Weekend story! BEN 10

Weekend story! BEN 10

Mimi ni ndugu msomaji tuu... mambo ya team nawaachie nyie...


Kimoyo moyo lazima uwe na team tu....ukubali ukatae...Au we shabiki jina tehtehteh....... mi bado nazoom kwanza mchezo sijausoma vizuri
 
Hahahahaha.. Dogo anamtamani kwa nguvu zote afu ajitia kuzingua lol utu uzima noumaaa na ujanja wote ameulaa
ila mechi ya hans haijanibariki kabisaaaaa......



cc Smart911
lazima utamani mixer kujitutumua,unakosaje kutamani gold mine labda.. hahhhahaha..
Same here kuhusu mechi,kapooza sana dogo Hance. Kwanza Verse zake azisevu after mechi..
 
Beggining of the end!

Kiukweli kabisa mwanamke wako akiwa anachepuka lazima utajuaaa. Lazima 3rd sense itakwambia tu. Mimi Kyle ana hanga out na watu kibaoo, naweza nisistuke kabisaa. Anaendaga nje na machalii zangu wanakaa mwezi na namuamini hawezi fanyi kitu ya jingaaa. Naweza sema yuko trust worthy 200%. Ila jana kitendo ya kuniambia yuko na Hans kwanza hilo jina lilinishtua sanaaa. Basi tu. Sio vile siwajui kina Hans.

Na jinsi anavo convoo na mimi bwana ake ikawa some how different like she cares what this Hans thinks. Na vile nimeongea nikaona ananiletea compeeeeee, nikaona hapana hawa ndo wale machaliii anakuangaIia usoni na kukubea ngachuriii wako. Nilikuwa home kuna msba namalizia nikaona hapana aisee nikawasha motocar usiku kucha nakanyagia oil mpaka asubuhi ikanikuta Dar.

Kilichoniuma zaidiii sikumkuta Hans, wala ushahidi wa simu haukuwepo ila Kyle alikuwa kachokaa kabisaa kama ametoka kulala na mwanaume. Sio mtu alie relax usiku kucha. Nikamwambia nipe mechi, kumpima tu saikolojia yake. Akakataaa. Nikamkomalia. For the first time in our realation ya 10 years akaniletea kibesiiii. Akaniambia "Mapenzi sikupi fanya unachowezaaa, wewe sio baba yangu mzazi useme utanisumbua kichwa. Liwalo na liwe."

She was certain, decesive, na hajaliii kabisaa. Kitu ambacho sio kawaida yake. Kawaida yake ni kuwa muoga muoga fala fala, anayeendesheka na ananijali mimi kuliko yeye. Baada ya kujibu vile. Sikubisha nae, nikaona labda ameteleza. Nikaondoka kimya kimya. Nikimchuniaga ndani ya masaa lazima yaani ni lazimaa aniombe msamaha yeye. Nikapanga akiniomba msamaha nauchuna kama wiki 5. Nikija kumsamehe tunaheshimiana.

Nimetoka nikaenda bar kucheza pool table, na kunywa, mpaka jioni kimyaa. Nikaenda club kimyaa, azubuhi kimyaaa. Nikajua tu huyo Hans sio mtu mzuri kwangu kabisaa. Mabadiliko anayoleta kwenye mahusiano yangu mbona yana kasi ya 4G. Nikajikazaaa. Ilipita wiki ndugu msomaji. For the first time tangu nianze kudate nae alidinda kuniomba msamaha.

Kinachoniuma sanaa ndugu msomaji sio kwamba nampenda sanaa huyu ngachuri ila kitendo cha yeye kufanya makosa, mimi kumfuma na kunikata like im nothing, sio kitu kabisaa. Kama MAFIA, MAFIA haswaaa. She is questioning my entire manhoodship. Niliumia sanaa. After 10 years kweli namfumania afu yeye ndo anajitia mbabe na kusepa huyo bwana akiniacha mimi kende zinanininginia.

Sawa nakubali our relation was already toxic, kupigana kama kote, matusi ndo usiseme, but in the end we had each other. Najua mimi ni wake na yeye ni wangu. Sio kwa style hii. Kwanza hakuwa demu bombaaa hata kidogo. Hakuwa na pesa yoyote ya kunitikisa mimi hata dakika. Yaani alichonacho ni moyo wangu tu kivutiwa nae ndo jeuri yake.

Na kinachoniumasanaa sanaa ni kwamba mimi ndo nimemuweka kwenye ramani ya pesa. Alikutana na Moza akataka mtaji wa kwenda China, million 20 nilitoa. Sawa tunasaidiana, yeye alikuwa kaajiriwa, so anatulea on daily basisi, ila mimi ni dalali wa magari, viwanja na nyumba, nikipata pesa na take care ya bills kubwa kubwa kama kodi, anapoishi kodi nimempa mimi, huo mtaji umeyumba mara kibao naweka pesa, million 10, 15, 20. Nimenunua plot 2 moja jina langu, moja jina lake. Vaccations zote nalipia mimi. Ana tabia kila baada ya mda anabadilisha furniture nyumba nzima, kwa pesa yangu. When i say i own her i mean she is my personal property.

Acha sacrifices nilizoacha, kama Linda mpaka kesho ananitaka, nakataa sababu yake. Nilipata mchongo wa USA sijaenda ili niwe nae. Leo hii anajibu fanya unachowezaaa. Baada ya siku nne nikaona kapost yuko uturuki. Nikazuka nyumbani kwake, funguo ninazo. Kutafuta ushahidi. Holaaa.

Nikamtafuta linda na kumwambia tumegombana na Kyle, hajanizungumzia. Akasema hapana. Ila lastlyalitaka kununua Subaru yangu. Maana nasafisha yard yangu ku a gari nyingi sitembelei. Nikashangaa sana. Since when Kyle mtu wa subaruuu hizi? Nikamuuliza kwani subaru unauza bei gani? Ni model ipi? Akasema we njoo uione, mi nilipewagwa zawadi. But i know its expensive, nimemwambia nitamuuzia million 28, kalalamika lalamika sanaa nimeshushia mpaka 18. Kasema anajipanga aje achukue.

Kyle sio mtu wa subaruu, wala sio wa mashauzi, lazimaa mtu anahongwa hio gari. Mamaeeee. Gari anayoendesha nimenunua mimi. Nikamuuliza Linda unamjua Hans? Akasema Hans yupi? Rafiki wa kyle mpya. Akauliza kale katoto? Nikakaa mkao wa kusikiliza. Katoto kivipi. Anajimaliza, si kale kasaniii cha bongo fleva. Nikamwambia msaani as msaniii ? Akasema ndio. Nikaingia ggogle nikakaona hata kwenye kiganja hakijai.

If Kyle was cheating on me sio na hiki kitoto. Maybe anakitumia kama kanya boya tu. Ila babzazi OG lipooo. Ukute hata mme wa mtu huyo bazazi. Wananichezea mchezo wa kijinga hawanijuii. Nikaamua kwanza huyu dogo lazima nimuweke sawaaa. Kupata sehemu zenye show sio kazi sanaa. Nikasoma tu ratiba yake insta, nikaibukaa. Kumkuta Nilienda mimi na mshkaji wangu Ngosha. Ni mtu wa gym, mwenye mtu wa gym.

Tumetinga pale, tukasubiri show iishe. Lengo ni tumshikie bastola ajinyee nyeee aache shobo na wake za watu. Tukamuita akaja vizuri, si ajatujua. Tukajitambulisha, wala hastukiii. Kabla ngosha hajatoa kitu dogo design akasema code red. Huku na huku tumezungukwa na maselaa kama woteee. Nikamwambia ngosha achaa. Tukajikataa kimya kimya. Ila ndo alizidi kunikeraaa balaaa.

Akarudi uturuki, nikaibuka kwake. Akaniambia naomba funguo zangu. Nikamgea. Akasema ukiwa unakuja uwe unatoa taarifa. Nikasema haina haja, maana nitakuwa siji. Akasema ni vizuri zaidi. Nikamuuliza hivi Kyle mimi nimekosa nini kikubwa mpaka kunifanyia haya? Akasema sio lazima kuwe na makosa ni uamuzi tu kama maamuzi mengine.

Nikamwambia dont get it twisted, im just giving you space uone umuhimu wangu, na kutambua makosa yako. Ila kaa ukijua mimi ni bwana wako tena sanaaa. Usije ukafanya jambo la kingese mbele yangu. Damu itamwagika. Mi nakuwa mstaarabu kwa mda tu. Hatujaachana na kuachana hakupo. Nikaondoka zangu.

Nikaona si mbaya na mimi nijipe break fupi, i wanted something short, casual but yet iwe ya civilized. Nikajiunga Jf. Ngosha yupo Jf na anakula sanaa toto za Jf. Nikaanza kufatilia. Ubaya huku huoni suraa, ila ngosha nishmfuma na totoz 4 zote kali sanaa. Nikaanza ku post najitia maprosooo.

