Weekend story! BEN 10

Weekend story! BEN 10

Njia panda.

Kyle alipokuwa anaelekea sikoo. Sikoo sikooo. Ikabidi nimuite kikao. Akaniambia nakuja Da Moza. Akaja kweli. Nikamuuliza Sam mshapatana? Akasema hamnaaa. Nikamuuliza uliomba ule msamaha? Akabaki ana gwaya gwaya. Nikamchana live hivo unakosea shoga. Usiache mbachao kwa msala upitao. Sam has been in your life over a decade. Huwezi kumuacha hivi hivi kirejareja. Kama ni issue ya kumuacha kuna taratibu zake special.

Kama ni mgogoro sisi dada zako tunakaa kikao tunasuluhisha. Shoga nilikushauri uchepuke ila kuchepuka kuna zidi nguvu. Wenzio tunachepuka miaka na miaka, mahusiano yote konki napiga mechi za nje kama kawaida ila nikirudi ndani shoga angu adabu debe zimaaa, unyenyekevu pishiinajaa, heshima kibaba kimoja. Mwanaume hastukiii. Hata mtu akimwambia anasema uongooo. Haiwezekani.

Mi nimekaa na Dulla nachepuka haamini, siku alioamini ni siku mambo yangu nisha ya set namuaga Dulla mi ndo naondoka na wanangu kimoja. Ndo aliamini watu waliokuwa wanamwambia ya nyuma. Isitoshe Hans sio mwanaume yule. Ni kitoto, trophy boyfriend. For recreational purposes only. Sio mwanaume wa kusema am replace Sam, aaaaah subutuuuuuuuuuuuuu. Yule kama mwanao wa kumzaaukikaa nae ndani,maana lazima umkague nguo umefua, umepaka mafuta, umeoga asubuhi, sasa katakwambia nini kale katoto? Kwanza kama ni mie, Moza nikiwa na Hasira zangu naweza kukitandika makofi kisawa sawa. Heheheeeeee! Tukacheka wote.

Yule mtoto kama mtamu lala nae, ukisikia nyege unakaita uko wapi, mnamaliza mambo basi. Sio cha kukigeuza bwana, hivo unafeli shoga angu. Haya mtaji umekata, kitakusaidia nini? Hizo show zake za laki 3. Ushubwadu mtupuuu. Kama umeanza kumpenda sio kesi, kuna procedure tunazifanya anakutumbukia nyongo, hamu inakuishaa, unatuliza mshono unarudi kwa Sam.

Akauliza procedure gani? Nikamwambia tuna pasiana tu, kama mpira wa kona, wewe ushakula unanipa mi cross, napiga nacho mechi, nampa na mama lake anapiga kichwa, anampasia Linda, hivo hivo. Wewe unafikiri baada ya list hiyo utakataka?

Akaaanza kutetea, oooh mnavomfikiria sivo alivo. He is actually smart kichwani, sawa hajasoma sanaa, ila ana IQ kubwa, he is sweet, na ananipenda mimi for me. Nikamkatishaaaa! Wanaume shoga ngu usiwalie yaminiii. Umtoka kwenye dating game kitambooo, actually rules have changed, yule hakupendi wala nini, inapendwa pesa yako shogaaa. Mi nakwambia. Kama huamini niruhusu mie nimtongoze, nitakuita uje ufumanie. Akakubali shongo upandee.

Kikao hiki na shoga angu kikanikumbusha mbali mnooo mnoo kwa Dullayo! Enzi hizo na ukame wa mapenzi mie. Kupenda ujingaa ujingaaa. Kama Kyle nilikuwa nimevurugikaaa naona Dulla ndo kila kitu, hunambii kitu.

Siku ile baada ya kupiga show usiku, nikaenda ofisini, nangoja mrejesho je kaelewa show ya jana, au baradhuli tu ndo namba keshafutaaa. Mpaka saa 6 mchana bila bila, Man U 0, Asenali 0. Hamna cha sms wala simu. Saa 10 bado bilabila. Nikasema siwezi kukubali penalty, nampigia simuuu mwenyewe asintanie. Show yote ile ya kibabe afu analeta umama. Nampigia hata nimtukane tu basi. Nikawaza ngoja nifike home nikae kitandani nimnyambeeee kisawasawa.

