Leilat!
Kwa umri huu niliofikia, na level ya maisha niliopo nadiriki kusema kuwa wanaume hawanipi stress kabisaaa. Zile zama za kujambishwa jambishwa na vidume zimenipita kwa kweli. Nashukuru Mungu kwa kweli. Nina mjengo wangu naupangisha, nina gari zangu 2, wazazi wangu nimewajengea, nina mtaji wa million 50 usioyumba, nina mashamba, million 5 za matumizi kila mwezi hazinipigi chengaaa, aaahhh Alhamdullialah kwa kweli. Kama kwenda nje nishaenda sanaa, naenda kama naenda Ilala. Mzigo ukiisha nafata. Yaani sijui wapi sijaenda. Nishaenda Ulaya karibia yote labda waongeze mipaka, hio Us nishaendaa, south america nayo nimetamba sanaa, tena kwa kujisikia tu. Kama kupanda ndege nishakuwa staff nina niko Gold member huko.
Sahivi sijui nini mimi kitanizuzua. Nashukuru wazazi wangu hawana kitu ila mwenyewe kwa kukomaa tu na dunia mpaka nimetokaaa, ofcourse there is also Gods grace. Kwa hio sahivi wanaume wanavo jamba jamba nawatizama tu, kwa masikitiko. I live my own life on my own rules.
The only 2 regrets i have maybe sikuzaa tu mapema. Not that sikuamua ila maisha yalibanaaa sanaaa. Nikaamua nisizae kwanza nikomae na life. Nina mpango wa kuzaa soon maana sasa ndo wakati muafaka. Na regret ingine nimekuwa mzinzi all my life, so disapointing to my God. Ndo maana dini zinasema oleweni na maskini wenzenu kusudi msizini, kukomaa na maisha unajikuta una over 10 years experience ya kuzini. Hata kama mume FREE P, walau unakuwa on the good side of God, tukiitwa wazinzi hutoki. Hahaaaaaa. And the worst part at my age kila mtu anajua there is no way lazima nazini on daily basis, maana mume sina, naishije kama sio kugongea kwa watu. Hahaaa. Kiukweli mi nishazini sanaa, hainisumbui kinachonisumbua ni kwamba Mungu kanitetea sanaa, why cant i do it for him. Nimlipe fadhila Mola, kwa sababu zamani nilimlilia njaa kali ndo maana nazini, kaniwekea jaba limejaa nyama, sasa nazini kitu gabi tena. Tseee tseeeee tseeeeee tseeeee. Inatia huruma.
Sio kwamba mpaka leo i never wanted to get married at a point in my life, bali ni kwamba zilitokea situations tu, zikasababisha ikashindikiana . Partly i blame me, partly i blame life, partly i blame the delvil. Whatever, it is what it is.
1st i wanted to marry Michael, my collage sweet heart. Tatizo Michael alikuwa mchoyo yule mwanaume sijawahi kuona. Na alikuwa ananiomba pesa tangu tupo chuo. Siku 2 utasikia nitumie vocha narudisha. Namtumia anarudisha. Siku 2 nikope kiasi hiki. Nikashindwana nae chuo hapo. Mambo gani ya kuchunana mchana kweupe. Alijitahidi sanaa sanaa kirudisha uhusiano wetu ila nishaa mua sichunwi ngoooo.
Baada ya chuo he got this really nice job at auditing firm. Tulipotezana like 2 years akaja kunitafuta. Nikajua he was changed. With his new job, gari ya mkopo, na kupanga nyumba nzima nikajua i must have made a mistake kuachana nae. Alivonicheki nikajirahisisha hatari. Akanialika kwake ndugu wasomaji, nikaenda, akala mzigooo. Hakunipiaaaaa. Ndio hakunipigiaaaa.
Nikawa nikimpigia hapokei, mara apokeee na kudengua denguaaaa kama shoga wallah! Amachotaka niende anilee afu basi. Hakusema ila inaonesha alikuwa na mtu mwingine he wanted a sexual relationship. Ila anakupiga miti afu baas. Nika mblock kwenye simu yangu.
