IQRA DARESALAAM
Iqra kidogo akawaa kapata ahueni shuleni baada ya ile party, it was like yeye kuwa na ndugu kama Fahad haikumatter tena. Like people didnt really care kama ndugu yake yupo vipi au vipi. Kidogo akapata ahueni na kupumua na kuanza kuwa na normal life like normal teenagers.
Siku Carry alivokuja dukani kwao alipata faraja sanaa, akajihakikishia kwamba atafanya awezavyo wawe marafiki, kiukweli ilikuwa ni jambo la kufurahisha sanaa, ukizingatia it is like Carry gave her life back. Wakawa wameenda dukani akampa zile nguo, na kumdanganya baba yake kachukua yeye, maana ziliandikwa yeye.
Siku hio karudi nyumbani, mda wa kula chakula baba akaanza mazungumzo ila akawa hamtizami usoni. Na bibi pia hamtizami usoni. Akajua lazima kuna kitu sicho cha kawaida. Baba ndo alianzisha maongezi, "Iqra, Uncle Nassor alipiga simu, akatuambia habari njema, tumekaa na bibi tumejadili na kufikia muafaka kwamba tukubaliane na habari ya uncle Nassor. Kikubwa Uncle Nassor alichokisema ni swala la Fahad kwenda kule UK, kuna shule maalumu za watu kama Fahad zenye vifaaa na ujuzi wa kuwafundisha, na itamsaidia sanaa Fahad. Itakuwa ngumu kwetu wote ila kwa Fahad ndo itakuwa jambo muhimu. Ni pesa nyingi sanaa, ila tutajitahidi kadri ya uwezo wetu.
Kabla hata hajamalizia huku Iqra machozi debe. So many times ali wish Fahad asiwepo achukuliwe au sijui apotelee wapi, now that wakati umefika wa Fahad kuondoka nafsi yake ikawa haitaki kabisaa. Akaanza kusema tu mi staki Fahad aondoke nitamuangalia peke yangu. Baba akae akamfanyia ukali kwamba we jiandae tu kisaikolojia, Nassor akikamilisha mipango Bibi atampeleka Fahad, na atakuwa anaishi kule kule kufatilia maendeleo yake. Bibi akiwa karibu na kule hakuna kitakacho haribika.
Iqra akaenda kulala na mawazo mengi sanaa , manake keshamzoea Fahad afu hana uhakika huko mbali kama watamuangalia vizuri, manake kiukweli Fahad anachosha sanaa. Yeye mwenyewe mda mwingine alikuwa anachokaaa sasa mtu baki je kama yeye ndugu tu anamchoka Fahad mara kibao. Akawa kwa upande mwingine anaona bora aende kama kweli ndo watamsaidia kama wanavosema sio mbaya kabisaa. Maybe Fahad anaweza kupona kabisaa maana wale wazungu na wazungu sio watu wepesi.
Akajikuta anakuwa mkarimu mnoo kwa Fahad kuanzia siku hio. Anakuwa kama mjinga sasa. Kila mda anataka Fahad awe karibia yake basi tu awe anamuonaaa. Roho yake iridhike. Dukani anataka akae jirani yake basi anakuwa anampigisha story ambazo hazina hata mbele wala nyuma, mradi mda wote yuko jirani yake anamuona afu basi.
Siku hio wakiwa dukani na Fahad hawana hili wala lile, ilikuwa tu siku shwari kama zingine, akarudi yule mteja wa redio aliezusha sekeseke majuzi. Wakajikuta wanaangaliana wote wasijue la kufanya. Iqra akahisi mwili unakufa ganzi asijue la kufanya kwanza mda huo. Akili yake yote Fahad maana yule mteja akisema ampige Fahad itakuwaje. Akatamani amwambie Fahad kimbiaaa, ila akajua tu Fahad hatomuelewa.
Akazitoa kabisaa pesa alizolipa yule mteja siku ile, hakutaka kabisaa malumbano nae wala nini. Mteja akaja akasalimia Assalam Aleykum habib! Iqra akamjibu kwa wasiwasi Alleykum Salaam! Mteja akaendelelea "Kaifa halak!" Iqra akamjibu "Ana bekhair, shukran!" Mteja akazidiwa sasa sio kwa uarabu wa kunusa. Hapo Iqra kaziweka hela juu ya meza, akianza tu anamtupia hela zote. Hakutaka kabisaaa tabu na yuel mteja.
Mteja kaanza za tangu majuzi? Iqra anamjibu tunashukuru Mungu, wale uliowapiga wameponaaa, wanaendelea vizuri tu vipi baba redio imesumbua tukurudishie pesaaa? Mteja akajibu hapanaaa kabisaaa.Mie nimepita hapa kuwaombeni radhi ndugu zangu kwa fujo zile. Babu naomba unisamehe yaishee, Kijana pale nakutaka radhi, nawaombeni radhi ndugu zangu nilikosea sanaa kuwafanyieni fujo naomba yaishe.
Fahad akawa katoka nje, Iqra akasema afadhaliii, apate wasaha wa kumkaanga yule mteja vizuriii. Babu Ali kashika gongo hapo akaamua kumtolea uvivu, hivi wewe kijana wa kunipiga mimi wewe? Kweli mi si nakuzaa kabisaaa wewe nikicheza bao, ila ulivokosa haya ukaniweka migumi ya hajaa na uzee huu wataka nikajifie mbele kwa mbele na Mungu alivojua kukulaani sasa sijafa wala nini. Kama ulikuja kuchunguza kama nilikufa ndo sijafa sasa, na nakwambia hiviii tokaa dukani kwetuuuu.
Walter akaanza kupanic tenaaa upyaaa, ila akajicontrol akawa kasimama pale pale aliposimamaa. Iqra akamwambia si umemsikia Mzee alichosema Tokaaaa dukani kwetu kama pesa yako sio tatizo hio hapo juu chukuaa redio ile tumekupa tu msaada , chukua pesa yako utoke humu ndani na usirudi tenaaa. Mteja akawa kasimama pale pale anawatizama tu wala hatikisiki kama mtu anaejishauri cha kufanya.
Mwajuma akadaki, sikia kaka yangu mzuri, wewe nenda tuuu, kama redio si ushachukua, au kama ni hela hizo hapo unarudishiwaaaa, usipende kuwa mtu wa fujo kaka yangu, hii dunia tu, na Mungu hapendi tuishi kishari, inatakiwa tuishi kwa amani tu kaka yangu. Sababu ugomvi ulianzia kwenye redio na ushaichukua, basi tuyamalize wewe nenda tuache sie tufanye biashara kwa amani.
Mteja akajibu, mbona mnakuwa sio waungwanaa ndugu zangu? Mi nimekuja hapa kwa heri tu, kweli siku ile sikufanya vema kuanzisha ugomvi na nyie, nimekaa kwangu nimejitafakari nimeona nije hapa kuwatakeni radhi kwa tabia yangu ya siku ile. Nimekuja hapa na nimewataka radhi ndugu zangu, kwa heshima na upendo kabisaaa. Ila nyie mnakuwa watu wa vinyongo na msiotaka kusameh kwanini lakini? Kama hivo nimekuja kuwataka radhi ili nisafishe dhamira yangu nyie mnanifukuza kama mbwa, pasipo kukiri kwamba mmenisamehe na yamepita wala nini. Ndo uislamu unavoagiza hivo? Sawa mi naondoka ila mkae mkujua mlichofanya sio utu kabisaaa. Mteja akatoka kwa hasiraaaa.
Alivotoka wakabakia wanaangaliana wote wamechokaaa sio kwa mteja sugu na kinganganizi kama yule. Alivotoka tu mlangoni wakaanza kujadiliana hivi huyu kaka anatutaka kitu gani lakini? Fujo la juzi kaona halijatosha badooo tu kutuchimbaaa. Hivi mmemuelewa lakini? Ikawa kila mtu asema lake sasa kumpond tu yule mtejaaa, wamejisahu kabisaaa na , akili yote iko kwenye ule mjadala wa yule mteja sugu.
Katikati ya mjadala wakasikia kelele nje, "Aiyaaaaaaaaaaaaa kauaaaaaaaaaaaaaaaaa! Mama weeeeeeeeeeeeeee! Mtumeeeeeeeeeeee! Yesuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!" Wote wakakimbilia kutoka nje! Iqra ndo kupata mstuko Fahad yuko wapi? Hawamuoni! Wakatimua kwenda nje! Kufika nje wanakuta watu wamejaaa, kuna zogo kubwaaa! Kila mtu anaongeaga lake, angemuua. Wengine wanatetea mtoto mwenyewe hajielewiiii, dreva hana makosaa, dogo ndo kaingia barabarani kichwa kichwa. Iqra akajipenyezea mpaka akaingia katikati ndo kamkuta yule mteja yuko na Fahad.
Pozi likamuisha kwanzaaa, akafa ganzi mwili, pembeni ndo akaiona gari na dreva ndani. Kwa mazingira ya haraka haraka inaonesha Fahad alikuwa anagongwa na gari kabisaa afu yule mteja ndo kamuokoaaaa. Fahad hata hajielewi. mteja ndo wametoka kumchamba mda si mda tena wima wima anamwambiaje sasa. Akaona maji marefu sanaa yale. Akapiga hesabu za haraka haraka, akajipenyeza kimya kimya kurudi dukani kakaa kimya kajikausha bado kiroho kinamuenda mbiooo.
Wakaja kina Hamis, babu Ali na Mwa J kwa mpigooo kumsimuliaaa Iqra yule mteja kamuokoa Fahad hapo nje. Iqra yuko na mimi nimeona basi kamchukueni, maana mi naona haya si kwa yale tuliomjibu mda mfupi uliopitaaa. Kila mtu anamsakizia mwenzie wote wanaona haya kwenda kumfata Fahad. Wakiwa wanatupiana mpira wa nani akajiaibishe na kumchukua mtoto nje, wakamuona Mteja anaingia na Fahad mkononi, wakaangaliana wote kimyaaa.
Babu Ali sababu mtu mzima akajikusanya akaanza kujichekesha, wooooo, mteja wetu wa ukweli kabisaa, tunakukubali, asante kwa kutuokolea mwanetu. Mungu tu ndo atakulipaa. Eti anampa stuli kabisaa akae. Makubwaaa. Mwanangu kitu ulichokifanya leo Mungu akuzidishie ulicho punguza. Uislamu ndo unavotaka hivo. Anaongea maneno mia nane yasiyo na uhusianoooo. Mteja kimyaaaa.
Mwajuma na Hamis wakadakia asante kaka, asanteeee. Mungu akubariki kabisaaa. Ulichokifanya Mungu tu ndo atakulipaa, tusameheane kwa yote, yale ya zamani yameishaaa. Tumeshakuwa ndugu sisi uongo kaka angu. Yaani sijui hata niongee nini, kaka yangu unafikiri. Mungu tu akuzidishieee.
Mtja kamkazia macho Iqra, Iqra anaangalia chini, anamchungulia kwa jicho pembe. Kila akimchungulia anamkuta anamuangalia. afu kamtulizia mijicho. Akaishiwa nguvu na pozi asijue aseme nini, maana yeye sio mnafiki kama wenzie ambao bendera fata upepo dakika hii wanaongea hili, dakika hii wanaongea lile.Kiukweli lilimshukaaa, na aibu ikawa imemtawala.
Mteja akadakia wewe Mwarabu bado kiburiii si ndiooo. Haya. Akaanza kutoka nje. Iqra akajizoa zoa akasema Asante kwa sauti kubwaaa. Yule mteja hata hakujibu akaondoka zake kimya kimyaaa.
ITAENDELEA SAA 5 USIKU.
Babu Ally akamjibu