Nimetoka pale, nikawa busy busy kutafuta chupa ya juice ya Ellah, na folleni, nimefika kwangu saa 2 usiku. Nikaoga, nikapanda kitandani na kushika simu sasa. Nakuta sms 5. Kufungua, Dullah! Bahati yakeeee. Nikasoa, sorry kwa kukutafuta mda huu najua ma teller hamruhusiwi kuwa na simu mchana ila now najua ushatoka.

Nikasahau yoote, tukaanza kuchat, huku na huku njoo ulale huku. Nikamgomea, mwanangu atalala mwenyewe kila siku. Moyoni nasema chiu huo kuufuja hivo baba umeoaaa. Akachomekea, mnapoishi na mwanao sipapendi haswaa mwanao. Mazingira sio mazuri kabisaa. Nikamwambia kweli ila ndo uwezo wa mama yake. Akasema njooni muishi huku.

Nikamwambia Dullah mimi nakupenda sanaa, ila mwanangu niachie mwenyewe. We mwanaume leo unanipenda mimi, kesho unamuona mzuri zaidi yangu unampenda pia, mimi mtu mzima nitavumilia nitayashinda, ila sio mwanangu. Hapo alipo anaumiza kichwa kwanini baba yake akaa na mwanamke mwengine sio mama yake. Najieleza kila siku Why am i not with daddy. Which is okay, nimeshajikubalia.

Leo nimbebe mwanangu wima, wima huyu nae pia baba, atafurahi yule malaika, kesho mara baba umeingia mitini. Sasa mtoto tutamvuruga. Akajibu kwa hio unaniona mimi muhuni sana sio? Nikamwambia no, sijaamanisha hivo, nachomaanisha watoto wawe off limits Dullah, hawa wanahitaji lifetime committments. Akajibu mbona masharti mengiii wakati ashatelekezwa na baba yake mzazi. Kmamae. Nika mblock hapo hapo. Asiniletee ungese.

Sikumtafutaa tena na pale kwa Dullah nikawa nimemalizaa kazi. Mimi utajiri wangu nilio nayo dunia nzima ni Ellah sasa mtu anavoanza kumchukulia kireja reja siwezi kumvumilia.Ikapita wiki, wiki ya 2 akaja kazini maana kila sehemu nime mblock, nikampotezea vile vile. Mnajua kwenye maisha kuna limits, na mtu akishazivuka hizo limits ni bora kukubali kunawa. Sasa niko kwenye mikopo akawa ananisumbua anajifanya kutaka mkopo. Kazi inanilazimu kwenda kumuhudumia.

Nikawaza sanaaa, sanaa, kazi ya mikopo naipenda mnoo mnoo, na exceed targets, napata bonus, afu shetani kaja kukalia hapo hapo. Nikakata shauri kwenda kwa boss. Nikamwambia tu boss mimi nishawahi kukusumbua , nishawahi kukuangusha au kukuletea compee? Akasema hapana you are the best here kwenye idara yangu. Nikamwambia boss nina ombi binafsi. Naomba unirudishe teller, au nipeleke hata recovery, au popote ila hapa credit siwezi kukaa tena.

Akastukaa, akasema hapana, mimi nakutegemea wewe kwa targets siweziii kuktoa. Jikaze tu. Moza usijifikirie wewe nifikirie na mimi. Isitoshe recovery sio sehemu ya kuomba kwenda, pagumu sanaa, na teller ni demotion siwezi kukufanyia hivo. Abdallah alikuwa sababu simtaki tena basi ananinynyasaaa ndugu msomaji acha kabisaa. Afu nampendaa. Usiombe unyanyaswe na mtu unaempenda ni kama unasulubishwa mwili na roho. Kuna watu aliniunganisha nao nikaanza kuwa processia mikopo akawapanga wa gahiri. Analalamika kwa boss namtukana. Basi tuuu.