Nikaja kukutana nae tena mbele mbele huko akanila tena afu basi. Yaani huyu motoni atakuwa kuni. Baada ya kunila akaja kuniambia naoa mwezi ujao. Nilikuwa na dhiki hatariiii. Sina kazi, nina nyumba ya kulipa, nimedataaa. Nikamuomba msaada wa kodi 150,000 hayo ya yeye kuoa sikuyajaliiiii, njaa mbaya sanaa. Akaniambia sina. Mtu yuko Auditing firm kabipa Free pumbu si chini ya mara 10. Kweli wa kuniambia mimi hivo.
Akaja kunitafuta akiwa marekani, alitaka kunidolishia, alijua bado nimechoka kumbe Mungu si lara 1, wala
Von Mo nikawa na kikazi cha kuzugia. Nikawa namjibu dry tu. Nika muuliza umeoa? Bado ila this June ndo naoa sijui nini. Nikamwambia niletee kadi ya mchango. Mpaka kesho hajaleta kimyaaa.
Nikaja kupata bwana White, Hb hatariii. Tulipendana vibaya mnooo. Nae akaanza tabia ile ile ya kukopa pesa. Sasa sijui mwenzenu na pesa nyingi au wanaume wakiniona wanaona mi safe la hela sijui. Nikawq namkopesha namdai. Namkopesha namdai. Ila nikachokaa. Akaniazima camera, akaja kudai imepotea najua aliibana kabisaa. Ndo tabia gani za kiswahilii swahiliik
Nilikuwa nampenda hatariii hasa uzuri wake nikajua nikizaa toto litakuwa zuriii hatari. Namvumilia. Ila akawa haeleweki heleweki, mara simu asipokeee, mara aende safari isio eleweka. Namvumilia tu. Mara aseme demu wake wa zamani anamtaka. Namchoraaa tu. Mara msichana wa kiarabu kamtongoza. Yaaaani mradi aninyime raha tu.
Huku na huku siku kuna namba alinipaga kitambo, akaja kusema niufute haitumii tena, tuko kitandani tayari kwa mechi kabisaa, akasema nimtumie picha ya viatu kwenye hio namba, nakuta kakiweka kitoto cha chuo profile. Mxiuuuuuu. Nikamuuliza huyu nani? Oooh usifatilie sanaa utaumia, mambo mengine potezea. Nikamwambia sawa baba. Usiku ulipita bila bila. Asubuhi kaondoka nikawa nampotezea. Ile mapenzi yamekufa zamani.
Sasa alipata kazi mkoa mwingine, ambapo kuna wazazi wangu. Nikamuombe apangishwe nyumba ya servant quarter. Mzee akampangisha. Mpaka sakata linaendelea la profile picture akawa anaishi pale. Ingekuwa mtu mzima anajiongeza angehama. Hakuhama. Mimi nikawa nashindwa kwenda nyumbani kwa amani. Nikakaza roho.
Akijua nipo analeta mademu hatari kama kunikomoa tu. Roho ikaniumaa sanaa. Nikamwambia Mzee mfukuze. Akakomaa kwanini? Ikabidi nimwambie uwongo anakusema kwa wtau sijui nini. Mzee sababu mimi bintiye akaniamini japo analalamika mpangaji wangu mzuri sanaa, hanikawizii kodi hata kidogo. Moyoni nasema nyooo. Akampa notice. Akagoma kuhamaaa kabisaa. Akamwambia naongeza kodi, mshaona mpangaji anajipandishia kodi??? Mzee akanicheki kweli nimfukuze, nikamwambia shauri yako, usomfukuza mtaa mzima watakuwa wanakishangaaa.
Akamkazia huo uamuzi wa familia kijana, hamaaaa. Akaja kuhama siku Mzee yupo ndani, afu fungua akamtupia uwanjani. Ila kwa dharauuuu. Mzee akasema kweli kijana mjeuriii nimejioneaaa. Hahahaaaa. Hatujaonana tenaa akaja tu kuni follow Instagram. Nikasema njoo mwana hizaya wewe nikukomesheee na maishaaa.
Ofcourse wote walikuwa na mazuri yao mengi tu walionifanyia, ila sio ya kujadiliwa leo. Yana siku yake niatawapa kwa undani.
Katikati hapo kuna Mnyalukolo aka mla mbwa tulikuwa tunakutana chuo sema hakuwa hata na 100, alikuwa katoka kijijini Iringa huko mshamba hatariii. Nilimzoea juu juu tu. Nikakutana nae posta kabla sijakutana na white ila nishatibuana na Michael. Tukapeana namba tukawa tunawasiliana. Alikuwa hana hela kabisaaa. Kachokaaa. Sema alinifundisha biashara ya kutafuta tenda, yeye kasome mambo ya electrical engineering, na security. Mi natafuta kazi wananilipa 10%. We made a lot of money together. Ila aliletewa msichana kijini mnyalu mwenzie amsomeshe nursing, akawa kamla wakazaaa. Ila hampendi hampendiii hata kumuonaaa. Sijui alilogwa sijui vipi.
Akataka kunioa mimi serious kabisaaa, tatizo maisha yake nilikuwa nayaona magumuuu, afu sijampendaaa, yaani balaaa juu ya balaa. He treated me very well. Ila sasa akanza kufosi tuwe woteeee. Namna gani tena , mnyaluuuu. Nikaachaga kufanya nao business. Akawa ananitafuta from time to time napotezea tu.
Hata nilivokuwa na white ananitafuta, namzingua siku zinaenda. Akaja kupata kazi pension funds. Alipewa kazi na ndugu yake waziri. Akawa boss mkubwa tu, kitengo cha tenda. Na kampuni yake ile tuliokuwa wote ikawa imekuaaa, anafanya miradi ya billions. Na hivi nyalukolo kama mkinga. Akainvest kwenye fuso, akawa nazo kama 6, mashamba anafuga na kulima mbao huko Iringa, matrekta yuko poa vibaya mnoooo. Still offer yake iko wazi all this time me kujiongezaaa.
Baada ya kumtimua white akaja tena na offer yake ile ile. Sasa mda huo nishachoka kudanga, sijanufaika chochote, nikaamua kukomaaa kufanya biashara mimi kama mimi. Huku na huku nikatoboa bisiness, bado marafiki wazuri sanaa. Mpaka kesho. Akanitafutia mashamba, of which sina intrest amenilimia mbao, nangoja kwenda kuvuna, maana alinunu heka 110, akasema ngoja nikupe hizi 10 zinavuruga hesabu. Mgagaa na upwa sili wali mkavu. Chakula sinunu mjini hapa, mchele, unga mbuzi, kuku, naletewa tu. Sms tu inaingia kachukua mzigo kwa J4 anakuja na fuso T ngapi ngapi. Gunia la mhele, viazi, mahindi, tenga la kuku. Aaaah sina stress.
Mpaka tunavoongea his offer still stands, mda m2ingine nawaza huyu kaka kanifanyia yote haya sijui nimzalie mtoto mmoja, si ndo atanifanyia 1000000 ila roho nzito, sikio la kufa halisikiagi dawa.
Kuna fupi pia, mwalimu wangu wa tution. Aliniomba sana sana anioe, tatizo ndo ufupi na kushikwa akili na mama ake. Fupi mfupi msijue fupi kishkaji. Kanibembelezaaa, akachokaaaa. Sikumpendaga tu. Nimegawa uchi bureee Ta mpaka dubai, mpaka china, mpaka Paris Free P tu napigwa huyo huyo Leila, ila fupi hamuwezi amini nilimnyima uchi mwenzenu. Ule ufupi wake nilihisi kibamia sijui. Sijui.
Akaja kukata tamaa, akaoa demu mkaliiii, bongeeee moja ya demu, naingia kwake mara laki moja labda. Mpaka nikajiona mpuuzi kumkataa fupi wakati mwenzangu mzuri kuliko hata mimi kamkubalia na wanajiachiaaa kwa raha zao. Ila sijui ilikuwaje ndo haikudumu hata mwaka.
Sijui details, ila mama fupi akiongelea swala la ndoa ya mwanae kuvunjika lazima anitaje mimi na kunitupia lawama zote. Maza kama mwanga. Ingekuwa nishawahi kumvulia chupi fupi ningestukaa na yanayosemwa ila sababu na umalaya wangu wote sikuwahi, that is the only case i am clean 100% sistukii. Fupi ana insist tukutane, tukutaneee, tuongee, nafanya kumkimbiaa. Maana watu si ndo watasema lisemwalo lipo.
Nikitaja list yamabwana zangu wote nitajaza hili jamvi, hao ni wale parmanent au waliojitokeza katika muongo mzima. Amabao siwezi kuwa ignore. Kuna hawa wa mpito tuachane nao kwanza, maana walipotea kama walivoibukaaa.
ITAENDELEA KESHO