi ya kujiimarisha kisiasa, ndivyo vilivyokuwa vinategemewa hasa kutoka katika vinywa vya viongozi na wale wote waliokuwa makamanda wakati wa kampeni.

Lakini hali haikuwa hivyo machoni mwa wengi. Wiki kama mbili hivi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo chama hicho kilitoa msimamo wa kususia na kutoka nje ya Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba ya kulizindua. Dhahiri walitimiza ahadi yao iliyokuwa na ujumbe mahsusi kwa Rais Kikwete wa kutorishishwa na mchakato wa uchaguzi wa Rais wakitaka pia kuwepo kwa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Lakini siyo wabunge wote wa Chadema waliotii wito huo wa chama. Baada ya hatua hiyo iliyoibua hisia na kauli tofauti kutoka kwa wanasiasa na hata wananchi wa kawaida, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe aliitishwa mkutano wa waandishi wa habari akisema kwamba alikataa kushiriki mgomo huo na kutoa sababu mbalimbali huku akitoa siri ya jinsi walivyokuwa wamefikia uamuzi huo. Yeye na baadhi ya wenzake walimua kutofika kabisa bungeni siku hiyo.

Siku chache baada ya kitendo hicho, Chadema kupitia kwa Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kilitangaza kuwa kimewaandikia barua wabunge wake 10, akiwemo Zitto kikitaka kujua sababu za kutotii maamuzi ya chama juu ya msimamo wake wakati wa uzinduzi wa bunge hilo la 10.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake, Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete hivyo asingeweza kutoka kwa kuwa wapiga kura wake wasingemwelewa.

Alisema kwamba uamuzi wa kususia hotuba hiyo ya uzinduzi ulifikiwa baada ya kupigwa kwa kura za siri, yeye na wenzake hao walishindwa lakini walikataa kukubaliana na uamuzi huo hivyo kuamua kutofika kabisa bungeni.

Kwa macho ya wengi, huo unaonekana kuwa ni mgogoro kama ule uliokikumba chama hicho mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mkutano wake mkuu ambao matokeo yake yalikuwa ni kujivua uanachama kwa David Kafulila na Felix Mkosamali ambao walijiunga na NCCR-Mageuzi na sasa ni wabunge wakitokea Kigoma.

Lakini licha ya kuonekana hivyo, Lissu na Zitto katika hili wanazungumza lugha moja, inayofanana kwa kila uzito. Kwa sauti pana kabisa wanasema hakuna mgogoro hata chembe ndani ya chama chao!

Lissu anasema kilichofanywa na chama chake ni taratibu za kinidhamu tu kusisitiza kwamba hilo lisitafsiriwe kama mgogoro au mgongano wa aina yoyote.

Wote wawili kwa nyakati tofauti wanawanyooshea kidole wanaosema kwamba kuna migogoro ndani ya chama wakisema ni wale wanaokitakia mabaya na ambao wamekuwa wakikesha kukiundia migogoro ili kisambaratike.

Lissu anasema hakuna mpasuko, mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliopo.

Anasema wapo watu ambao wamekuwa wakikiombea chama hicho kivunjike miaka mingi iliyopita, lakini anasema kelele hizo za kukisema vibaya ndizo zinazokiimarisha na kukifanya kiendelee kuwa imara kisichotetereka

"Chadema kimeombewa vurugu miaka nenda rudi, tumeitwa majina ya kila aina, mara chama cha Wachaga, tukaitwa chama cha Wakatoliki, sasa msishangae wakasema chama cha Wanyaturu, lakini ukweli ni kuwa Chadema ni imara na isiyotetereka," anasema Lissu.

Kwa upande wake, Zitto anasema taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja. Anasema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya Chadema na wengine kufikia hatua ya kusema uongo, kwa nia ya kuleta chokochoko... "Hao wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu."

"Katika siasa hamuwezi kuwaza mamoja, yapo maeneo mnatofautiana na hili ni jambo la kawaida kabisa. Huwezi kusimama na kudai kuwa huo ni mgogoro. Kuhusu kutofautiana na wenzangu wakati Rais akihutubia kutashughulikiwa katika taratibu za kinidhamu zilizopo ndani ya chama na wakosaji wataadhibiwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama, lakini huwezi kusema au kuuita huo ni mgogoro."

Zitto anasema wakati umefika kwa Watanzania kuwa na tabia ya kujenga na si kubomoa kama ilivyo sasa, jambo dogo linakuzwa hali aliyosema inaweza kusababisha watu wakasahau kutekeleza ahadi katika majimbo yao na kuanza kulumbana kwenye vyombo vya habari.
 
.....eeeh, gazeti la UHURU bado lipo? juzi nilijaribu kuliulizia hapa Tanga Bus Stand...amini usiamini..kati ya Newspaper Vendors watano niliowauliza, watatu walisema hawauzi gazeti la UHURU maana haliuziki linadoda! Kasheshe, ulizia mauzo ya Mwananchi, Raia Mwema, MwanaHalisi...yako juu saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana!!

UHURU=go to hell! Bahati yao wanapata ruzuku toka chamani otherwise ingekuwa ishekufa!
 
Dua la kuku kamwe halimpati mwewe,waache waiombee mabaya chadema lakini itavuka tu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom