Wekeza kwenye uchimbaji wa dhahabu kwa mtaji wa Tsh. milioni 60

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,705
Unaweza kuwekeza kwenye uchenjuaji wa dhahabu na ukapata faida kubwa sana kea muda mfupi kutokana na kiasi ulichowekeza.

Kuna sehemu inaitwa Mwamazengo iko huko Mwanza kuna eneo lina leseni kwa ajili ya uchimbani wa dhahabu.
Pale ukiwa na mtaji wa Tshs 50 milioni ndani ya muda mfupi inaweza double kila mwezi.

Huhitaji leseni kufanya shughuli ya kuchenjua dhahabu maana eneo lenyewe lina leseni.

Usichimbe mwenyewe kwakuwa utatumia ela nyingi na unaweza poteza pesa wewe ni kununua mawe yalikwisha kuchimbwa.

Utahitaji pia uwe na crusher yako kwa ajili ya kusaga hayo mawe. Itabidi ununue mawe yasiyopungua tani walau 300 ambapo tani moja ni between 30000 mpaka 120000 kutoka na kiasi cha dhahabu kilichomo. Crusher itakuwa ikiyasaga, ambapo mchanga utapitishwa kwenye process ambayo ndiyo inaozesha mchanga dhahabu inapanda jui then inakuwa tapped.

Kwa mawe kiasi hicho hukosi dhahabu kiasi cha 1kg plus ambapo ukiuza ni zaidi ya mills 100 na process nzima inaweza kuchukua miezi 3. Inabidi ununue mawe mengi upate dhahabu nyingi kwasababu kuya process ikiwemo chemicals, kukodi visima, na other costs ambazo ziko fixed ni kama 20 mls, so lazima ziwe covered. Yani kina fixed costs haijalishi ni mawe kiasi gani unaprocess.

Ikishapata dhahabu pale watu wa madini watakuandikia karatasi ya kiasi cha kodi cha kulipa serikali ambapo ikienda kuuza mwanza mjini watakata kodi na kukupa risiti. Pia, utalipa kiasi cha tshs30,000 kwa halmashauri kila mwezi. Watu wako huku wanapiga ela mjini wanarudi tu kula bata. Ila inahitaji uoate mtu sahihi na mzoefu katika hizi kazi.

Hii dhahabu iliuzwa 120 milioni kodi ililipiwa 8 milioni. Gharama za mawe na kila kitu ilikuwa approximately 55 milioni
Process nzima ilichukua miezi 3 na week moja.

IMG-20191109-WA0000.jpeg

Sio rahisi kama ulivyoandika, biashara hii ni kama kamari unaweza pata faida kubwa ama hasara kubwa, zaidi hainaga hasara ndogo. Sio kila mawe utakayonunua yana dhahabu kuna utaalamu wa kuyatambua, na mbaya zaidi uweke mtu wewe uwe Dar uwe unapewa taarifa. Utawapa mitaji watu au kuwajengea nyumba. Ushauri wangu ni bora utumie muda na gharama kijifunza uendeshaji wake ndipo uwekeze biashara hii ya uchenjuaji dhahabu.

IMG_20191017_183622_2.jpeg
 
Kuna watu wanaenda tapeliwa hapa.
Kuna watu watapoteza hela hapa.
Utauziwa mawe
utayasaga
Utakodi plant

Mwisho wa siku watakuibia Carbon au utaenda choma hupati hata gram 200

Siku hizi kuibiwa loaded carbons ni nadra sana labda kula mzinga baada ya elution.

Hii kazi inawatoa watu sana na pia inawaangamiza wengi sana wanaoingia kichwa kichwa. Chamsingi kama huna pesa na uzoefu wa kutosha usijaribu.

Ukitaka kufanikiwa pambana mwenyewe mwanzo mwisho na usimuamini mtu yoyote hata kama ni ndugu yako achilia mbali rafiki.
 
Mkuu unalosema ni kweli kabisa wala hauko sawa nimeanza hii shughuli mwaka jana na sikuanzia hapa nimeanzia huko mbeya nanunua makinikia mimi na rafiki yangu sikuwahi kula hasara isipokuwa kuna siku niliondoka huko nikamwachia mtu aninunulie mzigo akaninunjlia mzigo fake ndipo nilikula hasara ya 14 milioni.
Ila kabla ya kununua hasa makinikia lazima upime mzigo maabara.

Sio rahisi kama ulivyoandika, biashara hii ni kama kamari unaweza pata faida kubwa ama hasara kubwa, zaidi hainaga hasara ndogo. Sio kila mawe utakayonunua yana dhahabu kuna utaalamu wa kuyatambua, na mbaya zaidi uweke mtu wewe uwe dar uwe unapewa taarifa. Utawapa mitaji watu au kuwajengea nyumba. Ushauri wangu ni bora utumie mda na gharama kijifunza uendeshaji wake ndipo uwekeze biashara hii ya uchenjuaji dhahabu.View attachment 1259373
 
Na ndiyo maana nimesema lazima uwe na mtu mwenye uzoefu. Huwezi fanya hii biashara bila kuwa na mtu mwenye uzoefu. Mimi na partner wangu tuna mtu ambaye ni mtaalamu sana wa haya mambo na hapa Tanzania hakuna kama yeye alikuwa anafanya kazi kwenye mgodi huko Australia akaacha akarudi Tanzania na hapa kila muda kasafiri anakodiwa migodi mbali mbali afrika na nje.
Siku hizi kuibiwa loaded carbons ni nadra sana labda kula mzinga baada ya elution.

Hii kazi inawatoa watu sana na pia inawaangamiza wengi sana wanaoingia kichwa kichwa. Chamsingi kama huna pesa na uzoefu wa kutosha usijaribu.

Ukitaka kufanikiwa pambana mwenyewe mwanzo mwisho na usimuamini mtu yoyote hata kama ni ndugu yako achilia mbali rafiki.
 
Unanunuaje mawe bila kuyapima? Hufanyi kwa kubahatisha ila unafanya baada ya kuyapima. Hasara tuliyokula ni mara moja tena ni kwasababu ya kuacha mtu aninunulie mawe akaniongopea
Kuna watu wanaenda tapeliwa hapa.
Kuna watu watapoteza hela hapa.
Utauziwa mawe
utayasaga
Utakodi plant

Mwisho wa siku watakuibia Carbon au utaenda choma hupati hata gram 200
 
Siku hizi kuibiwa loaded carbons ni nadra sana labda kula mzinga baada ya elution.

Hii kazi inawatoa watu sana na pia inawaangamiza wengi sana wanaoingia kichwa kichwa. Chamsingi kama huna pesa na uzoefu wa kutosha usijaribu.

Ukitaka kufanikiwa pambana mwenyewe mwanzo mwisho na usimuamini mtu yoyote hata kama ni ndugu yako achilia mbali rafiki.
Habar kiongoz?wewe unauwelekeo wakufahamu hii kazi,kuliko ata aliye post.mleta mada hii kazi siyo kama ulivyo sema usipende kuadisia au kufika eneo ukaona process zinavyofanyika ukaona ni rahisi kama ulivyo kuja speed hapa jukwaani hapa wapo ma- master wa hii kazi ukiambiwa unaweza ukaona unahitaji zaidi uelewa wa hili jambo.MWISHO usipende kuongea kitu kabra haujamaliza utafiti wako juu ya jambo husika.
 
elmagnifico,

Ndo nyinyi huwa tukiwaleta sait hamtaki kujifunza mnakalia kupiga picha na ku-post,embu tuambie process za hizi?

1.MAABARA wana deal na vitu gani, ili kujua makenikia yako yana PPM ngapi?
2.mawe unayosema ukinunua ya 50mill je?nisawa na tani ngapi?
3.chemical unanunua za kiasi gani katika tan uliyotupa ya hesabu '2'
4.sample unapima kwa gharama zipi?.
5.ukipata sulphur & copper katika makenikia yako anatumia nni kujua hadi kupata gold.ahsante kwahayo machache kwanza.
 
Ndo nyinyi huwa tukiwaleta sait hamtaki kujifunza mnakalia kupiga picha na ku-post,embu tuambie process za hizi?
1.MAABARA wana deal na vitu gani?ili kujua makenikia yako yana PPM?ngapi?
2.mawe unayosema ukinunua ya 50mill je?nisawa na tani ngapi?
3.chemical unanunua za kiasi gani ktk tan uliyotupa ya hesabu '2'
4.sample unapima kwa gharama zipi?.
5.ukipata sulphur & copper ktk makenikia yako anatumia nni kujua hadi kupata gold.ahsante kwahayo machache kwanza

.hahahahhahahaha msamehe bure!
 
Siku hizi kuibiwa loaded carbons ni nadra sana labda kula mzinga baada ya elution.

Hii kazi inawatoa watu sana na pia inawaangamiza wengi sana wanaoingia kichwa kichwa. Chamsingi kama huna pesa na uzoefu wa kutosha usijaribu.

Ukitaka kufanikiwa pambana mwenyewe mwanzo mwisho na usimuamini mtu yoyote hata kama ni ndugu yako achilia mbali rafiki.
Naweza kuongea na wewe private
 
Back
Top Bottom