Stress hizi nikaanza kumchukia mwanangu, naona kama ndo ananiletea mikosi. Nikawaza labda nisengzaa na baba mtu ningekuwa mbali sanaa, labda tungewezana na Dullah. Design mtoto ndo ananiletea kauzibe mambo yangu yasiende kabisaa. Nikakumbuka mabwana kibao wa maana nilikuwa nawapata wakijua na mtoto tu kama kimavi vile wanaanza siasa. Sahivi mtoto anaiharibia mpaka kazi yangu nayoipenda toka rohoniii. Nikaanza kuwa nambabuaaa. Kosa dogo namshushia kipigo cha mbwa mwizi. Akiingilia mtu namwambia zaa wako umbabue kama unaona nafaidi kumbabua. Nilikuwa nampigaa, namfokeaaa, cha moto alikiona. Mpaka akaanza kuwa zuzu. Akiniona akili zinamkaa sawa, hata utoto unamuisha anajikalia kwenye kiti kimyaaa.

Dada yangu akaenda kumwambia baba yake, mwanao anauwawa huku. Akamuonesha na video nikimshushia kipondo . Hakuitazama mpaka mwisho. Wakasuka mipango dada yangu mie amsaidie kumuiba ampeleke kwa baba yake. Narudi siku hio mtoto simkuti, nawauliza wanasema hawajui. Nawauliza mbona hamjanipigia wanasema kwa unavompiga siku hizi hatukutegemea ungejali. Ila tushaenda polisi. Niliumwaaa, nilichanganyikiwaa. Nilimtafuta mpaka kwenye pochi. Mpaka usiku hajapatikana. Nilimpigia mpaka Dullah mwanangu kapotea. Akaja anatusaidia kutafuta mtoto. Magazetini, insta, wapi na wapi. Na wale wa nyumbani wamevimba macho na wanatafuta kama watu. Baba mtoto nae anatafuta na sisi anajiliza masikini mwanangu wakati sh 10 ya ada hatoi.

Akili ikanijia niende nyumbani kwa mzazi mwenzangu, basi tu, nikaibukaa. Nikamkuta mkewe akasema pole kwa kupotelewa mtoto. Nikamuuliza tu huku hayupo? Akasema hayupo ila haniangalii machoni. Nikasema pisha nikague nijiridhishe. Akagomaa. Huku huingiii. Nikamwambia dogo hapa nilipo duniani sipo na ahera natafutwa nitakupiga hutoamini. Akagoma. Teke moja tu la tumbo, akapiga uwiiiiiiii, yuko chumbaniii. Ellah! Hatoki. Nikazama humo ndani, Ellaaaaah! Kimyaa. Nikamwambia dada onesha dogo alipo kabla sijakupa za chembe. Akanipeleka chumbani, Ellah yuko uvunguni.

Namwambia twende anasema siendiiii. Namwambia twende hatoki.Kagomaa. Dadaanamvuta kagomaa. Mama atanipiga. Watu wakawawamefika. Kesi ikawa kesi. Hadi ndugu zangu ndo wanaongoza kesi nisipewe mtoto kabisaa. Na video wanazo. Wako tayari kuzipeleka ustawi wa jamiiiii ninyanganywe mtoto. Ndo nika realise nimemkosea sanaa mwanangu. Nikabakia peke yangu na roho yangu tu sina mtetezi. Mpaka Dullah kaziona zile video anasapoti namna hii hawezi kupewa mtoto, asipewe kabisaa.

Nikajiangusha kwanza kama nimezimiaa. Hamna mwenye mda, jomoni hata kunipepea kidogo. Nikainuka nika kaa. Nikawaambia naombeni mnisikie nimekosa sanaa, nimekosa mimi, nimekosa juu yenu, juu ya Mungu, na juu ya hii dunia. Hapa nilipo nimefukuzwa kazi, na mjuavyo kazi ndo kila kwangu , sasa nawaombeni mnihuku hata wiki lijalo, ila nipeni mwanangu nimuage maana ilipofikia naona ninywe tu sumu nife. Maana nishajifelisha, nimemfelisha na mwanangu , sina nilichobakiza, nishafeli. Nipeni mtoto nimuage walau wiki afu mtamchukua milele.