Wakaanza kujaa wenyewe Pm. La kwanza nitumie picha, ikiwa haina ubora na ku block Pm. Nikapata ngachuri kama 3 hivi za uhakika kabisaa. Nikawaza nizile vipi hizi. Wa kwanza nilimuingiza kingi niko USA. Akaanza kushoboka hatariii. Akaniomba picha, nikamwambia siwezi kukupa picha. Nakuja unione tufanyane. Nime chat nae wiki tu, akaanza kodi imeisha. Mngese kweli. Nikamwambia utapata Mola atakusaidia. Anataka kuniingiza kingi mimi, aaaaaa subutuuuu. Ikafika nimetolewa vitu nje, nikaona sasa this is bogus, nikamla block.

Wa pili nikambadilishia strategy, nikamuwahi yeye kumtangazia njaaa. Wiki tu nikaanza kujisemesha mambo yangu hayaendi vizuriii. Basi nae anajitia kavuuu. Nilichompendea ananipa sanaa ubuyu wa Jf. Akaniambia kuna mdada anampenda bwana wake. Nikamwambia nipe jina, akanipa nika search. Nikamuuliza mbona kama wanapendana sanaa. Akasema aaaaaa subutuuuuu. Bwana yule malaya mbwa. Mmmmmmh nikawa moyoni kumbe tuko wengi. Nikamuuliza kwanini? Alikutongoza? Akasema asinitongoze hio vipi? Kanitongoza ndio. Nikamuuliza ukamkubalia?

Akasema mwanzo alikuja na matashtiti ya kujitia cash money, ana ma dollari. Nikamuomba tu dola 100 tuuuu. Mavi ya kuku, mpaka kesho hakutumaaa. Mavi yake. Na kawatongoza mashoga zangu woteee. Sio nani kamtongoza swala ni nani hajamtongoza?

Nikasema mbona msimwambie mwenzenu mbona anajichoresha? Akasema acha ajichoreshee hivo hivo, si anajitia kungangania bwana. Ndo faida zake. Nikasikitika sanaa sababu niIjua huyu dada hanifaiii atanisababishia usumbufu wa kubadili badili ID kila mara, sio kwa umbea huoo. Hapo pengine na mimi kashanisambazaaa kwa mashoga zake.

Watatu nikakata shauri nikimchunguza sana bata sitomla. Huyu anajitia ni smartest woman jf, nikaenda nae direct. Mimi nimeoa na watoto wa 4, ila nahudumia hatarii, nipe mchezo huo. Akakubali. Sikutaka kufanya uzembe nikamwambia tukutane Morogoro anapokaa. Basi nikamega mzigo, na kulekeza ID kwani nina hasara gani. Sijui alinitafuta, sijui hakunitafuta sijuiii. Toka nimle sijainhia tena kwenye ile ID. Na namba sikumpa ukawa mwendo wa Pm tu.

Huku na huku Linda ananijia kasi. Sio kwamba simpendi, nishambanjua mara kibao, tagizo Linda jeuriii. Siku hio kama tumegongana tu elements, akaniambia kuna rafiki yake ana mngoja katoka mzumbe, yupo heart broken , ali date na mwanaume Jf kaenda morogoro wamebanjukaa, kamkoleaa kila sehemu ya mwili afu mwanaume kamkacha. Haingii online. Nikamsaidia kusikitika kidogo. Nilivopotea hilo eneo kwenye mazingira ya kutatanisha msomaji acha kabisaaa.

Nikawaza nimle mwanamke online afu huyo huyo awe shoga ake Linda mbona dunia hainipendi mie. Sababu sikumtumia picha nimepona hilooo. Hata kama ananijua nitamrukaaa. Ulipita kama mwezi sijaenda kwa Kyle wala hatusalimiani, siku hio nikaamua kuzuka ghafla. Nafika mchana yeye hayupo namkuta Hans anaangalia movies, kavaa pense, kifua wazi.

Sikutaka ligi. Nikamsalimia, nikamuuliza hii game if thrones season ngapi? Akasema 5, Nikaa wote tunatazama. Badae akaenda kupakua msosi, na mimi nikaenda kupakua. Kimya tunacheki Tv. Chombo kamaliza kakiacha pale pale. Mimi ndo bigger man, nikatoa changu na chake, akastukaa. Akasema broo nitakipeleka mwenywe. Nikamwambia acha tu nikutolee. Nikaenda kuviosha.

Saa 11, akaenda kuoga, akaniaga bro nina show, ukitaka kuondoka kama dada hajaa funguo weka chini ya ua. Nikamwambia poa haina noma mwanangu. Mtoto mkavuuu yuleee.

ITAENDELEA KESHO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom