Wengi hawajui kwanini tunasema 'Life begins at 40'

Wengi hawajui kwanini tunasema 'Life begins at 40'

Siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa kuelezea maisha. Yani wale wanyewe kufuatilia sana burudani wanaonekana watu wa hovyo kabisa,lakini hapohapo wale wenye kutoa hizo burudani na kuwaingizia kipato huonekana wachapakazi.
 
Maisha ni kuishi, kipindi chochote kile, si kusubiri ufike umri flani
 
Nasib umenena vyema.

Nafikiri pia maana ya kusema life begins at 40 ni kwamba akili imeshakomaa. Na unaweza kuhudumia familia kwa mahesabu zaidi na kumshirikisha Mungu. Kwamba badala ya kukaa bar na Malaya, kukaa na familia inakuwa vizuri zaidi.

Nilisoma article moja kuhusu singapore. Vijana wengi wanapiga kazi kama punda. Ile kupiga kazi hasa mpaka akifika 40 something kaishakuwa milionea na sasa Ana settle kuendeleza familia. Sasa mazingira yao na sisi ni tofauti.

Lakini NASIB. Mara nyingi life ni jinsi wazazi au walezi au ndugu watakavyo kumould. Kama tangu shule wazazi walikupa ABC za maisha. Kama jinsi ya kusave, labda usomee kitu gani, kozi ipi ni nzuri na ipi sio nzuri. Yaani mzazi anakupa muelekeo wa kufanikiwa maisha kinadharia. Au unakuta first bone wenu kakaimishwa uongozi na mzee au mama vizuri. Na anatoa support kwa wadogo zake na direction vizuri hapo UNAWEZA kusema life begins at 40.

Lakini mtu ambaye hata baba au mama hajawahi kumwambia soma. Akijisikia kusoma poa asipo jisikia poa. Baba wala mama kama alikuwa nao hawakuhi kumwambia labda somea kitu Fulani. Yaani yeye maisha yake ni Mungu tu. Ana hustle hapa na pale ale na ana familia. Mtu kama huyu ukimwambia life begins at 40 unamwonea sana.
 
Uw
Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40.

Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!!

At 40 inabidi uwe unaishi. Siyo ndo unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.
At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?

At 40 utakuwa bado unaomba nauli kwa baba na mama kwani?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu.

Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana.

Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi. Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40.

Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe inasubiri maisha bora CCM ndo wakupe. Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram unaLIKE picha za Wema Sepetu.

Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see?

Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload.

Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili..
Uwiiiie uwieee yelewiii, kelewiiii
 
Kweli kabisa
 
Mtoa mada amesema vyema. Lakini si kweli kwamba life begins at 40. Mimi naona Ameweka perception yake.

Binafsi kwangu life will begin at 30. By now nina basic education i.e degree (i dont trust in masters so hata nikija kuisoma siyo achievement kwangu) and By 30, nataka niwe na kwangu, gari yangu na ya mke wangu, niwe naweza kusaidia jamii inayonizunguka.

Kuwa na mtoto au kutokuwa naye ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu. Life is for you and your wife. Watoto ni sehemu ya jamii inayokuzunguka. Hivyo, ukijipanga vyema unaweza kuwasaidia wao na jamii nzima inayokuzunguza bila upendeleo.

Vijana in your 20s Msicheleweshwe na life begins at 40, hao wamechelewa wanajaribu kujificha humo.

Adios.
 
.
*LIFE BEGINS AT 40.... HOW OLD ARE YOU?*

Life Begins at 40..

Huo ni msemo wanao waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha [HASHTAG]#halisi[/HASHTAG] yataanza rasmi siku ukitimiza *miaka 40.*

Hapo kama bado nauli ya *daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk* basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.
Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika.

Sikia kijana mwenzangu *TODAY* is your future kwa taarifa yako..

Ulipokuwa mdogo ulisema, nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. *Je unayo?* Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.

Kama haijatokea je bado *hujawa mkubwa?* Basi kama ni mkubwa ujue kuna *kitu hujafanya.*

*Utasema tena nikifika miaka 40* nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda.

Usishangae kufika *40* bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini.

*Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!*

Hapo ndo unawaza kufuga *ng'ombe* wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu *12 kwa 15!*

Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha *bizness in Australia.*

Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa *300M!* Wamejenga mjengo wa ukweli.

Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz *(Google that).*

Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full *kutukanwa na makondakta.*

Wenzako in their *40s* wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo *una-mute!*

Wenzako in their *40s* wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia *5M* kimyakimya.. Wewe ukitoa *laki moja* basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita *Freemason.* Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... *(Malizia)*.

Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea UKUTA uwepo au usiwepo.. Sijui kuvunja viti uwanja wa taifa. Harmonize anajua kuimba au hajui. Wema Sepetu atafute mtoto au aache tu. *Can you imagine?*

Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina. Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali. Walishafika kuanzia *Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!!*

Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku *Tegeta Posta* ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! *Unaishi* au *unaisha?*

Acha mawazo mgando. *Eti mi nina mshahara mzuri.* Mshahara mzuri? Kweli?

*Sikia, hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu.*

Jiandae kusimama mwenyewe.

*Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini?* Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. *Don't be afraid*. Don't dwell in that comfort zone!! *Unasubiri kiinua mgongo?*

*Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi.*

*Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa.*

Kwa nini hukufungua ukiwa *30yrs* ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect. Kisa ulikuwa unafatilia ratiba zote za mechi za mpira na matamasha na mikutano yote ya kisiasa ukasahau muda unaenda. Hao unaowafatilia wako ndani ya kazi zao kwa hiyo muda wao unatumikia shughuli zao wakati wewe utatumia muda wako na pesa yako kwenda kuangalia nk.

*Jenga nidhamu mpya ya kulinda muda wako sasa.*

*Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET.*

Halafu ukianza kuregret ndo *pressure zinakuja, stress,* nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha na kuongelea mambo ya siasa sijui wasanii sijui msanii gani ana hela nyingi sijui nani kafulia sijui nani ana mimba.. Seriously? Sijui nani hajapendeza kunyoa bora asuke[emoji35][emoji34][emoji34]. Hivi vitu vinaiba muda wako sana ndugu zangu. Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo lakini nikastuka mapema sana! Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa. Ndo umri huo. Umri siyo mwaka kwa mwaka. Ni sekunde na dakika. Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY. Utashangaa unapoteza muda afu unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu. Be careful. Time flies.

*Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?* So kama wewe unasema "Mimi bado mdogo.." endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late. Endelea tu kupoteza muda na skendo za wasanii. Au unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake. Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira. Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa *sh Bilioni mbili kwa ajili ya kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo wewe unamiliki kigari cha mkopo unakipaki uwanja wa CCM unalipia sh 1000/- tu, *mnaita buku*. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri. Ilikuwa *January* sasa *November * hii. Mwaka unayoyoma. Wewe mwaka huu nini kipya hasa umefanya kimaendeleo. Kupost kuhusu *Lipumba*? Au *Scorpion?*

*Life begins at 40 my friend.... How Old are you now?*

You can change your life even now!

*TUBADILIKE*
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom