Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Weekend Story: You Can't Handle The Truth

Shall I handle the truth? I don't know. And at this point I'm too afraid to ask or guess.

Mimi napingana na suala la Walter kumla Iqra kwa nguvu zote. Mnataka kuniambia siku Walter anaenda kushinda dukani Collins na Caren walikuwa wapi? Doesn't make sense kabisa....yani Collins didn't fight for his love, backed by his sister? Why did Walter get to her first?

All the odds za kuwa na Iqra fall to Collins. But once again, can I handle the truth?

Thank you, lara 1

Kumbuka Carina alikuwa kwa mamake mkubwa akaambiwa akae huko mpaka afatwe. Collins alikuwa anamsubiria Iqra arudi nyumbani mpaka saa 10 asubuhi hakurudi wala nini. Iqra alikuwa dukani wakati Walter tangu ile ya usiku alikuwa kila siku lazima aende dukani kumngoja na akawa haji sababu Iqra alikuwa busy na kina Collins. Siku alipovurugana na collins akaenda dukani, ndo Walter akamchukua wakatembeeee, na ndo hakurudi nyumbani siku hio wakalaa hoteli wakati Collins kakesha mlangoni akimsubiri.

ODDS ARE WALTER GOT LUCKY WASWAHILI TUNASEMA MBINGU ZILIGEUKA.
 
Usishangae ukaambiwa Walter na Inspector wanashea baba na mama. Iqra akapata mimba ya Walter. Grace akaliwa na Collins. Muddy hana chake.

HAHAHAAAAAAAAA! NAONA WATU MMEANZA KUJI OVERDOSE SIO KWA TITTLE HILO NA SURPRISE MNAZOZIPATA KILA STORY IKIENDELEAAA. ANYTHING IS POSSIBLE IN THIS STORY
 
jaman roho imeuma! malaya walter kapata mechi ya kirafiki kiulainiiii! duuuu
 
jaman roho imeuma! malaya walter kapata mechi ya kirafiki kiulainiiii! duuuu
Katoto kalikua na stress kale, kakiendelea hivyo nadhan utakua ndio mwanzo kwa wandewa wa karibu nae kupata show za kirafiki
 
Leo weekend tupia moja ya mchana tupotezee swaumu maana kali sana leo daku Nimechelewa kula
 
Itabidi nianze kuwinda waliotendwa, ukimpata anatoa ushirikiano wa kufa mtu kwa kujifariji na kujiliwaza. "I repair the broken hearts "
 
Acha ufala (joke) jikaze mtoto wa kiume usiwe kama mvulana

penda story sio author....au unafikiria huyo lara nae ni mzuri kama Iqra? kwa taarifa yako hana tofauti na dakta kul.
Hahaa Me nampenda tuu.
Nimekua induced na story zakee
 
h


Hahahaaaa! Na ubaradhuli wote Walter alioufanya mpaka kumpaka mtu pili pili kumbaka Grace bado mko TEAM WALTER. Wanaume mwalimu wenu kipofu. Hands down.

aaaah aaaaah !! jamaa kaamua chenji basi ni kweli amechenji, so kawa. real man now, na Kumbuka Real Man always eat beautiful girls with beautiful heart.
 
COLLINS 4 YEARS LATER.

Ilikuwa siku yake ya kupewa nyota ya 2 jeshini Collins na baba yake Mzee Mujungu alikuwa na furahaa sanaa hususani juu ya mwanae kujiunga na jeshi na kufata family legacy yao. Kuanzia babu mpaka mjukuuuu wote ni watumishi wa taifa hili kwa upande wa majeshi. Mujungu ambae afya yake mda huo haikuwa nzuri sanaa kutokana na matatizo ya kibofu yaliyomlazimu kwenda nje mara kwa mara kutibiwa alifurahi sanaa, na kwa jinsi Collins alivokuwa anaenda haraka jeshini akajua kitu kilichowashinda yeye na baba yake na babu yake kufika level za MKUU WA MAJESHI GENERAL inaweza kufikiwa na Collins. Na yeye anaweza kustaafu kwa amani tu na furaha teleee.

Akumbuka babu yake alivopigana vita vya 1 ya kwanza ya dunia chini ya mjerumani akiwa mvulana mdogo tu wa miaka 19. Kutokana na umahiri wake wa kivita kwenye vita vya jadi, na ushujaa wake mkubwa wa kutosita sita wala kubabaika akiwa na mika hio 19 alishaua watu 20 vitani mpaka wazee wakawa wanamuogopaa kwa ujasiri wake na mtemi kumuozesha binti yake ambae alikuwa mkubwa kwa babu yake akafatwa na mjerumani kuhitajika kwenda kupigana vita kwaniaba ya mjerumani huko ughaibuni.

Kiukweli wajerumani wenywe walimkubali maana hakutakiwa training nyingi sanaa, pamoja na kutokwenda shule alikuwa mahiri sanaa na mwenye IQ kubwa. Aliona mjerumani akitumi bunduki mara moja tu na yeye akaitumia bila kuelekezwa kwa kufata tu alichokiona. Kadri walivokuwa wanaenda nae vitani wakazidi kumkubali ni kichwa kutokana na IQ yake kubwa kama kupenda kutumia mitegooo ya jadi zaidi kuliko direct combat ilio wawezesha kuua watu wengi kwa mkupuo na kuchukua ushindi. Sehemu zote alizo pambanakwa niaba ya wajerumani walishinda kwa kishindo. Kama kuna kambi walienda ilikuwa ghala kubwa ya silaha ya waingereza na kulikuwa na wanajeshi wengi sanaa. Kamanda wa kikosi chake akawa anapata shaka sanaa juu ya kuiteka hio campa, Ndo siku bila kutarajia Mujugu akamuita kamanda maanake lugha ilikuwa bado hajaijua vizuri wanaongea zaidi kwa vitendo, akamchore picha ya kambi iliozungukwa na nyasi kavu sanaa akamchorea mshale mtu anaziwasha zile nyasi na kambi itawaka yote maana upepo unaelekea kule. Afu akamchorea watu watakuwa wanakimbia nje na huku akamchorea wanajeshi wana silaha upande wao sasa watawamalizia wale watu hapo hapo maana watakuwa hawajajipanga. Kamamnda akamkubali Mujungu ndi kiboko yaooo. Kweli walipoiteka ile kambi Mujungu akawa officer wa level za juu sanaa kwa mtu mweusi kuwahi kushika cheo hiko akiwa hajui kijerumani.

Vita iliisha kwa mjerumani kupotezaa vibayaa, na Kamanda wake akamualika Mujungu asirudi Tanzania bali waende wote ujerumani kujipanga upyaa. Wakamuhakikishia kazi nzuri sanaa jijini Berlin ndani ya jeshi na mambo mengi sanaaa mazuriii ya kupendeza. Alitafuwa hadi mkalimani wa kumshawishi aende ujerumani na kulitumika jeshi la Ujerumani asirudi Tanzania. Mujungu akakataa aksema yeye hajui kijerumani, hataki kujua kijerumani maana akijifunza lugha ya Mzungu mizimu ya kwao itamlaani. Hakufa ugenini, wala hata vita ingeendelea miaka 70 asingekufa ardhi ya ugenini sababu kabla ya kuja vitani alikunywa dawa ya kienyeji inayomzuia kufia sehemu yoyote ile kasoro kwao Musoma. Na mizimu ya kwao itachukia akienda ujerumani, yeye anachoomba arudishwe kwao Musoma akake na mkewe na kuendela kufuga ngombe na kumtumikia mkwe wake Chieff. Wajerumani kwa heshima wakamrudisha mpaka Nairobi na kumtafutia usafiri mpaka Msoma.


Akiwa msoma akafatwa tenaa na Mwingereza kwenda kufungwa jela kwa kosa la kupambana upande wa mjerumani, alihukumiwa mahakama ya kivita kwa makosa ya kivita, akaletwa Dareslaam kutumikia kifungo. Akiwa jela alikuwa mtu wa amani sanaa, mwenye kupenda kufanya mazoezi na anae ogopewa na wafungwa wooote. Iliwahi kutoke fujo gerezani wazungu walishindwa kuamulia, ila mzee Mujungu mda huo bado kijana aliekuwa kalala alipotoka akasema nimesema wote mkalale fujoliliishia hapo. Tangu hapo uongozi wa mwingereza ukamtambua na kuanza mahojiano nae yaliyopelekea gereza kuwa na amani sanaa kwa vitu alivo washauri.

Akapewa msamaha wa Malkia na kuachiwa huru ila akitakiwa kulitumikia jeshi la Mwingereza kama askari Kea akimtumikia Govener wa enzi hizo. Akatumikia kwa ustadi mkubwa sanaa, mpaka vita vya pili vya dunia akaenda tena vitani chini ya serikali ya Mwingereza safari. Na akatumikia kwa ustadi mkubwa sanaa. Alivorudi akaongezewa vyeo na kuwa moja watu wa kwanza weusi kushika nafasi za juu jeshi la Mwingereza.

Akiwa moja wa ofisa wa juu siku alikuwa musomaa, mtemi mpyaa ambae ni mtoto wa shemeji yake akamkutanisha na Hayati baba wa Taifa JK Nyerere mtemi mwenzie na kuzungumza nae juu ya ufirauni wa wakoloni. Mda huo Nyerere ndo anafundisha Pugu sekondari ndo akamtaarifu juu ya harakati alizozikuta zimeanzishwa na madreva tax wa posta kina Hayati Mfaume Kawawa na kumtaka Mujungu aingie kujiunga nae. Mujungu akakataa kwamba yeye umri ushampitaaa sanaa kwanza anastaafu mwaka unaofata, afu hakusoma na pia mwili ushakataaa alichobakiza ni kuja Musoma kuishi na mkewe na kungoja kufa, ila atawapa mwanae Mjungu Jr wa kwanza amabe ni kijana mwenzao anaendana nao, na kasi yake itawafaa sanaa. Yeye kama yeye anasapoti nchi ikombolewe ila ule ufanisi wa kushiriki huo ukombozi ndo hanaa. Akawakutanisha na Mjungu Jr hapa DSM mwaka 1950 na mwaka 1954 Mjungu Sr alifariki huko Musoma na kuzikwa huko huko Musoma ambapo TANU yote ilienda kumzika.

Mjungu jr ndo aba yake sasa Mjungu na alishiriki harakati za TANU kikamilifuuumpaka uhuru kupatikanaa na baada ya uhuru alikuwa mmoja wa wanajeshi wa kwanza wa jeshi la Tanzania akitokea Jeshi la Mwingereza. Na alipata vyeo vikubwa vikubwa jeshini na alikuwa karibu sanaa na mwalimu Nyere mpaka yeye Mjungu alikuwa akimfahamu Mwalimu kiasi cha kukutana nae barabarani na kuulizwa Hujambo? Baba anaendleaje. Mjungu yeye nae kamam Collins hakuta kuingia jeshini ila hakujua afanye nini kingine maana baba alikuwa mwanajeshi na jeshi ndo kitu peke alichokijua akilini mwake.

Akakumbuka Collins alivokuwa hataki kuingi jeshini, na alishakata tamaa kabisaa Collins kuwa mwanajeshi, tofauti yake na collins mwanae alikuwa kichwa na amekaa sanaa nje akajua tu hatokosa namna ya kuishi vizuri kuliko hata ma officer wa jeshi na akawa asharidhia kuwa ile kizazi choa cha jeshi kifikie mwisho alichoshangaaa ni kurudi toka India juzi juzi na kumkuta Collins amesha ji enroll jeshini, bila msaada wake na anafanya vizuri kabisaa on his own. Furaha yake haikupimikaaa. Na siku hio ndani ya miaka 4 tu keshapata nyot 2 akajua tu Collins lazima aje awe GENERAL. Akawa anatabasamu tu siku nzimaa. Kwake afya ilimlazimu kuahcha ulevi na kusababisha awe bored mda mwingi ila siku hio alikuwa na furaha sanaa.

Koku alikuwa na furaha sanaa kwa Collins kufikia level zile, his little boy had grown so much. Na alifurahi zaidi manake Collins ni kichwa sanaaaa, na ndo maana hata alipanda haraka jeshiniii. Akawa all happy and smiles siku hio ya party. Na kilichomshangaza zaidiii ni kitendo cha GENERAL kupiga simu kwa Mujungu kulalamika kutoalikwa kwenye hio party yao. Mujungu akajitetea sanaaa, Koku akafurahi tu mashoga zake watamkomajeee Generali kaja in person kwenye party ya Collins hajatuma hata mjumbe.

