Wema: Natamani nikutane na Diamond tuyamalize, ila …..

Judi wa Kishua

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,066
1,048
Nani ambaye alikuwa hayajui mahusiano ya Wema Sepetu na Diamond? Hakuna ila yalikuja yakazima ghafla kama mwanga wa mshumaa, kila mtu akaendelea na maisha yake lakini vita ya mashabiki wao haijaisha kiasi cha wao wenyewe kushindwa hata kupeana support.

Hali hiyo imemchosha mwanadada, Wema Sepetu ambaye ameamua kutoa ya moyoni, amesema anatamani kuonana na Diamond wazungumze wamalize tofauti zao.

“Na nnatamani, one day tuweze hata tuka kaa hivi tukaongea nikamwambia bwana embu tuondokane na mambo haya yote whatever it is me nitakusupport, wewe ukinisupport wala usiponisupport sababu yule naye mswahili sana” Wema Sepetu alifunguka

Mbali ya kutaka kuyamaliza Wema amefunguka kuwa bado kuna kutoka kwa Diamond ambaye amedai kuwa bado anampinga kwenye mambo mengi, ametolea mfano jinsi Diamond alivyotaka kufanya kumpokonya ukumbi wa King Solomon kwa kutaka kulipia siku moja ambayo na yeye amepanga kufanya show kwenye ukumbi huo,

“Me naandaa hii show ya Christian Bella, nimepata ukumbi pale King Solomon sawa, yule mtu wa King solomon nimefika pale, tumeshaongea bei ya ukumbi na kila kitu nikamwambia mimi hapa nitakuja kulipa jumangapi jumatatu, tumeongea ilikuwa Ijumaa, Jumamosi naongea na yule mtu wa King Solomon, Jumatatu naenda pale naambiwa hivi, naambiwa kwamba Diamond anataka kuuchukua ukumbi kwa tarehe hiyohiyo tisa unaona, nikamwambia hivi, nikamwambia hivi ye anataka ku’host party? akanambia nimemwambia ukumbi umechukuliwa akaniuliza na nani, nikamwambia kachukua Wema, akanambia me niko tayari kupanda dau, Unaona” Wema aliendelea kuelezea “Mwisho wa siku me namchukulia Diamond kama mtu ambaye amekuwa kimuziki lakini yeye ki’personality bado”

Hata hivyo Wema amesema kwasasa hawezi tena kurudiana na Diamond, amedai kuwa kwasasa anamuona kama icon wa muziki wa Bongo tu.
 
Basi sawa judi wa kishua! Vipi wema swaumu inapanda? Anapenda kufturu nini?!
 
Maskini Zari kwa inavoonekana Kama diamond alifanya vile ni kwamba alifanya kwa sababu Ana hasira na wema na MTU ukiendelea kuwa na hasira na X wako it means bado unampenda, nina imani wema akitaka kurudiana na diamond diamond haweza kataa.. Maskini Zari
Wanawake wengi ndio mawazo yenu yalivyo ivyo.ila mngejua c wanaume tulivyo msingejipa moyo ivyo.
 
Maskini Zari kwa inavoonekana Kama diamond alifanya vile ni kwamba alifanya kwa sababu Ana hasira na wema na MTU ukiendelea kuwa na hasira na X wako it means bado unampenda, nina imani wema akitaka kurudiana na diamond diamond haweza kataa.. Maskini Zari

Yani Diamond akimuacha Zari na kurudi kwa Wema ni sawa na ukatoka kuishi Masaki na kuhamia Kigogo.
 
Yani Diamond akimuacha Zari na kurudi kwa Wema ni sawa na ukatoka kuishi Masaki na kuhamia Kigogo.
Mkuu kwa wema alikaa nae muda mchache lakn alishatangaza hadi ndoa kwa kumvisha Pete and what about zari, mpaka kamzalia hadi mtoto maskin ya mungu hajaonyesha hata dalili ya kumuoa basi hata kupropose tu ,ndo kwanza anamuhimiza kutoa mimba ya pilu
 
Mbona unasema kitu ambacho daimond ajasema mkuu
Kwasasa hawez sema lakini matendo yake yanaonyesha Kama wema alivoelezea hapo kwamba alimpokonya ukumbi yeye akaongez dau hiyo inaonyesha alikuwa analipa kisasi kwamba hajawhi kumove on bt thinking of wema kila siku. Ukweli unauma
 
Back
Top Bottom