Kidogo wakanionea hurumaa. Dada ndo kusema basi itabidi twende nae nyumbani maana mambo yamezidi kuwa makubwa mnooo. Kumbe huyu ana stresszake za kazi sisi hatujui maana sio kawaida yake, huwaga anampenda sanaa mwanae. Ndo kupewa mtoto sasa, damu nzito mwanangu bado ananipenda hivo hivo.

Usiku nikaandika resignation yangu vizuri kabisaa. Asubuhi nikaenda kukabidhi. Ilikuwa 24 hrs. Nikasafisha dawati langu, sikumuaga mtu. Baadae boss akaniita, akaniuliza haya ndo yale yale ya recovery, nikamwambia ndio. Akaniona siko kwenye form. Akaniambia nakupa siku 7 ufikirie, baada ya hapo kama usipobadili msimamo nitalazimika kui accept. Nikamwambia sawa.

Siku ya 4 akaniambia nimeongea na wanene wenye bank yao, na kukupigia chapuo, sema nimebadilisha gia kuwa unaacha sababu hawaja kugrow, wakati una potential kubwa. Huku na huku wamkubali kuku promote ukawe branch manager Kariakoo. Nikasema Asante Yesu mambo yamejisolve for the best. Nilimuona boss kama malaika. Kesho nikaenda training.

Mwanangu nikaacha kumpiga kabisaa, hata kikosea simpigi, namuangalia tu, nimempiga sanaa. Nikawa nawahi kurudi, tunacheza, tunapiga story, tunaenda kununua ice cream na kula junk foods. Nacheza nae rede. Kiukweli wanaume sio watu. Nikasema mimi KUPENDA BAAAASI.

Siku ya siku Dullah huyu kazoom kariakoo. Mi namuona kwenye kioo. Mie tena big boss. Sasa hivi nishapoona nishakuwa strong woman. Nammudu vizuri. Akaja anauliza mimi na yeye tuna ubaya gani? Nikamkumbusha ubaya wake wooote. Sikumfichaa. Mpaka alivo ni affect kisaikolojia kidogo nimuue mwanangu kwa kipondo. Akaomba radhi pale na nini. Nikamwambia mimi nisha samehe. Akaomba atolewe blcok. Nikamwambia block haitoki. Kufuli ndo mahala pake. Afterall sijapangakudate karibuni bado na repair damage ya uhusiano wangu na mwanangu. Kalia lia weee, holaaa.

Siku hio narudi nyumbani naambiwa kuna mshenga kaja, umeletwa barua kuna mtu anataka kukuposa. Nikajua wananizingua. Wakaileta kweli. Basi wanajisemesha tushakata tamaa kama hii barua haiji. Dullah huyo. Nikachukua peni nikaijibu Posa Imekataliwa. Sababu Bibi harusi ana mtoto na mtu mwengine, shurti akiolewa aje an mtoto wake, sasa je hilo sharti mnalikubali? Kwanza wanawake wako wengi ya nini kumngangania huyu aliezaaa.

Mshenga akaja kuchukua majibu. Mi nilikuwa sijamuona mara ya kwanza, nikajua Dullah na wahuni wenzie. Kumuona mtu mzimaaa. Na hesima zake. Akajitambulisha kaka yake Dullah wa kwanza baba mmoja na mama mmoja. Tobaaaa! Na posa nilivoijibu najua mwenyewe. Kumbe issue serious ya familia. Nikawa njia panda, Dullah nampenda ila mshenzi mshenzi sanaa. Anyway nishabugi step kuijibu ile posa kunya.

Wakaleta barua ingine wamekubali sharti la mimi kwenda na mwanangu, wako tayari kuoa, wapigwe mahari walete. Mmmmhhh! Kiukweli nilikua njia panda nikataka mda nitafakari. Bila kujua huku wenzangu wakajibu ile barua, mahari million 6 ndo akili zao zilivowatuma, na tarehe wakapanga. Mimi nakuja kuambiwa na mjomba Ommy, gaidi la magaidiii, kwanza kanissuza kwanini posa nijibu mimi? Hata kama wazazi hawapo na ndugu pia sinaaa? Yeye si mjomba wangu? Sasa nikae nikijua kwamba familia imeamua niozwe kwa Dullah hata mahari isipotimia na haina mjadala. Maana tangia miaka 20 nimepewa mda nitafute mume naempenda nimefeli. Sasa mume katokea huyo Dullah, kama baraka tu za Mungu, kwanza dini moja, pili mtu anaeleweka kwenye jamii, istoshe kwanza nishzeeka haina jinsi nikigoma kuolewa kwa hiari yangu watanioza kinguvu, bora nikatoa ushirikiano, ndo jambo la kheri, zinaa sio nzuri.

Nilichokaaa. Wakaja kulipa mahari, ukoo wake wote, nikaitwa naulizwa Mozaa unamjua huyu? Nikasema simjuiii. Mjomba anadakia haina haja ya kujuana, watajuana chumbani au nakosea jamani. Vigelegele kama vyoteeee. Nikarudi ndani. Walilipa mahari yote.

Dullah alienda kumwambia mjomba nimeblock, mjomba jioni kaniita, mie mjomba wako sio mjomba wako? Nikasema mjomba wangu. Mama yako aliniachia titi hajaniachia? Nikasema alikuachia. Sasa nasemaje mtolee Dullah, mumeo mtarajiwa, mumeo kimila tayari kofuli kwenye simu. Nikaanza kuongea. Akaniwahi, wewe wale watu kwenye mahari wooote unatuona wangese si ndio. tumeacha mambo yetu mangapi kuja kwenye issue yako hii? Bado unaona mzaha huu si atii? Wale wazee wa Dullah unaona rika lako kabisaaa, wameacha mangapi? Toa kufuli. Nikatoa. Nikamwambia nimetoa. Akampigia Dullah ashatoa embu mpigie nisikie hapa hapa. Simu ikaita.

Nikapokea Halooo! Mjomba sema Haloo mume wangu, sauti laini, wewe unatakiwa kungwi toka kijijini kabisaa, aje na bakoraa hawa makungwi wa mjini hawakuweziii. Nikasema Haloo mume wangu, Dullah bichwa hilooo kama loteee. Niambie mke wangu umenisamehe. Nikajibu Hapana short short mjomba asisikie, Dullah akaniambia nimwambie mjomba wako. Heheheheeee! Tukajikuta tunacheka tu wote. Anasema sasa nakuona llini kimila nilisha nunua zigo hilooo. Nimekamilisha taratibu zoote.

Usiku sasa hongeraaa hongeraaa mpaka watu nishawasahaugi. Kumbe ndoa big deal hivo. Hata nilivopewa umeneja sikupongezwa kiasi hiki. Hongeraa, kila mahali. Ofisini mpaka keki wakaniandalia. Nikaogopaaa. Nikasema hapa Dullah kaniweka kwenye kona, jamii yote inajua nipo nae, sina namna inabidi niwe tu nae. Nilichoogopa kuolewa nae siku date nae. Tumelala once afu ndoa kweli jamani. Nikapanda niazne kumtongoza upya aipeleke harusi mbele maybe we try dating again. Ikishindikana huu moto wa mahari utakuwa umepoa.

Sms kila saa, simu ndo balaa. Ananiambia natamani nimuite shehe nikuoe hata kesho. Namtulizaa, Dullah nashukuru unanioa, unanistiri, lakini my dream wedding sio hio unayoandaaa ya kuja kwetuna shehe, kula ubwaba na kuchukua mke. Dullah me and you tumesomaa, mimi i was thinking something like Dubai. Mimi, wewe na Ellah maybe na kaka zako, na ndugu zangu kidogo. Honeymoon ya kukata na mundu Dubai. Tukirudi Ellah ana mdogo wake. Nampanga tu ndugu msomaji.

Akajaaa. Kama ndo unachokipenda mke wangu, nitazungumza na mzee na familia tuone tunafanyaje. Michango na vikao vya harusi hatuto anza kabisaaa. I want you to be happy on your wedding day, i want to marry the happiest woman on earth.So kama Dubai ndo unataka, then Dubai it is.

ITAENDELEA KESHO
 
Hahahaaaa mjomba mjombaree. Anko ommy kanipa raha sana.
Natamani kumpenda dullah ila huyu lara hatabiriki. Kiboga alichotula kwa Hussein msomali sitakuja kukisahau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom