Whoever said money can't make you happy, has never had enough...quoted, I'm yet to prove that
...dahhh, am speechless kaka...na kweli, katika miaka kumi na mbili nikijumuisha najikuta nimeishi na familia siku 365 tu!
Swali gumu hili, ila kwangu naona kizazi cha Leo tumependa sana Kipato ama mali kuliko Familia, nasema hivi kwa sababu, unapata mtu katokomea hukooo nchi za mbali. Mtu akaa miaka ya kuhesabu, kipato anachopata wastan, pia nae ana mahitaji na maisha pia huko aliko si rahisi, huku nyumbani akituma, hela zenyewe hazitoshi....uzushi na wasi wasi unaanza.
Kumbuka wakati huo huo watoto wanakosa malezi na uzazi wa wawili. Mimi naona wakati mwengine, tukae chini kwanza na kujiuliza kama shughuli yenyewe itajipa kwa manufaa ya sasa na siku za baadae kwa familia. Familia jama....iwe kitu cha kwanza..isiwe Baba unasafiri mpaka ukirudi humkumbuki mwanao!!!!!Na pia ukiwa huko nje miaka Minne mitano..Kumbuka Hapo Mkeo au Mumeo umemwaachia majukumu yoote na huzuni!!!!
Swali gumu ila nimefurahishwa na maoni ya wasomaji wengi kwani wameeleza vema, mambo yote hayo ni muhimu sana kama inakulazimu kuwa mbali na familia yako kwa manufaa ya familia pia na kwa muda fulani huna jinsi ila yakupasa kuwa na mipango yakinifu uhakikisha kwamba kila mara itokeapo nafasi ya wewe kuwa na familia yako basi make sure unaitumia nafasi hiyo vizuri na familia yako. Kuna mifano mingi ya watu ambao waliacha kazi zenye fedha malipo makubwa kwa sababu ya familia ila wao tayari walikuwa na uwezo mkubwa sana na walikuwa na option nyingine na tamaduni pia zilichangia wao kuamua hivyo, ila pamoja na hayo yote bado nakushauri usiipoteze hiyo nafasi ila tumia vema likizo pamoja na familia with time mambo yatakaa sawa tu.
Swahiba,
Unaona hizo zinatosha au ni nyingi sana???
Kama ingewezekana, basi ningependa nisikae mbali na familia yangu kwa zaidi ya miezi 3 mfululizo!!
Kuna kipindi nilisafiri, nikamwacha first born wetu ana miezi 4 na huko nikaa miezi 3. Niliporudi nikakuta mtoto ana miezi 7 na anaanza kufahamu watu na vitu....Yaani alinichunia na kuniangalia kama kinyago... I failed to resist, na kuanza kumwaga machozi!!
Labda naumwa ugonjwa wa kuwa na familia yangu ....ila niko tayari tule majani ili mradi tuko wote na tuko wazima!! Mbona Watanzania walikula majani wakanunua ndege ya Rasi??? Jambo la muhimu ni kuelewana na kukubali kuishi kadri ya kipato chenu!!!!
Babu DC!!
...huwa najiuliza ni lini inafikia kikomo cha kusema sasa kimetosha.
Naamini ni majukumu tu yanabadilika.
Moskwito, I learned this from my old boss, wakati nataka kurukia kazi nyingine. Aliniambia money will never be enough, u think I am being paid a lot but iu still have money issues! I proved it for myself, japo I quited the new-better-paying job in 4months manake yalikuwa yananichachia. You are now dying to live, trust me. Kwani ukikaa na familia huwezi kupata the basics (if it is not too late), kama its too late already, u know what I mean with this; weeh jilipue tu babangu!
...mkuu we acha tu kiongozi, inauma sana...na kuna mengine yanayoumiza zaidi mfano kama huo ulotoa
mwanao wa kumzaa anapokuangalia kwa jicho la "...huyu nae nani!" au utaniambia nini wewe, kwani ulikuwa wapi
maisha yangu yote.
Hiki kisu kinakata kote kote,....mfano mzee wangu, yeye alikuwa anafanya zile kazi za wito...24hrs yupo on call ila alihakikisha kila jumapili ni family day. Bahati mbaya, elimu yangu ya sekondari yote nilisomea boarding school, mambo ya kurudi nyumbani twice a year...
...ipo siku tayari nishamaliza chuo, naye umri ushamuingia tumekaa tunapiga story na kucheka...ikamtoka
" ...nimepoteza a valuable time ya kukuona ukikua mpaka leo ushakuwa mtu mzima tunaongea haya!"...aisee, siwezi kusahau
huzuni yake alipoyatamka maneno hayo.
Mwenyezi mungu amrehemu huko alikolala.
Ahsante dada,
Hiki ndicho nimekuwa nikiongea wakati wote...Watu wanahangaika ila wanasahau kuwa safari moja huanzisha nyingine...Unapata pesa nyingi na hapo unaanza lust ya kutafuta nyingi zaidi.
Tunashindwa kujiuliiza, why mtu kama Bill Gates bado anafanyakazi??