WALTER!
Akiwa ameenda kwenye sherehe ya Muddy na Grace kikubwa kilichompeleka pale ni uhakiak kwamba Collins atakuwepo pale. Kukweli bado alikuwa na kijiba kitendo cha Collins kumtorosha Iqra tena chini ya pua zake kilimuuma sanaa sanaaa. Miaka 4 imepita na hakuna siku alioacha kumfikiria na kumkumbukaaa. Lengo haswa lilikuwa akimuona Collins hapo atafute namna ya kumteka na kumtesa mpaka aseme ukweli wapi alipo Iqra.
Amekuwa akimfatilia sanaa sanaa Collins ila akashindwa kungamua moja kwa moja Iqra atakuwa kafichwa wapi na Collins ukizingatia kwamba Collins anaenda nchi nyingiii sanaaa. Sasa katika hizo nchi ameshindwa kabisaa kungamua ni ipi. Katika peleza peleza yake akisaidiwa na mzazi mwenzie Inspector Jane, baba yake Jane tena alipata habari za kintelijensia kuwa Collins anamtafuta Iqra na kwamba passport ya Iqra mwishoni kabisaa ilionekana Somalia akivuka mpaka wa Kenya.
Akajua tu Collins ni mshenzi na anataka kumpoteza yeye maboyaa, hamna zaidi ya hapo. Yote hio alilenga kum mislead yeye Walter, iweje habari zimfikie baba mkwe wake, mzazi wa mzazi mwenzie. Iweje zije kumrudia yeye. Akajua tu Collins ashachunguza kajua amezaa na Janet kwa hio akafanya manuvaa manuvaaa hizo habari zimfikie ila yeye Walter ashindwe kumpata Iqra.
Kuja kushtuka ndo Collins kamgusa begaaa, hapo harusini akajua tayariii. Akamuwahi Collins tutoke nje. Collins akakubali. Wamefika nje wakajikuta kila mtu anamrushia mwenzie ngumi za mawe. Wamepiganaaa, wamepiganaaa, wamepignaaa. Akija kuamlia mtu anapigwa yeye. Na wote wajedaaa, wanajiwezaa. Watu wakaa pembeni kutizama show ya bure.
Katika kupigana kila mmoja anamtuhumu mwenzie sema Iqra yuko wapi? Umemficha wapi? !wenzie anamgeuzia kibao wewe ndo useme kabla sijakuua. Wamepiganaa mpaka wakawa nyanga nyangaaa waklala pale pale chini hamna mwenye nguvu ya kujisogezaa. Watu wakawachoka wakendelea na harusi. Naadae Walter akapata nguvu akajinyanyua na kuondoka eneo la tukio.
Collins akaja kuzolewaa, akalala wiki nzima hotelini ndo akapata nguvu za kurudi DSM kiendelea na kazi yake. Walter aliumwa wiki nzima mwili haujiwezi kabisaaa. Kuna jambo likaanza kimsimbua kichwa upyaaa kama Iqra hayupo na Collins atakuwa wapi? Alipotelea wapi? Wazo huenda ameshafariki likamtishaa sanaaa, akajikuta anaogopa mwenyewe. Akakumbuka alionekana anaenda Somalia, akawaza na nani? Kufanya nini? Kwanini wakati yeye alikuwa tayari kuishi nae, kimtake care mpaka siki angekufa. Kwanini Iqra hakumuaminiii?
Kwanini mwanamke mmoja tu ametokea kumpendamaishani mwake na mwanamke huyo ndo kampotea mazingira kama yale. Kwanini dunia inamdhulumu nafsi. Kwanini maisha ni magumu sanaaa. Akawazaa au kwa sababu yeye ni mtu mmbaya? Akawaza hapana mbona wazazi wake Dodoma anawajali sanaa kwa kila kitu, anawatembelea sanaa, na anapendana sanaa nao. Akawaza au sababu ya mambo alioganya alivokiwa mvulana ndo dunia imeamua kumuadhibuuu bila hurumaaa. Akasononeka kama angeweza kurudi nyuma ku undo yote aliofanya mradi tu awe na Iqra angerudi nyumaaa.
Akamkumbuka baba yake mzazi na mama yake mzazi, akawaza au labda vile alivowatupaa jumlaa ndo wamemlaani ndo maana anahangaika tu, hela anayo, connection anazo ila hana raha. Akakumbuka baba yake alivomwambia asirudi tenaa kwao, akawaza na kwanini mjomba wake Jiles hakuwahi kumgusia juu ya hao watu au hata kumwambia aende akasalimie.
