Weekend Story! The Workaholics Silence

Weekend Story! The Workaholics Silence

Hahahaaa! Huyu anakupenda nakwambiaa, msikize kijanaaa. WAGOMBANAO NDO MPENDANAO. Mi nawafatilia tu kwa ukaribuuu.
Yaani wewe Lara,ndio maana nikasema wewe ni matawi ya juu,kama mchawi vile,ukweli huyo mtoto mimi namzimikia ila kila nikitia gia yeye anachomoa,hata hivyo ukweli mimi nampenda.
 
Akili fupi! Si unaona mambo ya kitoto. Halafu eti akujue jue, wewe Matawi ya Stacy. Hebu shusha vitu vya kina Harry, Gill, Lau na Stacy! Hongera mami, ibarikiwe kazi ya vidole vyako.
Sasa wewe mrembo,mbona tulishasameheana sana,hata nikawa nakupa like?,ila nimeshangaa unanitilia kauzibe kwa Lara binti wa kimarangu?,basi yaishe mrembo ili tugange yajayo au unaonaje? huyo Lara hajakosea kabisa kwamba mimi na wewe tunapendana ila shetani ndio anatia kauzibe au vipi?
 
SOON NAKUJA NA BLOG, AMBAYO ITAKUSANYA STORY ZOOOTE ZANGU SEHEMU MOJA. SO INSTA IPOTEZEE. BLOG NDO KILA KITU. NITAKU TAARIFU.

Hii habari njema inabidi uipandishe juu kwenye bandiko la mwanzo i update wadau waachane na habari za Instagram. Ushauri tu lakini.
 
Unafikiri hata nikiweka ingine itawafikisha chini chini. Ndo kwanzaaaa naanza kuiandika. So ngomaa saa 6 au 7.
hahaaaaa hili dude nalisubiri mae
siwapendi watabiri hadi wananiondolea rahaaaaa
 
SOON NAKUJA NA BLOG, AMBAYO ITAKUSANYA STORY ZOOOTE ZANGU SEHEMU MOJA. SO INSTA IPOTEZEE. BLOG NDO KILA KITU. NITAKU TAARIFU.
hii ni habari njema usisahau kunishtua maana kuna stor nataman kuzirudia kwakwel
 
What i like about this lady I dnt know girl, ni Kwamba she never under perform katika hii career yake.. Mimi ni professional cinematographer nimekua nikifuatlia Sana story Zake na kupiga picha ya kitu harisi katika mfano wa film,believe me hiki kinachoadithiwa katika most of her story akipata waandaaji wazuri wa film my dear friends kina Taylor Perry wajipange haswa sababu anauwezo mkubwa wa kufanya continuity bila kupoteza ubora wa story yani she has a talent... Congrats
 
Laraaaaaaaaaaaaaaaa kamu zisi wei utamu unakuja utamu unakata daaaah .

ila Gill msengerema tu Harry angemuacha aunguzwe na yule Malaya.

Huu Uzi nimesabskraibu kabisa ili ukishusha madini nipate notifikesheni kabisa .

Chineeeeeeeeeekeeees
 
Harris kuujua ukwli kwamba Stacy hausiki na zile shutumaa, kilimuuma sanaa and he was always hating on her, bitter towards her alafu kumbe ni kitu ambacho hajakifanyaaa. Aiseeeeeeee. Tse tse tse. Akifikiria ule umafia aliomfanyia juzi kumkomoa tuuu. Na umafia mwingine mwingine. Akajisikia vibaya sanaa. Akawaza ama kweli ukimchimbia mwenzio shimo, usichimbe sanaaa, manake unaweza kutumbukia mwenyewe.

Akawa anawaza anaanzia wapi sasa kujirudishaaa. Manake juzi hali ilikuwa tete sanaaa. Akawa hapati muafaka. Akaamua kumtumia sms. Mambo! Ikajibiwa "Poa! Za kunitenda vile kisa nini?" Harry akajibalaguza nililewa sanaaa, nisamehe bureee, sikutendi vile tenaaa. Pombe ndo za kulaumiwa. Njoo basi nyumbani nikupe mambo mazito." Stacy akamjibu Akhahaaaa, namuogopa mkeo, nisije chanwa chanwa na viwembe bureee" Harris akamjibu hayupo, wamesafiri na mtoto tunavoongeaaa, jumba lote niko peke yangu." Stacy aka mwambia "Akhaaaaa! Prince ananitgemea".

Harry akawa focused na show yake ile ya kihistoria aliotaka kufanya show mikoa 8, siku moja, masaa sawa, tofauti ni wasanii tu. Mambo yakawa magumu pesa ilihitajika sanaaa nyingiii. Akaamua kubet all his money kwenye hio show, akijua akitusua hapo, returns zake Gill mwenyewe atakaa chini. Yani it was about making millions in a matter of hours.

Akaiuza idea kwa promotes wengine wakaigomea hio idea, kwamba t is too risky, haijawahi kufanyikaaa, ni kitu hatariii sanaa. Harry akamua to go with his hunch kwamba it was time kufanya kitu kama kile. Wakati wake aliousubiri ndo ule. Akaamua kuweka hela zake zote kuwa sole promoter wa hio kitu. Sasa hizi process zikawa zina mstress sanaaa, manae ni ngumu alivodhania. Akajikuta kichwaa kina muuma and he needs to relax. Akamkumbuka Stacy.

Akapiga mahesabu yake akimwambia zitaanza siasa nyingiii, na ukorofi wake wa mwisho utakumbushiwa, mwisho itakuwa kunyimwa game and he really needed that game for relaxing his mind ili aweze ku concentrate na kufanya kitu chenye akili. Kama hivoanakaa anawazaa na kufatilia mambo, afuanapiga game moja matata ya kumtuliza akili afu anawaza tenaaaa. Huo ndo mpango ambao ungeenda. Akachukua kibegi cha nguo akamuibukia Stacy kwake

Kufika pale hakwenda na gari, alienda na boda boda, kashuka kaingia getini, akakuta gari la Gill. Mmmmh! Roho ikamfanya Paah! Akaficha kibegi chake maana Gill angemuona n bag, asingeshindwa na yeye kwenda kuchukua bag akaja hapo hapo mradi tu kumkomoa afu ingekuwa vitukooo.

Kaingia sebuleni kakuta wana kunywaaa, akakaribishwa na yeye akajisevia, basi wakawa wanakunywa kimya kimya wanaangalia tv hamna anae msemesha mwenzie. Stacy akavunja ukimya, akamuuliza Harris "Kwema huko? Mbona ghafla bila taarifa?" Harris akajua tu Stacy anajikosha kwa Gill akaamua kuwakomesha wote. Akajibu "Jamani hapa si kwangu jamani nitoe taarifa ya nini? Labda tumuulize Gill kwemaa huko kwake mbona ghafla?" Hahahaaaa! Wakacheka wote. Gill akajibu "Mi hapa ndo kwangu kabisaaa, hizi furniture zote nimemnunua mimi, mtoto mwenyew nimemgomboa mimi sasa nitoe taarifa ya nini?" Stacy akaona hivi vita baridi vinapoelekea sio kwemaaa kabisaa. Akabadilisha topic "Wake zenu hawajambo?" Kuwakomoa woteee. Gill akafurahishwa na ile mada na hivi hana mke kidogo apige vigelegele, nderemo na vifijooo aleleleeeeeeeeeeeee! Akawahi kujibu "Tumuulize mwenye mke, tena ndoa changaaa bado mbichiiii, katoto ndo kwanza kamojaaa, mkeo hajambo, majumbani mwa watu mpaka saa 7 hii jamani huyo mkeo huko hom vepeeee?' Harris lile dongo likamuingia sawia, na kilicho mkossha nguvu kweli Gill hana mke sahivi akaamua kumpa ushindi wa mezani

Wakaendela kuangalia t mpaka saa 9 hamna anae aga. Stacy akaanza kusinzia, kuwafukuza haweziii maskini ya Mungu, akatamani awaambie anaingia ndani kulala, ila haweziiii. Akaamua kusinzia pale pale kwenye kochi. Harriis akavunja ukimya kumuuliza Gill, Gill unaondoka saa ngapi naomba lift, mi sijaja na gari!" Gill akamwambia "Boda boda mbona ziko nyingi tu, tunakutakia usiku mwema." Hahahaaaaaaaaaaa! Wakajikuta wote wanachekaa. Gill akaapa hata ikibidi kulala kwenye kochi yupo tayari sio kutoka mule kumuacha Harris ndani. Thubutuuuuuu. Harry uzalendo ukamshinda akaaga "Jamani niwatakie usiku mwemaaa. Stacy akamjibu tu haya Harry, msalimie mrembo na mama yake. Akanyanyuka kumsindikiza na Gill akanyanyuka. Harry akamuuliza "Gill kwa hio ndo tunaondoka unipe hio lift au?" Gill akamwambia " Hamnaaa sisi wenye nyumba ndo tunakusindikiza mgeni" Hahahaaaaaa! Wakacheka woote. Harry katoka mpaka nje ya geti kabisaaa. Akaita boda boda akaishia.

Gill kujriidhisha ashamkomoa Harry, nae akaaga pale pale kwamba "Thanks for the talk, imenipa faraja sanaa, ngoja na mimi nikalale usiku ushakuwa mwingi sanaaa. Akaingia kwenye gari lake akaondoka. Stacy akafunga geti lake vizuri finally nae akalale manake picha la leo lilikuwa limeungua ungua. Akajiuliza Harry alitokea wapi ghafla vileee. Akatikisa kichwa, anafunga grilli la mlango akasikia mtu anagonga. Akauliza Naniiiii? Akasikia "Harry nifungulie bwana nitakabwa hapaa" Akaenda kumfungulia. "Vipi umesahau kitu?" Harry aajibu "Nilikuwa nimeenda kumpoteza maboya Gill maana nisingetoka nae asingetokaa" akaongoza ndani, akainama kwenye maua akatoa kibegi chake akaingia nacho ndani wakati Stacy anafunga geti


Kuingia ndani anakuta kibegi, akaguna Mmmmmhhhh! Akauliza "Umetoka safari au ndo unaelekeaa? Harry akamjibu "Ndo nimefikaa safari yangu" Akakipeleka kibegi chumbani kwa Stacy. Hahahaaa! Stacy moyoni anafurahi lile swala lae la mbegu huenda likafanikiwaaaa. Akajipa moyo huyu akikaa wiki nzima hapa si habaaa. Na asha soma mambo yake jinsi ya kunasaaa, yaani she was ready.

Kufika chumbani wakaingia kuoga, Stacy akaanza, akafatia Harry aaah. Mechi ikaanza kupigwa. Stacy anawaza tu na leo akmwaga nje namtimua usiku huuu huu asiniletee ubaradhuli. Wameenda vizuriii kabisaaa, hakumwaga nje wala nini. Mechi imeisha Stacy akawa kakaa miguu juu. Harry anamuuliza vipi tena mbona miguu ukutani, akamwambia miguu inaniuma kweliii mwenzio, ndo nainyoosha hapa. Baadae akaenda kuoga tena akalala akamucha Harry anafanya kazi kwenye laptop na kuongea na simu.

Asubuhi anaenda kazini, Harry kalala. Akawahi kuamka, kamuandaa Prince fresh kabisaa, akamuandalia na Harry bonge la break fast, baba mwenye nyumba tenaa. Akamwambia dada akiamka mpashieeee. Umpe na juice hii naiweka kwenye fridge. Akaenda kazini. Zinaingia sms za "Thanks baby for he breakfast i really enjoyed" Basi Stacy bichwaaa hilo. Saa 11 anawahi nyumbani akaulizwa shoga saluni hupiti? Akasema "sipitiiiii, siku hizi naishi na bwana nawahi kupikaaa, kama nimeolewaa vile." Hahahaaa! Wakacheka hayaaa.

