Wema Sepetu aonesha alama ya Freemason liveeee!

Bongo movie ni hatari sana wale vijana full ngonoka na ufuska na uswahili kwenda mbele usisahau ulozi
 
Jamani hii kitu nimeisoma mahali, nikaona si vibaya nikiwarushia wanaJF hasa ambao hawajaiona. Soma mwenyewe basi...SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa huku akiwa na ujauzito wake, Amani linashuka na mistari ya habari hii.
Akizungumza na Amani jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka sana.
“Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?” alihoji Jeff.
Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu mwingine.
“Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!” alishangaa Jeff.
Juhudi za kumpata Aunt ili kuthibitisha madai hayo ya ujauzito hazikuweza kufua dafu baada ya simu yake anayoitumia huko Umangani kutokuwa hewani.
Jambo lingine lililomshtua Jeff ni kusikia kuwa aliyemuoa Aunt huko Dubai anaitwa Sunday Dimonte kwani msanii huyo ‘alisevu’ namba yake kwa kutumia jina hilo.
“Nilipomuuliza kwa nini ananisevu kwa jina la Dimonte, Aunt aliniambia kuwa jina hilo lilimaanisha mpenzi kwa Lugha ya Kifaransa,” alisema kwa masikitiko Jeff.

Mim huwa siamini habari ya upande mmoja,kama Aunt hakupatikana walikua na ulazima gani wa kuiandika habari hii
 
yaani bongo bana,filimason,filimason! hivi hii singo bado inabamba!? teh,teh!
kwa watu wanao amini mungu hawatochoka kuwazungumzia hawa jamaa(freemasons) hata kama si wote wanafanya yale ambayo mungu ameagiza tufanye na kuacha yale aliyokataza .Ndugu rejea itabu vitakatifu ususni biblia kwenye vitabu vya ufunuo na injili hawa watu wametabiriwa.Jaribu kuangalia matukio yote makubwa yanayogusa jamii duniani then compare na maandiko hapo utapata mwanga kwanini kila mtu freemason freemason ni kwa sababu ya hofu ya watu juu ya hawa jamaa kutuletea utawala wa lucifer waziwaz na kushurutisha .Kama nimeongea pumba sawa kwani LUTU na NOAH waliambiwa hivyo hivyo japo mi si nabii .FIGHT FOR YOUR EVERLASTING LIFE IN JESUS NAME.AMEN
 
Hivi wabongo freemason mmeijua mwaka jana nini.? Kila celeb w kibongo sasa hvi mnasema ni masonic, hvi mnajua kwamba freemason sio kama mnavyoichukulia nyie., its not that simple.. Kuna hadhi ya watu na vigezo vya kuingia freemason.. Kwanzia pesa uliyonayo na power uliyozaliw nayo kumanipulate watu.. Kibongobongo sidhani kama kuna artist mwenye uwezo huo, wataishia kwa waganga wao tu kutafuta mafanikio. Deep in ujue vizuri vigezo vya freemason ndio utaelewa.. Wema hiyo ni wazi alitaka ku-make headlines., mbona mnataka kusahau kwamba yy ni Mrs.magazeti?
 
Freemason na nyumba za kupanga wapi na wapi?
Umaarufu unawasumbua tu
freemason sio kazi ndogo kama unavofikiri
ni level ya kibilionea
 
.... huyo anapenda kutengeneza stori kwenye magazeti, hakuna kitu hapo......!
 
wavivu wa kufikiri watajiunga sana freemason ili wapate easy cash.the scripture must be fulfilled
 
free mason haina jinsiayoyote anaweza kua free mason after all ni makubaliano yako na shetani kwamba atakupa utajiri wewe utampa roho yako na kumsaidia kukusanya roho nyingine kupeleka motoni huo ndio uhalisia wa free mason ambao mungu wao ni Lucifer
 
Roho yake ndio utajiri wake ni matter of consideraions tu unataka mali yes nataka mali nie ntakupa kila unachotaka Dunia hii kwa "undisclosed cost" utaijua ukishakula kiapo na hapo ndipo utakundua kwamba huna power to reject, hapo ndipo unapoambiwa gharama ya utajiri ulionao ni roho yako na zile nyingine ulizotoa kafara roho ambazo hazijajiandaa kufa kiroho.
To be Honest free mason sio kitu kizuri kukizungumzia kukisikia kukifuatilia au hata kukifuata(kukisadiki) coz ni other side of God our creator.
 
IMG_3267.JPG


T20.jpg


T18.jpg


Angalia kwa makini vidole vya mkono wa kulia wa Wema Sepetu,
Anaonesha ishara ya Wajenzi Huru (Freemason) lakini anafanya hivyo kijanja sana maana kageuza kiganja.
Alama aliyoionesha haina utofauti na hii ya George Bush Jr.

bush_satan_sign.jpg


Sitaki kabisa kuamini kama ilikua ni bahati mbaya, maana Wema anaonekana kwa kudhamiria, amepozi kwa picha.
Na wala siamini kuwa alikua hajui anachofanya, maana habari hizi watanzania wengi twazijua sasa


"Mwenye macho haambiwi tazama"

Kumbe wana vitege!
 
Freemason hawaruhusu mwanamke kwenye jamii yao.labda awe kwenye freemason fake
 
IMG_3267.JPG


T20.jpg


T18.jpg


Angalia kwa makini vidole vya mkono wa kulia wa Wema Sepetu,
Anaonesha ishara ya Wajenzi Huru (Freemason) lakini anafanya hivyo kijanja sana maana kageuza kiganja.
Alama aliyoionesha haina utofauti na hii ya George Bush Jr.

bush_satan_sign.jpg


Sitaki kabisa kuamini kama ilikua ni bahati mbaya, maana Wema anaonekana kwa kudhamiria, amepozi kwa picha.
Na wala siamini kuwa alikua hajui anachofanya, maana habari hizi watanzania wengi twazijua sasa


"Mwenye macho haambiwi tazama"
Mbona hakuna jipya hapo?
Hiyo alama inamaana ya "I love you" kwa mujibu wa American sign Language inayotumiwa na viziwi duniani kote
 
Mbona hakuna jipya hapo?
Hiyo alama inamaana ya "I love you" kwa mujibu wa American sign Language inayotumiwa na viziwi duniani kote

haya bhana..ila do again your research mkuu
 
Back
Top Bottom