Akawazaa sanaa, sijui watakuwa na hali gani, au ndo maana mambo mabaya mabaya yanamkumba hana radhi ua wazazi wake. Akawaza kama aliuzwa kwa mbuzi basi sahivi hela anayo wakamlipe huyo mbuzi, watengeneza mambo kimila na yeye kuwaangukia wazazi wake labda dunia itamsamehe na mbingu zitamchekeaaa upya. Akakosa usingizi kabisaaa.
Asubuhi akapanda basi la Arusha, akaenda mpaka kwao kabisaa. Akahisi kutetemeka mwili kabisaa na kukosa nguvu za kwenda kwao. Akaamua aende kustua kilabuni kwanza hata na bia mbili zimpe ujasiri. Alivofika kilabuni akasikia sauti anayoijuaa kabisaa, ni miaka mingi ila hio sauti haiwezi kumpoteaaa kabisaa akilini mwake, baba yake Mzazi. Akaka kwanza chini kwa mshtuko na kumsikiliza.
Akaja muhudumu nikupe nini kaka, akamwambia Casttle light! Muhudumu akasema hapa hatuuzi hizo kuna Safari tu. Walter akamwambia niletee 3. Akamsikia baba yake anasema mnasema mimi sijazaa, sina uzaziiiii hahaaaa mnachekesha sanaaa, mimi nina mtoto, dumeee anaitwa Walter ninulieni pombe niwasimulie. Walevi wengine wakamsonya tu kimya kimya.
Walter akamuita mhudumu akamwambia mpe safari 5 yule mzee. Usimwambie zimetoka huku, nataka kusikia hio story. Mdada akenda kwa chapombe akamwambia safari hii hapa leo nimefurahi nataka kusikia ukiwaburudisha wateja wangu, eeeeh aya simulia una mtoto dume anaitwa Walter yuko wapi sasa? Mbona unahangaika unaomba omba pombe za bure? Walter kusikia yale maneno moyo ukampasukaa haswaa liboona mzazi wake anapiga magoti kushukuru safari moja aliopewa na yule dada. Akajisemea ndo maana nilikiwa nimelaanika mimi, kumbe mzazi wangu anaishi kama mbwa huku. Akajikaza kusikia hio story.
Mzee cha pombe akaendelea, mwanangu nimemuuza ukoo, hela yote nikalewea pombe. Pombe kweli shetaniii, tena mlenye pembe sabaaa. Katika makosa niliyowahi kufanya ni kumuuza yule mtoto. Hakuna kitu nilichokipenda maishani mwangu kama yule mtoto, nawaambia. Siku anazaliwa naikumbuka kama jana. Na siku anaondoka kwenda Dodoma naikumbuka kama jana. Ni mda sanaa! Mwaka 1982 ndo alienda Dodoma. Sijui yuko wapi au anafanya nini.
Hakuna kitu nayoilaumu pombe kama maamuzi yangu ya kumuuza yule mtoto. Kila siku lazima nijute hilo swalaaa. Nilimuuza kwa nia njema apate ukoo mzuri awe na maisha mazuri ila ngombe wa maskini hazi ngooooo na akizaa anazaa dume, taarifa ya mwisho kupata yule mtoto shule kafeliiii, kawa mipombe kama mimi baba yake mzazi na tena kawa kijeba huko Dodoma apiga watu tu. Mxiuuuuuu. Angekaa na mimi ningemnyooshaaa asingeishia vile. Sema vile mjomba wake mtaratibu sanaa, hana mkono wa kupigaaa ndo kisa cha yote hayo. Lakini namuchia Munguuu. Namuombea Mungu siku zote. Mkiona nimeingia kanisani ujue naenda kumuombea yule mtoto.
Walter akajikuta ana machozi. Akaondoka pale kwenda mpaka kwao. Akakuta wanaishi vile vile, tena mama yake ndo kachooka kaishaaa. Amezidi kuchakaaa. Akaingia ndani akawa amekaa kimya. Mama mtu akamkaribisha asijue ni Walter, akajua tu labda mtu wa svikoba alipo kopa sasa amepitisha rejesho. Akaanza kumsimulia mwanagu mnivumilie naumwaa mie, naumwa sanaaa, ila pesa zenu nitarejeshaaa.