Carina akamzindua mama yake, mom mbona kama tumbo linaniumaa umaaa. Koku akamgeukia Carina amabe alikuwa mjamzitooo wa miezi tisaa, kachokaaa kabisaaa akamwambia jikaze tu mwanangu ndo mwishoni mwa safari hivooo. Jikaze leo kaka yako amepata achievement kubwa sanaa. Unakaribia kuitwa mama na wewe inbidi ujikaze you are not my little girl anymore. Aaaaaaaaaaaaaaaw mya Carinaaa. Akamkumbatia na kuanza kulichezea tumbo la Carina. Carina analaamika mbona kina Imma hawajaja bado mpaka mda huu? Imma is so irresponsible. Koku akajua mimba hio inamtia visirani visivokuwa na maana. Akaamua kumtetea mkwe wake, Carrina kuwa mvumilivu, Imma nae ni mtoto mdogo sio mkubwa kama unavodhania. Watakujaa, wazazi wake ni watu wazuri watakuja wote everything will be okay. Ngoja nikuletee juice mwanangu.

Collins alikuwa dirishani akitafakari, alitakiwa awe na furahaa sanaa siku hio manake mipango yake na malengo yake yote jeshini yalikuwa yanatimia kama alivopenda yeye. Tatizo hakuwa na furaha yoyote moyoni kiukweliii. Kila akijitahidi kumsahau Iqra anajikuta haweziiii. Kesha mtafuta sanaaa sanaaa na hakufanikiwa kujua alipo. Mpaka amejiunga jeshini ili atumie vifaa na mtandao wa kijeshi kumtafuta ambavyo amekuwa anavitumia miaka 4 iliopita bado alikuwa gizani kujua Iqra yuko wapi na anafanya nini.

Ukizingatia kuachana kwao hakukuwa kwa faraja wala raha yoyote ndo kilichomuumiza zaidi yeye. Amehangaik sanaa na kwa taarifa alizokuwa nazozilionesha kwa namna yoyote IQRA ITAKUWA MIKONONI MWA WALTER. Manake baada ya kutorudi kwao siku ile, katika upelezi wake alioufanya kwa kinaaa sanaa akajua mara ya mwisho mchana wa jana yake Iqra alionekena akiwa na Walter dukani amabapo walionekana tena woote usiku Club na wakaonekana tena wote mara ya mwisho wakiwa hotelini pamoja walipolala wote.

Baada ya hapo wote wakampoteaaa kwenye radar, sio Iqra sio Walter. Baada ya kumtafuta sanaa sanaa Iqra na kutumia nafasi zake jeshini, na kuwa amepata hela nyingi sanaa baada ya kuanza kuwaagizia ma boss wa jeshi magari makali ya uingereza na ujerumani, kwa connection zake kwa Mkuu wa upelezi nchini akaweza ku extend operation yake ya kumsaka Iqra nchi za kenya na Uganda. Kwa pesa aliyoiwekezaa na kuimwaga nchi hizo 2 akaambulia tu taarifa kwamba Passsport ya msichana alie itwa Iqra Idriss Mselem ilionwa na askari mmoja kwenye mpaka wa Somalia na Kenya. Kwa maelezo ya huyo askari msichana huyo alivuka mpaka huo kulekea Somalia mnamo mwaka uleule Iqra aliopoteaaa.

Collins akaongeza helaaa, huyo akari atafutwe na akutanishwe nae, pamoja na jitihada zote ikaonekana askari huyo alisha fariki mda mfupi baada ya kutoa taarifa hizo kwamba kweli amewahi kumuona huyo binti, na anakumbuka sanaa tukio hilo sababu binti alikuwa kavaaa nikab kwenye hilo lori, na kilichomfanya amkahue binti alikuwa analia sanaa na alionekana yuko peke yake. Akamshusha akamvua nikab kwa umri ulimtishaaa maana alikuwa mdogo sanaa, na kumbana akasema anaenda Somalia kumtafuta baba yake aliekuwa huko kwa biashara na amepewa taarifa kuwa baba yake alipata matatizo huko, na kapewa taarifa yuko hospitali mda huo hana msaada wowote. Askari anasema kiukweli alimpenda yule msichana saana ila hali aliyokuwa nayo haikuwa elekezi.

