Wengine wametajwa, wengine wamefanywa siri, haki na usawa viko wapi hapa?

Wengine wametajwa, wengine wamefanywa siri, haki na usawa viko wapi hapa?

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,986
Reaction score
30,180
Wadau,

Leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amekabidhi file lenye majina 97 ya Watanzania wanaodhaniwa kua ni wanajihusishs na Madawa ya Kulevya katika kile alichokiita awamu ya 3. Mh. Makonda amegoma kuwataja hadharani kwa kile alichosema kua awamu mbili zilizopita alizisimamia yeye ndio maana aliwataja kwa kua ni style yake ila kwa sasa anakabidhi kijiti kwa Kamishna wa Tume ambae nae ataangalia style yake ni ipi.

Hapa napata na ukakasi kidogo kuelewa sababu inakuaje kwenye jambo hilohilo moja wengine walitajwa hadharani na wengine waefanywa siri. Nimejiuliza maswali mengi sana kwenye hili swala bila majibu. Kwani wale aliowataja kwenye awamu mbili za mwanzo hawatoshughulikiwa na Kamishna Sianga?? Kwanini na hawa asiwataje tu ikiwa ajina yote yatashughulikiwa na huyu Kamishna?? Au kwenye Haya ajina mapya kuna watu ambao wakijulikana hadharani itakua tabu kwake?

Nachojua kila awamu/phase ilivyokua ikitajwa ndio ukubwa wa majina ulikua ukiongezeka. Kwaba waliotajwa awau ya pili ni wakubwa zaidi kuliko awamu ya Kwanza. Na yeye Makonda alituaminisha kua awamu ya tatau itakua na Majina makubwa zaidi kuliko awamu yote. Mbona kama hawa ndio wa hatari zaidi ambao ilifaa jamii iwajue ili kujiepusha nao?

Je wale waliotajwa mwanzo wakilalamika kua wameonewa sababu hawakushughulikiwa kama hawa 97 wa awamu ya tatu si watakua na haki?
Iweje watuhumiwa wa makosa hayo hayo washughulikiwe tofauti?

Au kuna alieelewa hapa sababu za kueleweka za haya majina kutotajwa hadharani?
 
Angenitolea photocopy hayo majina..... Tuna mambo mengi ya kufanya ili kujiletea kipato. Kama hawezi akafie mbali, Mungu hadhihakiwi!...akina Mungu wapo wengi watamdhuru
 
Wadau,

Leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amekabidhi file lenye majina 97 ya Watanzania wanaodhaniwa kua ni wanajihusishs na Madawa ya Kulevya katika kile alichokiita awamu ya 3. Mh. Makonda amegoma kuwataja hadharani kwa kile alichosema kua awamu mbili zilizopita alizisimamia yeye ndio maana aliwataja kwa kua ni style yake ila kwa sasa anakabidhi kijiti kwa Kamishna wa Tume ambae nae ataangalia style yake ni ipi.

Hapa napata na ukakasi kidogo kuelewa sababu inakuaje kwenye jabo hilohilo moja wengine walitajwa hadharani na wengine waefanywa siri. Nimejiuliza maswali mengi sana kwenye hili swala bila majibu. Kwani wale aliowataja kwenye awamu mbili za mwanzo hawatoshughulikiwa na Kamishna Sianga?? Kwanini na hawa asiwataje tu ikiwa ajina yote yatashughulikiwa na huyu Kamishna?? Au kwenye Haya ajina mapya kuna watu ambao wakijulikana hadharani itakua tabu kwake??

Nachojua kila awamu/phase ilivyokua ikitajwa ndio ukubwa wa majina ulikua ukiongezeka. Kwaba waliotajwa awau ya pili ni wakubwa zaidi kuliko awamu ya Kwanza. Na yeye Makonda alituaminisha kua awamu ya tatau itakua na Majina makubwa zaidi kuliko awamu yote. Mbona kama hawa ndio wa hatari zaidi ambao ilifaa jamii iwajue ili kujiepusha nao??

Je wale waliotajwa mwanzo wakilalamika kua wameonewa sababu hawakushughulikiwa kama hawa 97 wa awamu ya tatu si watakua na haki?? Iweje watuhumiwa wa makosa hayo hayo washughulikiwe tofauti??

Au kuna alieelewa hapa sababu za kueleweka za haya majina kutotajwa hadharani??
Jibuu nii kwamba taaluma itatumika kuwashugulikia, mwanzoni ilikua mihemuko. sasa wenye taaluma yao wameingia. pia maoni ya wananzuoni na wananchi yamefanyiwa kazi. watu walilalamika kwa nn walitajwa adharani? Serekali imesikia kilio chao na sasa watashughulikiwa kwa kwa kutumiaa taaluma. Kama niya yako nikuwafaaham, subiri utawajua tu siwatafikishwa mahakamani.
 
hapa leo HOJA kuu ni jinsi WAPINZANI walivyo badilisha GIA tena ANGANI...KIVIPI....

Leo MAKONDA hajataza majina WAMEANZA kubwa bwaja .....Ooooh mbna leo hajataja MAJINA.....

Hivi mnataka nini hasa.....Mkitajiwa MAJINA shida....MSIPO TAJIWA NA penyewe shida.....

Tuna safari ndefu sana kwenye nchi hii.........
 
Ambacho hujaelewa hapo mkuu ni kipi hasa!? Walipotajwa watu tulilalamika kwamba hajatenda haki, sasa hivi amejirekebisha tunataka ataje tena, Sio nzur hivyo. Cha msingi tusubiri outcomes za vita hii ndo tuone kama alienda sawa ama si sawa
 
Nimesikia kamtaja kijana mmoja hadharani sijui kisa anauhakika hajui siasa kwahyo hatoweza kugoma kufika centre ...
 
  • Thanks
Reactions: 365
acha kuimba taarabu wewe hii vita ni yetu sote makonda anapaswa apongweze kwa nini mnakua hamkosi visababu kwa kila juhudi zinavyofanywa
Apongezwe labda na ''wauzaji'' maana aliwaita jumatatu kuwa waje ijumaa hivyo aliwapa muda wa kuficha ushahidi na mwisho wa siku wakasearch nyumba na ofisi zao wakakuta hamna kitu je tumepata nini??? ndio vita hiyo inapiganwa kidhaifu hivo???

kabla hajaenda phase ingine ameeleza mafanikio ya phase 2?? au ndio ameshaupata umaarufu alioutaka kwa kuchafua watu ambao wamekutwa hawana hatia???
 
Back
Top Bottom