Walter akaendelea kuwa amekaa kimyaa. Yule mama akajielezaa akamaliza akawa anamsikizia Walter. Ghafla akamwambia nina mwanangu angekuwa kama wewe kijana, rika lako kabisaaa, anaitwa Walter sema maisha tu yupo hiko mbaliii sanaaa. Walter akaanza kulia. Ile sauti sasa maana kilio cha kwikwi Mama yake akastuka na kusema Walter baba umerudiiiii. Asante yesuuuuuu. Akamkumbatiaaa. Baadae wakawa wanlia wote. Baadae wakawa wanakaa wanaangalina tu.
Baadae mama akamuuliza Walter ulienda wapi, nilikutafuta sanaaa. Walter akamsimuliaaa, mama akapanic yani baba yako mshenzi sanaa, nimeumia miaka yote najua umekufa au sijui uko wapi kwanini asi iambie uko kwa Jiles? Jilesi na baba yako sitokuja kuwasamehe mpaka nakufaaa sio kwa kunitenganisha na wewe, siwezi kiwasemehe.
Walter anamueleza ni kwa nia nzuri na mjomba alikaa na mimi vizuri tu. Mama hataki kusikia nini wala nini. Walter akajua Mzee cha pombe akirudi hiko leooo analoo.wakabakia tu kimyaaa. Mzee cha pombe akarudi hajalewa sanaa wala nini. Safari 5 kwake ni dozi ya kawaida sanaa. Kuingia kukuta wamekaa kkmyaa wanaangalian akasema tu Walter! Wakamuangalia wote, nae akaa kimya. Tofauti na Walter alivotarajia mama kwa cha pombe hakuleta fujo wala nini. Zaidi aliwatengea msosi, wakala. Msosi duni sanaa. Walter akaendela kuwaza ndo maana nalaanika mjinj, kumbe wazazi wangu ndo wanaishi hivi.
Baada ya kula wakawa wamekaa wote kimyaa. Baba akauliza Walter siku hizi unafanya nini? Nilisikia shule umefeli na upo mjini unafanya fujo? Mama akadakia usimseme mtoto mbaya hata kama hafanyi kitu, wewe baba yake unafanya nini? Walter akajibu nimeajitiwa srikalini. Wakangaliana baba na mama. Mzee cha pombe akachekaa, akasema Jiles alihongaa serikali ikakuajiri, hahaaaaaaa, shemeji yangu yule hatari sanaaa. Bila vigezo amekuingiza serikalini, yule mwanangu ndo baba yako. Walter akaa kimya akaona ayaachie hapo.
Akamwambia Walter twende tukanyooshe miguuu, mam akamwambia cha pombe sasa hela ya kuku si kuna mgenii? Chapombe akajikunguta mifuko akaona hamna kitu. Walter akatoa noti za kutosha haraka haraka, cha pombe anajikosha mwanetu huyo kawa afsa wa serikali. Mkewe akapokea zile hela wakaenda ipande tofauti na kilabuni. Akamuuliza mzee leo hupati? Chapombe akasema leo sitaki kupata nataka tuongeee nikiwa kamili kuna mambo ya msingi nagaka nikwambie.
Wakaenda kama shambani hivi wakawa wamekaa juu ya mawe. Akamuiliza Walter una familia? Umeoa tayari au? Walter akasema nin mtoto mmoja kuna mtu nimezaa nae ila hatujaoana bado na sina lengo la kumuoa. Chapombe akamuuliza kwa hio umemtelekeza yule mtoto si ndio? Walter akaa kimya. Chapombe akamfokea kamtafute huyo mwanamke na umuoe ulee yule mtoto.
Walter akapanic sio kwa kuingiliwa kwenye masuala yake na Iqra. Akaanza kumsimulia Chapombe kuhusu iqra na alivokuwa anamtafuta miaka yote bila mafanikio na jinsi alivompa moyo wake akiwa hana nia ya kubadili mawazo, mtoto ilitokea tuuu. Chapombe akamsikilizaa, akamwambia lazima umuoe huyo mama watoto kuvunja laana ya ukoo. Walter akastukaa kuvunja laana ya ukoo kivipi?
Chapombe akamwambia yeye sio baba yake mzazi kama anvofikiri, yeye alikuwa tu mwalimu wa mama yake anafundisha hapo kijijini na alipata ajali ya baiskeli ikamjeruhi uume wake kutokana na tiba hafifu akawa ha function kabisaaa. Alivopoteza uwezo wa kujaamian akawa mlevi tu na kutunza siri yake. Sasa mama yake alipewa mimba akiwa shule akafukuzwa kwao. Yeye akitoka kilabuni usiku wa manane akamkuta njiani anlia, anaohopa anatetemeka. Akamkaribisha kwake. Basi akawa anaishi nae ndo akazaliwa Walter. Watu wakajuaga mimba ilikuwaga yake, baadae akamuoa kanisani harusi kabisaa.
Ulevi ukamshinda kucontrol kabisaa alivooa, manake akawa anaumia mkewe mzuriiii, kampendaa yuko ndani afu hawezi kumfanya kitu. Akawa anamuhamasihsa tafute wanaume wengine mama yake hatakiii. Basi akawa anamshika shika labda kumtizama ila ndo hawezi kumfaidi ile inavotakiwaaa. Basi akawa anpanic anakunywaaaa kujiliwaza.
Mwisho akafukuzwa kazi ya ualimu akawa mlevi tu wa kijiji, akajua mkewe atamuacha maana woga wake uliomfanyaanywe snaaa ni kuwaza iko siku mama yake angechoka maisha yao ya kushikana na kunawana nawana labda angerudi asingemkuta akamkuta kaenda kwa mwanaume mwingine au angesikia anatembea na mwanaume mwingine ndo akawa anakunywa kujihamiii. Cha ajabu walaaa hakuwahi kusikia hata tetesi anamsaliti.
Sasa baadae kungamua yule ndo mwanamke wa maisha yake, na yeye ndo ashakuwa levi la kutupwaa, hana maisha ya kumpa ndo kwenda kumpigia magoti Jilesi amuuzie mtoto ili Jiles amsaidie kumpa Walter maisha yoyote. Asipotee kama alivopotea yeye. Uzuri Jilesi alikuwa na shida ya mtoto hivo kakubali.
Kiukweli kabisaa japo hajamzaa ila kila siku anamchukulianyeye kama mwanae wa kumzaa na mkewe ndo mwanamke wa maisha yake. Akamwambia alikuwa na GF kabla ya ajali, alivomueleza kuhusu ajali akamkimbia na ndo alimsababisha aanze kunywa. Kwa hio saa zingine HUWEZI KUMJUA MWANAMKE WA MAISHA YAKO MPAKA BAADAE SANAAA MAISHANI. So anavowaza Walter kwamba Iqra ndo mwanamke wa maisha yake ukute Captain ndo mwanamke wa maisha yake.
Akamtafute mwanae na awe kwenye maisha yake. Amuombe mzazi mwenzie radhi na kuhakikisha mwanae hakui bila baba kwani Mungu alimpendela walter baba yake alimkataa ila akampa baba wa 2 wa hiari waliompenda sanaa. Sasa Mungu anaweza asimpendelee mwanae. Akamwambia asimwambia mama yake kabisaa kama kazaa na mtu na hampendi au katelekeza mtoto ataumia sanaa.
Walter akachokaaaaaa! Wakarudi nyumbani, wakayaongea mengi tu, yakaisha. Akaahidi kuwa atawatunza wazazi wake kuanzia hapo. Wakati anaondoka mama yake alilia akajisemea naona kama sitokuona tenaa sijui. Aliliaaaa. Walter akaondoka na mawazo mengi sanaaa.
Akakumbuka alivomblast Inspector alivompa taarifa ya mimba na kimwambia mimba haitaki atafute wa kumpa. Yeye ana mwanamke anaempenda hata iweje hatoweza kumpenda Inspector. Tangia mtoto azaliwe hajawahi kumuonaaa. Aliletewa tarifa Inspector kazaa hakwendaaa, akaja kumpigia Janet mwenyewe kumtaarifu wamepata mtoto wa kiume, akamjibu kunya kuwa yeye ndo kapata sio wamepata, na huyo mtoto kampa zawadi. Akaja kuambiwa mtoto anabatizwaa akajibu kunyaa. Akaja kuambiwaa mtoto anaumwa mambo ya kimila anatakiwa akamtemee maji kichani, akasema akifa mkishazika mnitaarifu. Mmmmmmmh! Ndo akangamua laana yake inatoka pande nyingiiii. Ataanzia wapi kwenda kudai ubaba wa mtoto kama huyo kwa aliyokwisha yasemaaa na kutendaa. Akawa mdogo kama piriton.
Alivofika dar akaulizia kwa watu wa ofisini Inspector Janet anaishi wapi? Na kama kaolewa au vipi ajue pa kuanzia. Akaambiwa anakaa nyumba za polisi Mikocheni, ana mtoto tu hajaolewa. Akaenda mpaka kule jioni hio hio. Akaulizia akapajuaa. Kufika akamkuta dada wa kazi na mtoto wakamkaribisha ndani. Mtoto anamuita uncle, akamwambia mi sio uncle mi baba yako mzazi. Basi mtoto akanza kuita baba bila hiyanaa. Dada wa kazi akastukaaaa.
Janet anarudi msichana anmkimbilia anamwambia baba Ethan kajaaa. Janet akastukaaa, baba Ethan? Msichanaa ndioo, Ethan alikuwa anmuita uncle akamwambia niite baba. Janet akaongeza hatuaaa mpaka ndani. Akamkuta Walter katuna pale bila hayaaa anacheza na yule mtoto kwa yoite aliomfanyiaaa. Hasira zikamkabaaaa sio kidogooo.
Akamsalia za miaka Walter? Walter hawezi kumuangalia usoni akajibu tu nzuri. Janet anamuuliza umetukumbuka leo eeeh baba. Walter akamtuma msicha wa kazi dukani. Akampigia magoti Inspector na kumwambia hakuna maneno nitayoongea hapa yatasadifu wewe kinisamehe kwa ufirauni niliokufanyiaaa. Naomba msamaha wakooo na kubwa zaidi naomba unipokee tusaidiane kumlea huyu mtoto. Nimekukosea sanaaa.
Janet akaanza kulia sio kwa mambo Walter aliomfanyiaaa jamaniii. Acheni tuuuuu. Walter akaona hio hio ndo chansi yake akajitia kumbembelezaa hapo hapo akaanza kumla mate na hivi mziki wake kaumisss kitambooo. Wakajikuta wanahamia chumbaniii. Kama kawaida akampa dozi nene sanaaa. Balaaaaa mpaka Janet akajikuta tu anamsamehe upyaa na kuanza tena kumpendaa.
Bila haya alivotoka chimbani anamwambia dada nipe mabegi yangu na kuyaingiaza chumbani kwa Janet. Ndo ashakuwa baba mwenye nyumba tenaaa. Kiukweli mtoto wake kumuonaa tu moyo uliyeyukaaa, damu nzito kama maji. Sasa tatizo hampendi Janet kabisaa ila sasa mtoto anampenda sanaa. Akajikuta kachanganyikiwa kabisaaa. Mara kibao kwenye mechi alijikuta anamuita Janet Iqraaa. Sema nini Janet akawa anapotezeaaa. He just got his man back, and his babys dady she was more than happy kiwaza kaitwa Iqra afu mtu mzima kwa hio anaelewa maishaa.
Walter akaka pale kwa Janet kama miezi 6 analishwa na kunya buree na kazi anafanya hatoi hata 100. Baadae kadri anavoishi na Janet na dogo akaanza kumzoea na kumpenda pendaa kw ambali. Akaanza kuhudumia nyumba ananunua mpaka chumvi. Janet akaona kweli maombi yanafanya kazi. Alikiwa na kiwanja akamuandika Ethan. Akamwambia Janet nataka huyu mtoto asome shule ghali sanaa nitakuongezea ada. Janet akawa haamini kama Walter ndo yule yule ama kawa malaika. Akwa mpaka anamfata kazini mda mwingine. Wazazi wake walikuwa Walter hawataki kumsikia kabisaa, ila baada ya mabadiliko chanya wakaanza kuja kwa Janet na kumhesabu Walter kama familia. Janet could never have been any happier.
Akaja kumpeleka Janet kwao Arusha na mtoto, wakapokelewa vizuriii tu. Kidogo Janet ndo aaknza kumjua Walter. Mama yake wa Dodoma akawa anakuja hapo kwa Janet na Wayne. It was almosy like she was married to Walter. Ule wasiwasi kwamba iko siku atatoka kazini asimkute Walter ukaanza kimtoka kidogo kidogooo.
Siku hio Walter akaenda kwa Collins ofisini, hio ni mara ya 2 kukutana baada ya mpambano wao. Collins akagoma kuonana nae. Akaacha bahasha pale. Collins akapelekewa akaifungua instant, ni kinote tu kimeandikwa kwa mkono "NAOMBA UWE MSHENGA WANGU NATAKA KUMUOA MTU MWINGINE." Iqra harudi tena, umri umeenda tuoe tu ndugu yangu. Daima nitampenda Iqra, ila nimepata mtu mwingine alie hai, na ni mwema na mkarimu sanaa kwangu kwa hio namuoa nakushauri na wewe ufanye hivo hivo ndugu yangu. Kila laheri. Nitakuletea kadi ya mwaliko. WALTER!
ITAENDELEA SAA 5 USIKU.