Wekeza kwenye uchimbaji wa dhahabu kwa mtaji wa Tsh. milioni 60

Maduara mawili tu nashusha mwenyewe lakini ninalamani ya uhakika ya Utajiri hapo. Andaa ramani ya gest. Kunamukanda wa nyanda 24 wenye ppm 20


Awww! Yaan ww hatari tupu..sema tu mie ni kakismart nitafata nyayo zako..sema ninataka kujitwist kidg kivingine!..hongera tuombeane heri tu!
 
Kikubwa mtaji mzuri. Utaalamu na weredi wa kutosha.
Ila nako
Unaweza toboa au ukafirisika kabisa
 
Mimi nauliZa hivi mercury nyekundu dumu mojaa inawez kuwa bei gani hii kitu nipambana sana kuipata ila now naogap kulizwaa msaada

Hakuna proof yoyote kuwa kuna red mercury
Mkuu huwa wanadanganyana kuwa ukipata kichupa kama cha dawa ya sindano umeula
Sasa wewe unaongelea dumu kabisaaaa
 
Mkuu itakuwa bora kwanza ufike eneo la tukio uone hali halisi. Ila kama unaweza supply zile gunia za katani siyo jute huku ni deal sana maana ndizo zinatumika kutoa mawe shimon na zinauzwa hadi 8000 iwe used or mpya
Vipi suppy ya vile viroba vya kubebea mawe?

Gunia za katani zinaweza kuisha ngapi kwa week kwa makadirio?
 
Huuu uzi wa Wanga.
Kazi za Madini hapa Tanzania zinahusisha Kafara sana. Huko Kahama, Geita, Chunya, Musoma na Tarime ni mwendo wa kuzindika Tumigodi tyao au Marundo yao na Viungo vya Binadamu. Sitaki kukumbuka mauaji ya Wanawake na kuondoa Kiungo tekenyu. Mlaaniwe kabisa nyie mnaotafuta Utajiri kwa kuondoa Uhai wa Binadamu wengine manina zenu mtakufa kwa laaana, hapa mnabana pua ooooh Mercury kumbe wanga wakubwa nyie.
 
Dah
Unaweza kuwekeza kwenye uchenjuaji wa dhahabu na ukapata faida kubwa sana kea muda mfupi kutokana na kiasi ulichowekeza.

Kuna sehemu inaitwa Mwamazengo iko huko Mwanza kuna eneo lina leseni kwa ajili ya uchimbani wa dhahabu.
Pale ukiwa na mtaji wa Tshs 50 milioni ndani ya muda mfupi inaweza double kila mwezi.

Huhitaji leseni kufanya shughuli ya kuchenjua dhahabu maana eneo lenyewe lina leseni.

Usichimbe mwenyewe kwakuwa utatumia ela nyingi na unaweza poteza pesa wewe ni kununua mawe yalikwisha kuchimbwa.

Utahitaji pia uwe na crusher yako kwa ajili ya kusaga hayo mawe. Itabidi ununue mawe yasiyopungua tani walau 300 ambapo tani moja ni between 30000mpaka 120000 kutoka na kiasi cha dhahabu kilichomo. Crusher itakuwa ikiyasaga, ambapo mchanga utapitishwa kwenye process ambayo ndiyo inaozesha mchanga dhahabu inapanda jui then inakuwa tapped.

Kwa mawe kiasi hicho hukosi dhahabu kiasi cha 1kg plus ambapo ukiuza ni zaidi ya mills 100 na process nzima inaweza kuchukua miezi 3. Inabidi ununue mawe mengi upate dhahabu nyingi kwasababu kuya process ikiwemo chemicals, kukodi visima, na other costs ambazo ziko fixed ni kama 20 mls, so lazima ziwe covered. Yani kina fixed costs haijalishi ni mawe kiasi gani unaprocess.

Ikishapata dhahabu pale watu wa madini watakuandikia karatasi ya kiasi cha kodi cha kulipa serikali ambapo ikienda kuuza mwanza mjini watakata kodi na kukupa risiti. Pia, utalipa kiasi cha tshs30,000 kwa halmashauri kila mwezi. Watu wako huku wanapiga ela mjini wanarudi tu kula bata. Ila inahitaji uoate mtu sahihi na mzoefu katika hizi kazi.

Hii dhahabu iliuzwa 120 milioni kodi ililipiwa 8 milioni. Gharama za mawe na kila kitu ilikuwa approximately 55 milioni
Process nzima ilichukua miezi 3 na week moja.

View attachment 1259121
View attachment 1259125
View attachment 1259122
 
Back
Top Bottom