Akaamua tu kumkagua passport yake, ndo kuona jina lake hilo Iqra Idriss Mselem, raia wa Tanzaniaaa. Na passport yake ilikuw na mihuri ya London na Oman kitu kilicho mkmvise yule askari kwamba kweli binti atakuwa familia yenye uzwezo tu na anaenda kumtafuta baba yake, maana waarabu wana tamaa saana labda alienda kwenye dili ya kupeleka mahindi ya UN kwenye balaa la njaa afu akapotela huko. Akamuachia na kuruhusu lile lori kuvuka mpaka.


Collins taarifa ile ikamuaminisha moja kwa moja kwamba mshenzi Walter ndo amemtoreshea Iqra Somalia. Akakwazika tu of all countries kwanini aende Somalia. Akawaza labda Walter alikula dili la Un kwenda kulinda wafanyakazi wa UN ila alimtrack sanaaa na hakukuwa na trace za mtu huyo Walter katika wanajeshi wote waliowahi kutokea Tanzania.

Maduka ya kina Iqra kuja kufunguliwa yakawa yamenunuliwa na watu wengine ambao wafanyakazi wote wakawa ni wapya, akajaribu kuwatafuta wa zamani hakuwai kuwapata. Akawa amefikia dead end kabisaa na akawaza Walter atakuwa na Iqra huko Somalia na labda washazaa hata mtoto na huyo mtoto atakuwa tu mkubwaaa. Akafuta chozi, na kurudi kwenye sherehe.

Akiwa bored na zoezi zima la party kama Mungu tu akamuona Grace na Muddy wakiwa na watoto wao 2. Akamfata Grace na katika story story akamuuliza kama washaoana na Muddy akasema badooo, ila wanaishi wote kikubwa ni dini yeye Grace hataki kutiwa maji ili kuslimu na kuolewa na Muddy ila technically ni kama wameoana tu maana wanaishi wote na watoto wawili.

Collins akachomekea swali la kizushi tu Eti Grace unaweza kujua au kuniuliza kwa Muddy Walter yuko Somalia sehemu gani na anafanya nini manake nina shida sanaa kuna deal za UN nataka kuongea nae. Grace akastukaaaaaaaa! Walter yuko Somaliaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!! Mbona mi Walter nimemuonaaa juzi tu hapaa au kaenda jana huko Somalia????????. Collins yuko ni juzi tuu hapa miaka mi 4 sio mingi kwa kweli. Grace akazidi kupata mshangao, Walter yuko Somalia miak mi 4??????????? Inawezekana lakini maana kwa miaka hio mi 4 nimemuona kama mara 3 tu na moja yapo ikiwa Juzi hapaa kuamkia jana alikuwa akitokea Dodoma. Collins akastukaaaaa! Ina maana unataka kuniambia inawezekana Walter yuko nchini mda huu? Grace akamwambia mi nimemuona juzi hapo kama huamini akaita Muddy njoo Baba Raul.

Muddy akaja karibu wakasalimiana na Collins, Grace akamuuliza eti Walter yuko Somalia siku hizi? Muddy akasema mi sifahamu hajaniambiaaa kabisaa, inawezekana maaana juzi ile alivopita pale nyumbani aliniuliza kama naweza kujua wewe Collins Somalia unaishi wapi na uanendaga sehemu gani specific unayofikia. Nikamjibu tu mimi siwezi kujuaa sababu hatujazoeana kiasi hiko. Collins akastukaaa sanaaaaa, akajua Walter kashajua anamtafuta sasa anataka kumuua kabla hajawapata na kweli atakuwa na Iqra, na atakuwa anajua anawatafuta.

Akili ikafanya kazi haraka sanaa, atawezaje kumpata Walter haraka kabla Walter hajampata yeye. Akamuita Muddy pembeni na kumwambia shemeji mbona humtii dada etu maji ukamuoa? Utazini mpaka lini? Mkazie mwambie kama hataki ku slim unaoa mke wmingine. Ramadhan zote unazini, watoto wote wa 2 wana haram utaishi hivi mpaka lini? Mimi mwanaume mwenzio kina niuma sanaa.

Muddy akashukuru Collins kajua matatizo yake, wacha ajielezeee kwa kina hio hali inavomuumiza. Collins akamwambia ita harudi haraka sanaa, mi nitakusaidia kushawishi ndani ya familia. Muddy anamsimulia Walter mwenyewe alinishauri hiko kitu juziiii. Alinishauri sanaa. Na mimi nakubaliana na nyie nipeni mwezi tu nawahakikishia huyu mwanamke namtia maji na namuoaaaa. Ngojeniiii. Collins yuko sawasawa shemeji nakuamini hutoniangushaaa.

The rest of the party was boring kwa Collins cause hela alizopata jeshini ni ndogo sanaa ukilinganisha na hela alizopata kwenye mambo yake ya magari na deal zake zingine. Alijua kutafuta pesaaa. Wakasherekeaaa, shughuli ikafana, rafiki yake General alikuja in person kumpongeza na kumuahidi atamkumbuka kwenye ufalme wake, na kuongea ane mpango wake wa kuagiza Yatch kali sanaa maana ni member wa DSM yatch club.

Kesho Collins akajaribu kumtrack Walter kwa wiki hio bandarini na airport kama amevuka border na amevukia wapi kwenda wapi hakupata kujua ikawa inawezekana Walter hajavuka border yuko nchini au atakuwa Walter ni kikosi maalumu anatumia Black Passport ambayo ni untrackable. Akajua tu harusi ya Muddy lazima na lazimaa Walter atakuja na ndo atampatia hapo. Akaendela kumsumbua Muddy kuhusu harusiii.

Muddy akafanikisha Grace akakubali kuslimu na harusi ikawa tayari Dodoma. Collins alienda Dodoma siku 3 kabla na kujaribu kumrack Walter kimya kimya bila mafanikio. Akajuia tu Walter lazima atakuja na Iqra kwenye hio sherehe pia ua, na ndo hapo atakapo ondoka na Iqra iwe isiwe.

Jioni kwenye harusi kweli akamuona Walter, kabla Walter hajamuona yeye, na alivomuona Walter alikuwa anahangaika kujificha huku akijitahidi kumtafuta mtu, akajua tu anamtafuta yeye. Iqra hakuwepo mahali hapo wala dalili za yeye kuwepo hazikuwepo. Akajiambia bahati yako umestukaaa hujaja na Iqra ila by the time i am done with you utaenda kuonesha Iqra alipoo mwenye bila wasiwasi.

Akamfata akamgusa bega, Walter kugeuka Collins huyu hapa, na ndo alikuwa anamsaka, sasa kugunduka Collins ashamuona kabla yake, ashamfikia na ndo kamgus abega akafa gazni kwanza kwa mshangao.

ITAENDELEA BAADA YA FTARI
 
Kumbuka Carina alikuwa kwa mamake mkubwa akaambiwa akae huko mpaka afatwe. Collins alikuwa anamsubiria Iqra arudi nyumbani mpaka saa 10 asubuhi hakurudi wala nini. Iqra alikuwa dukani wakati Walter tangu ile ya usiku alikuwa kila siku lazima aende dukani kumngoja na akawa haji sababu Iqra alikuwa busy na kina Collins. Siku alipovurugana na collins akaenda dukani, ndo Walter akamchukua wakatembeeee, na ndo hakurudi nyumbani siku hio wakalaa hoteli wakati Collins kakesha mlangoni akimsubiri.

ODDS ARE WALTER GOT LUCKY WASWAHILI TUNASEMA MBINGU ZILIGEUKA.

Mama unatupa dawa sasa....
 
Pamoja na kuzaliwa ughaibuni, elimu bora, maisha safi, pesa kibao na maadili mema.....vyeo kedekede na connections lukuki na interejensia ya kutosha plus read handed (sijui nimepatia yai)

Walter is still my favorite - atachomoka tu "Walter The Great"
 
kudadeki mtoto iqra kawapotea wote!!! hii kitu zaid ya isidingo aiseee........ ngoja tuone walter vs collins
 
Noooooo pls jamani Lara isiwe hivi!
Nakuomba sana usibadili gia angani.
Iwe tu kama ilivyo
Walter Inspector
Collins Iqra
Muddy Grace
Nitaumia mno ikiwa tofauti na hivi.
Sitaki kabisa kumsikia Firaun Walter yuko na Iqra.

You can't handle the truth remember.
 
Back
Top Bottom