IQRA DARESALAAM.
Iqra akanyongea kama siku 3, baadae akapata ujasiri wa kurudi kawaida. Akawa anaenda shule na kukaa dukani kama zamani. Ila ile nuru yake ikawa imepotea. Akawa yupo kama hayupo. Babu Ali anamsemesha Iqra usiyachukue maisha, maisha ni kwenda nayo yanavotaka sio unavotaka wewe. We mbona bado maisha hujayaonaaa, unfikiriii? Iqra wala hamjibu mawazo yake yako mbali sio kidogo
Kila akijitahidi kumsahau Jabir anashindwa. Shuleni anashindwa kujizuia, anamuuliza Nadya, Jabir hajaniuliziaaa? Nadya anamjibu kwakweli sijaonana nae mda sanaa so sijajua kama angekuulizia au vipi. Kwani vipi mbona sielewi kwani anatakiwa kuku ulizia? Iqra anaona aibu anazug zuga basi. Nadya akahisi tu huenda Iqra kampenda Jabir.
Alivoona Iqra hakati tamaa, Nadya akaamua kumuuliza Jabir, eti kaka mbona kila siku Iqra ananiuliza kama umemuulizia kwani vipi? Muulizie basi leo nikamwambie umemuulizia. Haahahaaa. Jabir akashangaaa, eeeh anakuuliza kila siku? Nadya akamjibu ndio kila sikuiendayo kwa mola lazima aniulize. Jabir akagunaaa Mmmmmmh! Jabi akamuuliza Nadya kwani wewe unamjua yule mdogo wake hazimtoshi chizi chizi? Nadya akamuuliza Fahad? Namjua ndio si mdogo wake toka nitoke. Jabir akatikisa kichwa kusikitika. Akamwambia sikia mimi Nadya nampenda sanaa, tena sanaa tatizo siwezi kudate nae wakati mdogo wake yupo vile. Nadya akamuuliza kwanini? Jabi akamwambia tuta taniwa sanaaa. Wenzangu watanicheka na kunidhihaki, aaah mi siwezi. Na isitoshe mimi mkali yule chizi akinifanyia kitu cha kijinga naweza hata mbutuuuuuaa Nadya akabakia kusikitika.
Kesho kama kawaida Iqra akamuuliza Jabir hajaniulizia? Nadya akamwambia kiukweli jana kakuuliza. Iqra akatahamaki na nuru ikamrudi usonii. Akamuuliza eeeh alikuuliza nini? Nadya akasema alinambia tu nikwambie kuwa ana demu mpyaaa usimuulizie tena. Iqra akasikia mtu kapita na kisu tumboni raaaaaaaaaaa. Akanywea kabisaaaa. Hakutaka tena mazungumzo ya aina yeyote. Akaenda kuaga kwa matron anaumwaaa.
Akawahi kukaa dukani siku hio, babu Ali anamuuliza kwemaaa? Akawambia ikifika saa 7 mfate Fahad shule. Babu Ali akasema sawa mama. Akawa amekaa anajihisi kufa kufa. Akawa kakosa amaniii na nafsi inamsokota. Siku ilikuwa ndefu sanaa na hio wiki ilikuwa chungu sanaaa. Akawa jeuri na katili sanaa kwa wanaume. Akatokea tu kuwachukia wanaume. Wateja walimkomaaa mbona. Kuogopa kuumizwa akawa ana wawahi wanaume kwa ukauzu ili wasimzoee na kuweza kumuumiza.
Mda si mda akapata jina mtaani kwamba yule binti wa kiarabu usimuone kakaa pale na hijab yake ukajua mpolee, ana majibu ya kunyaaaa huyoooo, ooooohhhh! Anakujibu mpaka utafurahii. Hacheki na kimaaa. Ni kauzuuu balaaa. Utaanzaje kumtongoza kwanza, jicho analokutizama, na anavojiamani si balaa hilo. Yaani ni kauzu zaidi ya dagaaa. Anachekea wanaume wa 3 tu. Baba yake mzazi, mdogo wake Fahad na Babu Ali. Baaaaaaaaaasssss! Wengine hana jema ni kukujibu kunyaaaaaa mpaka utie akili.
Mpaka wafanyakazi wao wamemjuaa kwamba Iqra ni kubwa la maadui. Akija mwanaume kumuulizia na kushoboka nae, utaona wanavo mchoraaa na kumngojea aingie kwa Dr. Iqra kupata Kristapen. Kuna mkaka siku hio alijitia kuleta maua kwa Iqra, wacha achapwe nayo usoniii. Hhahahaaaaaaaaaa! Walicheka mule ndani mpaka basi. Yaani wakakubali Iqra kiboko ya vibolo dinda mjini.
Ikafika birthday ya Fahad, akamshauri baba yake mwaka huo wamfanyie party maana hajawahi kufanyiwa party. Baba mtu akawa na mashaka na hilo akamuuliza sasa ataweza kweli kufanyiwa party na hali ile? Ataweza kuhandle miki miki ya party? Na atamualika nani? Maana hana hata rafiki shule wenzie wote wanamtengaa, na isingekuwa kumuonea imani bibi yao hata shule wasingempokea. Hata jirani hapo hawana rafiki wa kusema amualike. Iqra akangangania wafanye party, si aliona party ya Nadia. Akatamani na kwao wafanye kitu kama kile basi tu.
Baba yake na bibi mtu wakawa hawana budi kumkubalia na kumuachie Iqra aandae kile kitu baba yao atatoa pesa yoyote itayotakiwaa. Akaongea na mamake Nadya akamuelekeza sehemu za kuchukua vitu vya mamapambo, vinywaji keki, kila kitu. Akaongea na mwalimu wa Fahad darasani amsaidie kuwaalika wenzie kwenye hio party, aongee na wazazi wao. Mwalimu akasema sawa akampa na namba zao za TTCL ajaribu kuongea na na yeye kuwasisitiza na kuwaelekeza ukumbi wa hio birthday. Bibi akawa kawapigia wote na kuwaelekeza party ilipo wakawa wamemuitikia sawaa tutakuja ondoa shaka kabisaaa.
Jumamosi party ilitakiwa ianze saa 4 kamili, kukapambwaa, kukapendezaa, Fahad naye akavalishwa nguo mpyaaa, za kupendezaaa, akawa anafurahia baloons, cake, navitu kama hivo maana si anaonaga wenzie wanafanyia party darasani. Ila anakuwa anafanyiwa ukali sanaa na walimu asijaribu kitu. Sasa siku hio hivo vitu vipo na yupo na watu wa kwao, bibi, Iqra, baba kawazoeaaa. Akawa anafurahiiii. Na wimbo wake wa Makarena ukawa unapigwa. Fahad asubuhi hio tu furaha yake ikawa haipimiki.
Saa 5 ikaingia hamna hata mtoto mmoja aliekuja. Bibi na baba wakaanza kupata mashaka. Iqra bado anajipa matumaini watakuja. Saa 7 hamna hata mtoto mmoja aliekuja. Wahudumu wakaanza kuongea wenyewe kwa wenyewe, kujadiliana mmmmh mbona kimavi tenaa, ji party kama hili hamna mtu anaekujaaa, mbona tutafaidi kugawiana mavitu yote hayaaa. Maskini yule chizi alikuwa kafurahiii, inatia imaniii, sasa kwanini hawajaja mpaka mda huu. Yule mwarabu atia imaniiii, na kile kibibi cha kiarabu machozi yana mlenga mlenga. Daaah Imani sanaaa.
Saa saba na nusu Iqra akapanic akajua hawaji wamemsusia Fahad party yake. Ikamuuma roho mpaka basi. Akimuangalia Fahad ndo moyo unamyeyukaaa, akatamani wangekuwepo na watoto anefurahia zaidiii, Akimuangalia baba yake na bibi wanavojikaza anawaona kabisaa lile tukio limewavunja mainiiii umri kama ule. Kukawa kama kuna msiba sasa. Akatoka pembeni karibia na swimming pool akajikuta tu analiaa kwa kwikwi kabisaaaa. Akaka chini na kuanza kulia vizuri kabisaa kwa kujiachiaa sio kulia kwa kujibana bana.
Akasikia dada unalia nini, mbona umekosa raha kabisaa na kunyongeaaa. Kugeuka akamuona mkaka mbae sura yake sio ngeni usoni pake ila hakumbuki kamuona wapi. Akahisi pengine mteja wa dukani ila akawa hana uhakika kabisaa kamuona wapi. Akaedela kulia tu. Yule kaka akampa hankerchief. Akamuulia wewe upo hapo kwenye party? Iqra hapo yuko frustrated hana hata hamu ya kujibu. Akamuuliza nimeona mmepamba mda kweli hamna mtu anaekujaaa, kuna tatizo limetokeaa au watu kutokuja ndo imekufrustrate sana mpaka umelia hivi? Iqra akajikuta tu kapata nguvu z kumsimulia.
Kakka ujue nina mdogo wangu alizaliwa kwa shida sasa, yupo slow sanaa ana miaka karibia 12 ila akili yake kama ana miaka 9 au 8. Sasa nilitaamani tumfanyie party leo. Ila nimewaalika wenzie tumetumia gharam hakuna mtu aliekuja hat mmoja. Nikiwaangalia baba yangu na bibi nakosa raha kabisaa. Akaanza kuli upyaaa. Mungu kwani sisi tumekukosea nini? Kwani sisi ndo wadhambi kuliko watu wote duniani? Kwanini hutaki mdogo wangu afurahi kama watoto wengine japo siku hii moja tu. Why? Anazidi kulia.
Yule kaka akaanza kujisemesha mimi nina mdogo wangu anajuana na watu sanaa, ngoja nimpigie simu alete watu umri wa mdogo wako waje kumshangilia. Iqra akawa kachoka mwili na roho wala hamuelewi anaongea nini. Yule kaka akaenda kuongea na simu ya TTCL. Kapigaaa mda. Baadae akaanza kuongea. Thanks God Carina uko nyumbaniii, sasa sikia mimi nipo huko Embassy Hotel kuna party huku ya mtoto mmoja ni special case kama ana autism hivi. Carina akamkatishaaa Collins go to the point mi hayo yananihusu nini taking into account umenitosa kwenye mtoko wako. Yule kaka akaendelea kumsihi Carina, chonde chonde nifanikishie i will do whatever you ask. Carina akatafakari na kumuuliza wahtever i ask? Are you sure? Collins akamjibu absolutely Carina. All you have to do just get me 10 kids wenye 9 years waje kwenye hii party. then i will do whatever i you want. You have friends with young sis, young bros get your friends to bring their young ones kwenye hii party, ikiwezekana na wewe njoo. The kid anasikitisha sanaa. Carina aksema nimekubali sababu tu ya hapo you will do whatever i want for the whole week. Collins akamwambia poaaa.
Akarudi kumwambia Iqra, the kids are comming now, my young sis analeta friends wake na wadogo zako, you will have your party. Iqra akataka kumwambia bibi yake ila akaona angoje kwanza kama watakuja kweli. Carina akapiga simu kuwaaambia watu, anawaambia wawaambie na rafiki zao waje kuna party ya ndugu yake Embassy. Akaenda na yeye Embassy. Kufika akauliza party iko wapi akaoneshwa akajua Collins hayuko mbali. na kweli akamuona akiwa na Iqra. Akajitambulisha tu, Carina tenaaa alivo fastaa. Im Carry, i came to your rescue. Iqra akampenda tu alivo changamkaa na mwingi wa habari. Carry anamwambia Iqra the entourage is comming are you sure kuna enough food and drinks maana i am afraid nimealika watu wengi sanaaa. Iqra anamuhakikishia money is not an issue tutanunua vingine.
Akampeleka Carry kule kwa baba yake Carry akasalimia Hi! mara ashaenda kumsalimu bibie, Iqra akamwambia baba yake huyu rafiki yangu tunasoma nae kama bahati nimekutana nae hapa nikamwambia kuhusu party ya Fahad ilivoharibika akasema ataleta rafiki zake umri wa Fahad and we can still have a party. Baba yake akawa ashakata tamaa ila akajitia kufurahi na kuwa na matumaini asimvunje moyo Iqra. Carina akawa anacheza na Fahad na anaelewana nae vizuri sanaa. Wakaona anaongea nae kwa vitendo zaidi na Fahad anamuelewa haraka.
Watu wakaanza kuingiaaa wanakuja wa 3, 2, wanamfata Carry, Hi Carry we heard about the party, everything is so Waohhh! I didnt know you had Arab cousins. Carina anazuga you didnt, i do. This is Fahad my cousin he is a little slow but okay he is so sweet when you get to know him. Basi watoto na Hi Fahad! Mda si mda watoto wamejaa kibaooo. Fahad akawa na shangwe la kufa mtu. Watoto sio bibi wala Iqra wala baba yao anajua walipotokea. Waarabu humo humo, wazungu, mataifa ya kutosha.
Carina akawa MC, na MC alipatikana mbonaaa, anajua events zile za kunogeshaaa. Mara watoto wacheze Makarena ataeshinda anapata zawadi. Watoto cheza cheza. Mara washindae kuimba anaeimba vizuri anapata zawadi. Watoto imba imba kuanzia humpty dumpty, babaa black sheep, London wall, tafranii. Kulinohaaa ni balaaa. Watoto wanaongezeka kadri mda unavoendaaa. Kukashona nyomiii la kutishaa. Birthday ya Fahad. Mpaka wanaosoma na Fahad ikawa wamekuja bila kujijua ndo wamekuja birthday ya Fahad manake walifanya kuzolewa na dada zao. Baba yao akashangaa kuna watoto Fahad anawajua kwa majina kabisaa.
Mara waweke viti wacheze stand up sit down mpaka abakie mtu mmoja. Yaani MC alipatikanaa. Jioni mwisho kabisaa ndo waote sasa kwa umoja wao wakamuimbia HAPPY BIRTHDAY FAHAD! VERSION ZOTE 3. Fahad akata keki na sababu Carina anaweza ku communicate nae, akamuelekeza amlishe Baba yao, bibi, Iqra na yeye Carina. Akmuuliza kama kuna friends from schoola ngependa kuwalisha akataja kama 10 akawalisha wote. Basi cake iliobakia ikagawanyishiwa wahudhuriaji wa hapo. Saa 12 Carina akaifunga party kila mtu aende kwao.
Iqra akamshukuru Carrina kupita maelezo, akamuuliza tu anasoma wapi akmwambia anasoma IST, Iqra akamwambia anasoma Aghakani. Iqra akamkaribisha dukani kwao, Carina akamuuliza mnauza nguo? Iqra akamwambia hapana ni duka tu la electronics. Ila akiwa Kariakoo asiache kumpitia. Na wana duka lingine la nguo, akija atampeleka akachague anachokitaka. Waka aganaaa.
Iqra, bibi, Fahad, na Mzee wakawa wamerudi nyumbani na furaha ya ajabu. Wakasema tu Mungu hajawatupaa. Baba na Bibi wakawa wanashangaa Carry aliwezaje kuongea na Fahad wakaelewana wakati hajawahi kukaa nae hata siku moja, wakashindwa kuelewa. Tena Fahad akawa ana mtii kweli Carry kila anachomulekeza anafanya inavotakiwa, mpaka kuweza kumcontrol kwenye haliki kama lile, wakakubali kweli Carry kama malika tu ameletwa na Mungu kuwasitiri siku hio. Wakawa wanawaza tu asingetokea Carry ingekuwaje sasa.
Jumatatu Iqra kwenda shule darasani lawama tupuuuu. Iqra umefanya party la kukata na shoka, talk of the city Embassy hujatualikaaa? Iqraaaa! Kweli wewe wa kutufanyia sisi hivo? Party lina madada wote wa mjini mpaka kubwa lao Carry? Kumbe unajuana na Carry wa IST. Lawamaa juu ya lawamaa. Kila anapopita anasalimiwa Hi. Iqra! Mpaka na form 4. It is like kama dunia yake imebadilika ghaflaaa. Walte talk of the school wanamfata Iqra nisaidiee i have a party i need arry aje kwa party yangu, pleaseee pleaseeee. Yaani ikawa sasa Iqra ndo star wa shule sasa.
Moyoni akaanza kuogopa watu wanamuona wa maana sababu ya Carry na yeye Carry ndo kamjua hio juzi na hana uhakiak wa kuonana nae karibuni. Hajui kama atakuja duakni ama la. Chupi ikaanza kumbana si kidogooo.
ITAENDELEA.