Kawahinyumbani, kalisimamia jiko mwenyewe, kapika makaroni ya kusaga hatari sanaa. Mpaka dada na Prince wakaongeza wakati sio walaji. Akawaambia wa wahi kulala mapemaaaa, sio kutaka kuwabanaa. Akawa amekaa anamngoja bwana arudi, saa 7 hajaja. Akawa ashanunaaa. Akatuma sms, "unakuja au ndo umeenda kwa mkeo?" Akajibiwa nakujaa bwana, usilale ningojeee. Akafurahiiii. Akaaamua amngoje pale pale kwenye kochi.Akaja kustukaa saa 11, kalala pale pal kwnye kochi, mwili unamuuma, Harry hajaja wala nini. Akachukua chakula kwenye hotpot akatumbukiza kwenye friji. Akaanza kumuandaa Prince shule. Saa 11 na nusu, Harry ndo anaingia. "Baby so sorry, yalitokea mambo sikuyaelewaaa." Stacy yuko serious. Amemaliza kumuandaa mtoto kajiandaa kazini kasepa kimya kimya bila kumsemesha. Moyoni anawaza sasa huku kufanyana wajingaaa. unilaze kwenye kochi kisaaa.

Akiwa kazini akapokea sms toka kwa Harry, "sorry baby, najua nimekukera ila nilikuwa kazini mda ule kazi yangu ngumu. Ila nitajitahidi nisiwe na kukwaza. Ila makaroni matamu sanaa." Wanawake kwa kupenda sifa sisi hovyoooo. Akalainikaa. Saa 11 huyo anawahi kumpikia bwana, chezea kuishi na bwana unae mkubali rohoni. Akafika amkua Harry ashafika, akajua labda baadae ndo atatokaaa. Akamuuliza utakula nini, akasema wewe pika chochote tu. Akapika saa 2 wakala, kina Prince na dada kulala.

Stacy akawa yupo kwenye laptop yake, akashangaa mtu anamgusa gusa, akamuuliza "huendi kazini leo?" Akamwmabia jana alimboa sanaa so leo he is going to make it up for her. Ikawa mechi moja matata sanaaa. tena yenye round nyingiii. Baada ya mechi ndo akamwambia kuhusu hio show yake ya mikoa 8. Stacy akawa tu supportive si hela yake bwanaaa. Aaaaaah! Akamwambia show hizo ni jumamosi, he is going to make history! Stacy was happy for him akawa anaomba tu Mungu by jumamosi awe na mimba tayari. Manake after hio history going concern ya bwana akawa haielewi.

Kuanzia ijumaa hajaenda kazini, kumsupport Mr. Mda wote wako bega kwa bega. Hela hazikutosha akaweka bond gari, nyumba na viwanja. Akapata hela za kujazia last minute. Mpaka siku ya tukio kila kitu kiko fresh kabisaaa. Stacy was exited for him. Yeye Harris was exited. Mambo yakawa moto moto.

Kufika jioni Harry akawa na mood mbayaaa sanaa. Anapigiwa simu huko kwenye show karibia zote zime FLOP! Yaani zimebumaaaa zoooteeeeeeeeee. Mahudhurio yalikuwa mabaya, kazi kubwa sanaa watu alio waamini kusimamia wamemuangusha Harry. Yani Harry ni kwamba KAFILISIKA FIIIIIII. Vitu alivoweka bond vyote kwishaa, na bado ana madeni mengineee. Na reputation yake u promoter ndo basi tenaaa.

Stacy akachokaaa kwa taarifa. Akamuonea imani Harry si kidogo.

ITAENDELEA KESHO USIKU SAA 2.
 
Kubwa la maadui kama kawaida haujatuangusha team popo, shukrani.
 
Laraaaaaaaaaaaaaaaa kamu zisi wei utamu unakuja utamu unakata daaaah .

ila Gill msengerema tu Harry angemuacha aunguzwe na yule Malaya.

Huu Uzi nimesabskraibu kabisa ili ukishusha madini nipate notifikesheni kabisa .

Chineeeeeeeeeekeeees
Angemuacha nae angeingia kingi uwezekano wa kushare stacy ni Mkubwa, japo naamini stacy ni wa Gill tu,... Na ktk kuotea sikoseagi..... Wacha muvi iendelee
 
Haha haha haha shah harry kacheza betting na muhindi aka kanjibaj kala mshiko wote hahahhhah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom